Maandiko yanasema watatokea manabii na mitume wa uongo nao watakuwa na uwezo wa kuponya wagonjwa, kuhamisha milima hata kufufua wafu, Watatenda miujiza mingi kwa jina langu LAKINI MSIWAAMINI HAO!
Sasa hizi nguvu wanazipata wapi?
Sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu hivyo basi tuna uungu ndani yetu.. Ile nguvu alitumia Mungu ya KUTAMKA na IKAWA kwenye uumbaji ndio hiyo nguvu waliyo nayo hao watu
Na si kwamba wao ni maalum sana la hasha hii nguvu ipo tu duniani na yeyote yule anaweza kuipata na kuimiliki.. Nguvu ya KUTAMKA NA IKAWA
Kinachotokea ni kwamba tunai customize kulingana na kaliba na haiba zetu. Tunaipa majina kama
Nguvu za asili
Nguvu za giza
Nguvu za kutenda miujiza nknk Lakini kiuhalisia ni kitu kilekile