Wachumi tusaidieni, Mtaani hali ngumu fedha hakuna biashara imekuwa ngumu. Pesa iko wapi?

Wadau kwa wanaofahamu nnini kimeipata pesa ya nchi hii mpaka kufikia kupotea kiasi hiki??nnauliza hivi maana huku mtaani kwa mmfano nilitoa shilingi elfu 5000 nikanunua kitu cha sh.500 basi kabla hajapokea hela jamaa akaniambia hana chenchi nikaenda duka la pili,la tatu napo ni
hivo hivo ikabidi ninunue vitu vya shilingi elfu 3 lakini bado jamaa akadai hana chench ya kutosha.
 
Ukienda Kenya ukitoa 1000 kwa kitu cha 200 change hana na uchumi wao upo juu, labda kwetu ni dalili ya kukua kwa uchumi. Mimi sio mchumi ndio maana nikasema huenda. Hii book yetu huenda ikawa pesa nzuri baadae
 
Sasa kama malipo ya mkenya ni makubwa hivyo mbona wanapigana vikumbo kuja Tx kutafuta vibarua? Unatufanya sisi mazezeta siyo? Fanya kazi..
 
Wajuzi wa mambo hebu mtujuze ,nimetembea mikoa na wilaya mbalimbali nimekutana na kilio cha wananchi kuhusu ukata wa pesa mtaani wananchi wanalia sana .Nini chanzo maana binadamu yoyote yule anahitaji chakula , mavazi na malazi ,sasa hata chakula imekuwa Shida kumbuka kina wazee ,watoto ,walemavu na wasiojiweza watafanyaje wakati watu lazima tu mambo magumu ,hii awamu ya tano ndio waliyotuahidi ? au ndio imeshakuwa Zimbabwe .
 
Mtawala ana tabia za kike kila kitu anaweka rohoni tu, na pia kila jambo anakurupuka tu
 
Wajuzi wa mambo hebu mtujuze ,nimetembea mikoa na wilaya mbalimbali nimekutana na kilio cha wananchi kuhusu ukata wa pesa mtaani wananchi wanalia sana .Nini chanzo maana binadamu yoyote yule anahitaji chakula , mavazi na malazi ,sasa hata chakula imekuwa Shida kumbuka kina wazee ,watoto ,walemavu na wasiojiweza watafanyaje wakati watu lazima tu mambo magumu ,hii awamu ya tano ndio waliyotuahidi ? au ndio imeshakuwa Zimbabwe .
Chanzo ni jiwe na poor fiscal policy zake
 
Hili ni Jambo la msingi kabisa, ingekuwa vyema wajuzi wa uchumi waje na ufafanuzi yakinifu kabisa mana hata biashara haziendi kabisa, watu wanalalamika pesa hakuna mtaani
hadi inakuwa kero,
 
Kwani mwanzo walikuwa wanazipatia wapi? Wakwambie kuwa mwanzo tulikuwa tunaenda ofisi ya mtendaji kila ijumaa na kupewa laki moja moja ila siku hizi hatoi.
Na kama walikuwa wanazipata baada ya kufanya kazi, wakutajie hiyo kazi waliyokuwa wanafanya, halafu rudi hapa.
 
Ukiwa na shibe usivimbe kiburi na kumsahau jirani yako mwenye njaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moods yaani mnaunganisha Uzi na huu wa mwaka 2016 tunazungumzia halitete tulionayi sasa Kwa nini msiuache tu .
 
Wasalaam wakauu,

Wengi wetu humu ndani tunamiliki 'vijibiashara' vya kutuingizia sent mbili kila siku.

Wengi watakubaliana nami tangu Magufuli aanze kubana Matumizi na kutumbua majipu Kwa sasa biashara nyingi zimedolola hakuna wateja kabisa! mtu unaweza ukakaa karibu siku mbili hujauza chochote.

Hapa kunauwezokano wa Shilingi imebanwa katikati hapa. Mzunguko wa pesa haupo kwa sasa, Magufuli hebu achia hiyo shilingi.

WACHUMI TUSAIDIANE, MTAANI HALI NGUMU, FEDHA HAKUNA BIASHARA IMEKUWA NGUMU. PESA IKO WAPI?
Pasi bado haijamaliza kunyoosha nchi hadi treni ya Mwendo kasi mradi wake uishe, Majengo yote ya wizara ya huko Dodoma yamalizike ,mradi wa Stieglers gorge umalizike n.k
 
Back
Top Bottom