‘Wachokonozi’ wapandishwa kizimbani Arusha kwa ‘Makosa ya Kimtandao’

‘Wachokonozi’ wapandishwa kizimbani Arusha kwa ‘Makosa ya Kimtandao’

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601
Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko wanaojulikana kama “Wachokonozi” jana Juni 27, 2025 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kushtakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act) na kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na kifungu namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kanuni za Maudhui Mtandaoni).

Baada ya kusomewa mashitaka, Kabalo na Mrindoko walipatiwa dhamana kutokana na makosa wanayotuhumiwa nayo kuwa na sifa ya kupata dhamana na hivyo kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Juni 21 Julai 2025.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Vijana hao walikamatwa Juni 20, 2025 katika Kijiji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoa huo, Justin Masejo alithibitisha kukamatwa kwao
 
Ngoja wakijue kilichomtoa kanga manyoya
 
Jackson Kabalo na Joseph Mrindoko wanaojulikana kama Wachokonozi jana Juni 27, 2025 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kushtakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha taarifa za uongo kinyume na kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao na kosa la pili ni kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kinyume na kifungu namba 116(3)(b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta.

Baada ya kusomewa mashitaka, Kabalo na Mrindoko walipatiwa dhamana kutokana na makosa wanayotuhumiwa nayo kuwa na sifa ya kupata dhamana na hivyo kesi hiyo itatajwa tena kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali Juni 21 Julai 2025.

Watuhumiwa wote wanawakilishwa na mawakili Ally Mhyellah na Simon Mbwambo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).

Vijana hao walikamatwa Juni 20, 2025 katika Kijiji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoa huo, Justin Masejo alithibitisha kukamatwa kwao
Wasikate tamaa
 
Nashauri tu..
Wenyewe si wachokonozi... Wakawachokonoe huko huko
 
Back
Top Bottom