wachina waomba kuwekeza katika umeme na usafiri

ckatai wanaweza kuja kufanya mambo tofaut tofaut na kuja kuiweka nch ye2 pazur ila ckuzote muharibifu wa nch hii c mzungu wala mchna ni mtanzania mwenyewe mana 2takuja kuwawekea vkwazo hata vcvyo na maana nia yao wale wao na vendelee kukaa vkiwa vmehalibika yan hapa ndo tanzania
 
Ingekuwa jambo la maana sa kama wangeomba kuwekeza kwenye uongozi wa nchi (uraisi, bunge, mahakama nk) manake kwao kosa la kifisadi unanyongwa sio hapa bongo unakumbatiwa, wangetusaidia sana kunyonga mafisadi papa kama JK, RA, EL, Zombe, Chenge nk na kurudisha nchi katika mstari na maadili. Baada ya hapo ndio wawekeze kwenye usafiri na umeme.

Hamuoni kama tutakuwa tumepiga hatua sana, yaani hamna rushwa, umeme upo na miundo mbinu ya usafiri ipo.

wachina wawekeze kwenye uraisi na ubunge???!!
Unamaanisha bungeni tuwakilishwe na wachina na raisi wa tz nae awe mchina au?
Huo ni mtazamo wa mtazamaji anaepotea.
 
serikali ya china yataka kuwekeza katika umeme kilimo miundo mbinu na usafiri wa anga nchini.
Wamesema wamekuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina rasilimali nyingi ukilinganisha na nchi nyingine za afrika,
hayo yamesemwa na mshauri mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa China alipokuwa mjini dar es salaam na pia wameisifia mbuga ya serengeti wakaahidi kuwa wataitembelea kabla ya kuondoka:
source:mwananchi.co.tz

Nchi yoyote haiwezi kuendelea inaposuasua kumiliki njia kuu za uchumi. Hivi sasa serikali inasuasua kwa sababu njia kuu za uchumi zinamilikiwa na mafisadi ambao wananufaisha matumbo yao wakati wananchi wanapata tabu. Umeme, mawasiliano i.e. simu, habari etc, usafiri wa reli, usafiri wa anga, Bandari, madini etc. Tanzania haiwezi kupiga hatua hadi itakapochukua hatua madhubuti kuhakikisha njia zote hizo muhimu zinamilikiwa na walipa kodi.

Hata BOT sasa wanafanya kazi za mafisadi badala ya kazi za walipa kodi. Lakini kama kawaida serikali hii ya mkwere haitasikiliza kilio cha walipa kodi, itafanya vile ilivyozoea kusikiliza nguvu za giza na maswaiba wao. kama tulivyosema wakati TRL ilipopewa wahindi, TTCL walipopewa Canadians etc.
 
Wawekeze kwenye umeme! duh kazi kweli kweli, lazima tukubali kuwa wafanyakazi watatoka china, tegemea wabongo kulipwa na kunyanyaswa kama ilivyo makampuni mengine ya kigeni! Tegemea pia kuliwa zaidi na mafisadi.
 
ninavyojua huku China ukipatikana na kosa la kutoa au kupokea rushwa hukumu ni kifo, nina wasiwasi kama serikali ya Tanzania itakubali kusaini mkataba kwani hautakuwa na chakula!! si unajua viongozi wa Tanzania wameweka maslahi yao mbele ndio maana hata mikataba mingine ilisainiwa Bar/hotelini
 
Kwanini kila kitu tufanyiwe?
Kwani tatizo nini?
Hiyo misaada na mikopo tunayopata hatuwezi kuwekeza wenyewe katika hizo sectors??

Jamani si akina Mwakyembe waliwahi omba waruhusiwe wakanunue majenereta kwa ajili ya serikali? Na kwamba hakuna kinachoshindikana? Hivi tumerogwa na nani sisi? Kwa namna hii kweli tunahitaji wasomi? Kama kila kitu tunahitaji watu wengine watusaidie kufikiri? Mbona wakati wenzetu wanakwenda mbele kwa matendo sisi tunakwenda mbele kwa majigambo ya kijinga huku vitendo vyetu vikiturudisha nyuma? Hiki ndicho baba wa taifa letu alichokikusudia pale alipoamua kuiacha rasilimali yetu mpaka tutakapopata wasomi wa kuweza kuisimamia kwa faida? Hoja yangu hapa ni kwamba kamati ya kina Mwakyemba iliwahi sema bungeni kwamba ikipewe cash itaweza kununua majenereta kwa bei nafuu kabisa, mali ya serikali. Kumbe kama watu wakiwa committed tunaweza kuvuka wenyewe kama walivyofanya Senegal.
 
Back
Top Bottom