wachina waomba kuwekeza katika umeme na usafiri

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
serikali ya china yataka kuwekeza katika umeme kilimo miundo mbinu na usafiri wa anga nchini.
Wamesema wamekuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina rasilimali nyingi ukilinganisha na nchi nyingine za afrika,
hayo yamesemwa na mshauri mkuu wa wizara ya mambo ya nje wa China alipokuwa mjini dar es salaam na pia wameisifia mbuga ya serengeti wakaahidi kuwa wataitembelea kabla ya kuondoka:
source:mwananchi.co.tz
 
Hawa watu ni lazima kuwa makini nao sana wataiba kila kitu lakini yote heri kama tutafaudu na uwekezaji wao ruksa kuliko kulala giza kama tupo karne ya ujima. Walitujengea reli hawa watu kwa hivi hope wana nia njema. Lakini wasipewe ardhi yetu wakafanya yao.
 
mkuu si ni bora hawa jamaa waje watuzaishie umeme kuliko mafisadi na dowans yao wanayojipigia danadana huku wananchi tukiteseka? Ingekuwa nchi za mbele hawa wote wasingekuwepo madarakani
 
Nafikiri tuwape wawekeze katika sekta ya umeme na kilimo maana nishati ya umeme ni muhimu sana kwa sasa ambapo tumejikuta katika minyororo na mitego ya Dowans. Katika kilimo hawa jamaa ni hodari sana,watalima tukula na ziada itauzwa nje. Lakini kila kitu kifanywe kwa uwazi na tahadhari kubwa,hatutaki tena mikataba feki.
 
kwanini tusiteseke sasa hivi kwa ajili ya vizazi vyetu ....... we need to empower our self and do all we need for our country .... i am afraid our lovely country is in auction
 
mkuu si ni bora hawa jamaa waje watuzaishie umeme kuliko mafisadi na dowans yao wanayojipigia danadana huku wananchi tukiteseka? Ingekuwa nchi za mbele hawa wote wasingekuwepo madarakani

Nakubaliana na wewe kwa hili.
 
serikali ya china yataka kuwekeza katika umeme kilimo miundo mbinu na usafiri wa anga nchini.
Wamesema wamekuja kuwekeza nchini kwa sababu Tanzania ina rasilimali nyingi ukilinganisha na nchi nyingine za afrika,

Ni vyema, ila tu wasibadilike / kubadilisha nia njema ya kuwekeza katika umeme, miundombinu na usafiri wa anga.
Tunawajua wachina kuwa ndio wanaochimba madini all over Africa na kupeleka kwao kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. So isije ikawa ni mtego wa kutaka kuzoa kwa "kasi zaidi..."
 
lakini kwa kuwa umeme ni mradi wa watu kujipatia hela sidhani kama watakubali kirahisi, kwa sababu toka uhuru mpaka leo sidhani kama hakuna njia zozote zilizowahi kufikiriwa kuwa zaweza kupunguza hili tatizo..,
 
Kama ni serikali ya china hamna shida, maana ina mtaji mkubwa sana na inaweza kuhuisha miradi mingi iliyokufa ikawa na ufanisi.
Nina imani kama ni serikali ya China inahusika hakutakuwa na mizengwe, kila kitu kitafuata kanuni. Hofu ni kuwa viongozi wa serikali yetu hawatakubali kwa kuhofia kukosa maslahi ikilinganishwa na makampuni ya kifisadi yanayoletwa nchini.
 
Ni vyema, ila tu wasibadilike / kubadilisha nia njema ya kuwekeza katika umeme, miundombinu na usafiri wa anga.
Tunawajua wachina kuwa ndio wanaochimba madini all over Africa na kupeleka kwao kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali. So isije ikawa ni mtego wa kutaka kuzoa kwa "kasi zaidi..."

Acha zengwe Mkuu,

Hawa watu si ndio waliowajengea TAZARA, (one of the best railway in Africa) na kuwapa magarimoshi kwa mkopo (baada ya hao wazungu mnaowathamini kuwatolea nje!!!.)

Tena hata huo mkopo wenyewe mkashindwa kulipa na wakaamua kuwasamehe deni...
 
wawekeze katika umeme na kilimo, bonde la kagera linauwezo wa kulisha africa nzima, tukiwapa wachina hilo litawezekana... kuhusu umeme si mbaya tukiwajaribu pia maana hao waliopo sasa ni wevi watupu!
 
Ingekuwa jambo la maana sa kama wangeomba kuwekeza kwenye uongozi wa nchi (uraisi, bunge, mahakama nk) manake kwao kosa la kifisadi unanyongwa sio hapa bongo unakumbatiwa, wangetusaidia sana kunyonga mafisadi papa kama JK, RA, EL, Zombe, Chenge nk na kurudisha nchi katika mstari na maadili. Baada ya hapo ndio wawekeze kwenye usafiri na umeme.

Hamuoni kama tutakuwa tumepiga hatua sana, yaani hamna rushwa, umeme upo na miundo mbinu ya usafiri ipo.
 
Ohh

Wachina...Wachina wawekeze kwenye umeme then waiuzie Tanesco hii siisomi katika angle nzuri...tutaleta mambo hapa after muda flan..hata wakisema ni serikali ya chini bado ni wachina tu.Na kuna haka ka kasumba ka magharibi kuwa wachina na wazungu kufanya kazi pamoja inakuwa ngumu...Tusije poteza wengine kwa kuji engage na wachina...

Halafu wataoa fanya kazi nao wachina nawaonea huruma toka mradi utakapo anza mpaka kwenye production..hawa mabwana Juu ya wingi wao watanzania watateseka sana..kwenye ujenzi wacha tuteseke wakati tunatafuta ufumbuzi then watafaidi vizazi vijavyo...kuliko wapa hawa rasilimali zetu..wataacha empty hii nchi.
 
Hawa ninavyowafahamu mimi (nilikaa kwao miaka 2) hawana mchezo katka kufanya kazi na kutimiza malengo. Tatizo ni kwetu sisi wakati wa kuingia mikataba ya kibinafsi ambayo haitakuwa na tija kwa umma. Umeme utawaka na hakutakuwa na giza kamwe, ila malipo yake tutakoma kwa kuwa jamaa walioko madarakani watachukua 40% badala ya 10%
 
Hawa watu ni lazima kuwa makini nao sana wataiba kila kitu lakini yote heri kama tutafaudu na uwekezaji wao ruksa kuliko kulala giza kama tupo karne ya ujima. Walitujengea reli hawa watu kwa hivi hope wana nia njema. Lakini wasipewe ardhi yetu wakafanya yao.
.. ni heri ya wachina kuliko wazungu.. bado wanatupa na madaktari wao kututibia maradhi... je tuwape kazi ya umeme wazungu walituibia na mpaka leo wanaendelea kutuibia na kutudhulumu bado tunawasifia "wazungu wana akili sana!" tumesahau katika wazungu heri ya wajerumani ambao walitujengea reli ambayo leo kuna wachache bado wanaonufaika nayo!!! Je hatuoni katika migodi wazungu wanachotufanyia?
 
Kwanini kila kitu tufanyiwe?
Kwani tatizo nini?
Hiyo misaada na mikopo tunayopata hatuwezi kuwekeza wenyewe katika hizo sectors??
 
Back
Top Bottom