Wachina wakamatwa na Shehena ya Meno ya Tembo Bandarini Dar

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Japo naiweka kama tetesi ila napenda ifahamike kuwa ukweli wake utajidhihiri muda si mrefu.

Tetesi yenyewe ni kuwa Kuna Wachina wamekamatwa na Shehena Kubwa ya Meno ya tembo Bandarini Dar na sasa wamechukuliwa kisiri na "watu flani" ambao hawataki habari hii ijulikane.

Napenda kuviarifu vyombo vyetu vya dola kuwa makini na "watu hawa flani" kwani wananchi hatutakaa kimya endapo hili litanyamaziwa.

Namna yoyote ya kuzima huu ujangili italeta balaa kubwa si kwa vyombo vya dola tu bali hata kuitia doa serikali kwa ujumla. Msifiche, waanike ili waueleze umma nani yupo nyuma yao!

Happy New Year 2014!

========
UPDATE:

Ili wajue tumeshajua na si siri na kiasi cha "mzigo" tunajua, naongeza data:

Ilikuwa ni meli ya kijeshi ya China ambayo ilikuwa imeegesha gati namba 3 baada ya kuwa nchini katika shughuli za kawaida za ushirikiano katika kudhibiti maharamia (Pirates). Katika kuuficha mzigo kwa kudai magari yamebeba chakula ndipo wakashtukiwa.

Chanzo chetu kinatufahamisha kuwa Wametiwa pingu na wanajeshi wa JWTZ na TISS na wamepelekwa Ukonga na msafara wa magari mawili yakiongozwa na pikipiki za Polisi.

Hata walipo tuna chanzo chetu ambacho kitaendelea kutujuza kinachojiri.

Kutoka chanzo chetu - wajaribu kuhonga, wakutwa na Tanzanite pia!:
 
Funga mwaka hio jamaa ujue wanataka wapige pesa kesho watusumbue kwenye Bar. Nadhani we need to intervene kuwasubiri wawataje ni kupoteza muda na kuja kupewa hadithi kama za akina Masogange kuwa hayakua madawa ya kulevya. Utaambiwa sasa hivi kuwa walibeba mbao...
 
wananchi wote tupaze sauti hawa wachina hawawezi kuruhusiwa kumaliza tembo wetu kwa vipamde vya thumuni container tano haiwezekani wananchi paza sauti paza sauti wote tuseme hapana kontena tano tembo gani wamebaki haiwezekani taarifa zisambazwe vyombo vya ndani na nje
 
Invisible motto ya JF inasemaje inakuwaje mtu jama wewe unauhakika na taarifa halafu unaileta kama tetesi halafu unataka tukuminisha au lengo lako nini? je unaogopa ya Abdallah Shimbo na trillion zake 3 huko sauth Africa..acha uoga, funguka zaidi
 
Last edited by a moderator:
katiba mpya ipige marufuku watu wa jamii ya kichina kuingia nchini , ikiwemo kufunga hata ubalozi wao .
 
Wanyongwe hadharani,

Hii operesheni tokomeza irudi tu tena kwa nguvu zaidi

Mimi mwenyewe nimesikia hii habari kutoka vyanzo ninavyoviamini sana
Kwa sheria ipi? Watueleze ni nani anayesaidiana nao kwenye hii biashara.
 
hawa marafiki wa ccm wanadhani tutawaangalia tu jamani wote tuseme wachina bye bye wabaya hawa
 
Nhnnn...so hiyo meli ya kichina ilipiga nanga hapo mwambaoni kutulizisha kuwa tuko salama? Shimbo arudishwe haraka kutoka china. Huu ujangiri umeratibiwa na serikali ya ccm. Juhudi za tokomeza ujangili ni kiini macho. Waliotumwa kazi hiyo walifanya 'surbotage' ilikieleweke.

Wananchi tuchukue hatua wenyewe la sivyo meno yatazidi kukusanywa na kupelekwa China...yupo anayeratibu hiyo hukohuko kwa faida ya magamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…