Wachina wakamatwa na Shehena ya Meno ya Tembo Bandarini Dar

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,108
2,000
Wakuu,

Japo naiweka kama tetesi ila napenda ifahamike kuwa ukweli wake utajidhihiri muda si mrefu.

Tetesi yenyewe ni kuwa Kuna Wachina wamekamatwa na Shehena Kubwa ya Meno ya tembo Bandarini Dar na sasa wamechukuliwa kisiri na "watu flani" ambao hawataki habari hii ijulikane.

Napenda kuviarifu vyombo vyetu vya dola kuwa makini na "watu hawa flani" kwani wananchi hatutakaa kimya endapo hili litanyamaziwa.

Namna yoyote ya kuzima huu ujangili italeta balaa kubwa si kwa vyombo vya dola tu bali hata kuitia doa serikali kwa ujumla. Msifiche, waanike ili waueleze umma nani yupo nyuma yao!

Happy New Year 2014!

========
UPDATE:

Ili wajue tumeshajua na si siri na kiasi cha "mzigo" tunajua, naongeza data:

Ilikuwa ni meli ya kijeshi ya China ambayo ilikuwa imeegesha gati namba 3 baada ya kuwa nchini katika shughuli za kawaida za ushirikiano katika kudhibiti maharamia (Pirates). Katika kuuficha mzigo kwa kudai magari yamebeba chakula ndipo wakashtukiwa.

Chanzo chetu kinatufahamisha kuwa Wametiwa pingu na wanajeshi wa JWTZ na TISS na wamepelekwa Ukonga na msafara wa magari mawili yakiongozwa na pikipiki za Polisi.

Hata walipo tuna chanzo chetu ambacho kitaendelea kutujuza kinachojiri.

Unachosema mkuu ni kweli, hii habari nilipewa leo asubuhi na jamaa yangu anayefanya kazi bandarini.

Sio tetesi ni ukweli mtupu!

Nafikiri mambo haya yanatokea wakati muafaka kabisa, wakati tunaandika katiba mpya. Watanzania wote tushirikiane na kuhakikisha inawekwa sheria ya kunyongwa mpaka kufa au kifungo cha maisha without any possibility of parole kwa watu wote wanaopatikana na hatia ya kufanya biashara ya pembe za ndovu/ujangili pamoja na wanaouza madawa ya kulevya!
Kutoka chanzo chetu - wajaribu kuhonga, wakutwa na Tanzanite pia!:
Sakata la Wachina na kukutwa na Nyara za Serikali limeendelea kuchukua sura mpya ambapo Wachina wawili walifika bandarini wakitaka kuwasailimia ndugu zao ambao ni Wanajeshi.

Walipofika getini, kwakuwa tayari wanajeshi wa JWTZ waliishaimarisha ulinzi baada ya tukio la jana yake (usiku wa kuamkia leo) na meno ya tembo. Wanajeshi walitaka kuwakagua Wachina hao wakagoma na ndipo wakapekuliwa kwa lazima na kukutwa na madini aina ya Tanzanite. Wakaitwa maofisa wa Nishati na Madini na polisi wakawachukua!

Tukio la awali lilikuwa la jana Jumatatu saa 3 usiku wa kuamkia Jumanne (leo) ambapo gari moja binafsi likisindikizwa na gari la Polisi na mtu mmoja mwenye sare za Polisi lilifika katika lango la bandari eneo la geti namba 2 wakielekea geti namba 3 iliko meli ya kijeshi ya Kichina yenye wanajeshi takribani 600.

Katika gari la kiraia kulikuwa na Wachina watatu; wawili wanajeshi na mmoja raia na dereva Mtanzania.

WACHINA walitaka kuwapa walinzi rushwa ya sh milioni 25 baada ya walinzi kukuta kuna vipande 81 vya meno ya tembo.

Walinzi waligoma na kulazimisha kulikagua gari. Kuona hivyo gari la Polisi na mtu aliyevaa sare za polisi wakatoweka na wale wanajeshi wawili wa Kichina wakatoweka na kukimbilia katika meli yao ya kijeshi na kujichanganya na wenzao.

Ndipo walinzi walipowasiliana na wanajeshi na Polisi na wakaja wanajeshi na maofisa Usalama wa Taifa wa Tanzania ambao waliwachukua Mchina na dereva Mtanzania na kuondoka nao.

Tunaendelea kufuatilia zaidi kuwafahamisha kinachojiri
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,109
2,000
Funga mwaka hio jamaa ujue wanataka wapige pesa kesho watusumbue kwenye Bar. Nadhani we need to intervene kuwasubiri wawataje ni kupoteza muda na kuja kupewa hadithi kama za akina Masogange kuwa hayakua madawa ya kulevya. Utaambiwa sasa hivi kuwa walibeba mbao...
 

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,295
0
wananchi wote tupaze sauti hawa wachina hawawezi kuruhusiwa kumaliza tembo wetu kwa vipamde vya thumuni container tano haiwezekani wananchi paza sauti paza sauti wote tuseme hapana kontena tano tembo gani wamebaki haiwezekani taarifa zisambazwe vyombo vya ndani na nje
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000
Invisible motto ya JF inasemaje inakuwaje mtu jama wewe unauhakika na taarifa halafu unaileta kama tetesi halafu unataka tukuminisha au lengo lako nini? je unaogopa ya Abdallah Shimbo na trillion zake 3 huko sauth Africa..acha uoga, funguka zaidi
 
Last edited by a moderator:

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,044
2,000
katiba mpya ipige marufuku watu wa jamii ya kichina kuingia nchini , ikiwemo kufunga hata ubalozi wao .
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Wanyongwe hadharani,

Hii operesheni tokomeza irudi tu tena kwa nguvu zaidi

Mimi mwenyewe nimesikia hii habari kutoka vyanzo ninavyoviamini sana
Kwa sheria ipi? Watueleze ni nani anayesaidiana nao kwenye hii biashara.
 

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,295
0
hawa marafiki wa ccm wanadhani tutawaangalia tu jamani wote tuseme wachina bye bye wabaya hawa
 

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Nhnnn...so hiyo meli ya kichina ilipiga nanga hapo mwambaoni kutulizisha kuwa tuko salama? Shimbo arudishwe haraka kutoka china. Huu ujangiri umeratibiwa na serikali ya ccm. Juhudi za tokomeza ujangili ni kiini macho. Waliotumwa kazi hiyo walifanya 'surbotage' ilikieleweke.

Wananchi tuchukue hatua wenyewe la sivyo meno yatazidi kukusanywa na kupelekwa China...yupo anayeratibu hiyo hukohuko kwa faida ya magamba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom