Wachimba dawa kituo cha Makambako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachimba dawa kituo cha Makambako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magane, Sep 20, 2011.

 1. M

  Magane Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Niko ndani ya moja ya mabasi yaendayo Dar kutoka Mbeya mara basi linasimama na konda anawaambia abiria " jamani mkachimbe dawa , msichelewe ni kwa muda wa dakika tano tu" basi kila abiria anatoka haraka kwenda nje ya basi kuelekea uchochoroni. Utararibu ni kwamba akina baba wana mwelekeo wao na kina mama hivyo hivyo na ni marufuku kwenda kinyume. Sasa wana jf nilichojionea kule uchochoro ni kwamba kumechimbwa mashimo kina na diameter ni kama ft moja halafu kumefagiliwa wacha tu.Baada ya hapo unasikia tena konda akiwahimiza abiria wangie ndani ya basi.Ninachotaka kupoint out ni kwamba watu wakiamua wanaweza wakajiongoza wenyewe bila hata katibu kata au mwenyekiti wa mtaa kuwasimamia katika jambo lao la maendeleo.Kumbuka pale kituoni pana biashara za bites na vinywaji baridi.Kweli wanawajali wateja wao.
   
 2. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  umeposti hii thread baada ya kuchimba dawa, au siyo?
   
 3. N

  NIMIMI Senior Member

  #3
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Upele umemfika mkunaji!
   
 4. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Uchafuzi wa Mazingira!.
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Hivi pale kuna maji kweli???
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni uchafu tu na kudhaliisha abiria wengine hasa akina mama. mahali pale huwa hapana maji wala privacy ya kutosha.
   
 7. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kuchimba dawa ndo kitu gani???
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani hawawezi kusimama shm ambayo ina vyoo kwa ajili yakutunza mazingira?
   
 9. Mghoshingwa

  Mghoshingwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Ni neno lenye tafsida linalo maanisha kujisaidia. Neno hili ni maarufu sana wakati wa safari ndefu za kutumia bara bara hasa kwa kutumia mabasi.
   
 10. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mabasi mengine bwana,Dar-Mbeya,kuchimba dawa mara nne,panda Happynation,tunachimba dawa Aljazeera tu.
   
Loading...