Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,459
- 29,157
Hivi Karibuni Mchezaji Dejan alipofunga goli Mashabiki wengi wa Simba tulifurahi sana. Sababu ya kufurahi ni kua toka asajiliwe Mchezaji huyu hakua amefunga goli kwenye mechi yoyote ile ukiacha mazoezini labda.
Wengi tulianza kuamini kua Mchezaji huyu "tumepigwa", wengine kufikia kusema aheri ya Meddy Kagere na Chris Koppe Mugalu walioondoka kuliko Dejan Mzungu.
Kwa kua mechi zilizopita hakucheza dakika zote 90 sikuweza kumuangalia Kwa mapana zaidi, lakini jana ndio nimemuona vizuri kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Al Hilal.
Wachezaji wenzake hawakua wakipeleka mipira kwake ipasavyo, wangeweza hata kurudisha mipira nyuma kuliko kumpasia yeye.
Alikua akikimbia sehemu mbalimbali, kati, kushoto na kulia ili aweze kupewa mipira lakini haikua hivyo. Ni kama vile Wachezaji wenzake hawamuamini au wanamfanyia mtimanyongo.
Yaani mmepangwa Wachezaji 11 uwanjani wa timu mmoja lakini Wachezaji wenyewe wanaamua kucheza 10 kwa kumfanya mmoja wao kama mfanya mazoezi tu. Ataanza mechi, atakimbia kimbia, atatoka jasho, na halftime atarudi tena lakini ukimfanyia assessment unagundua dakika zote 90 hakua na any impact.
Hii inaweza isiiathiri timu kama inacheza na timu yenye kiwango kidogo kuliko Simba (dhaifu) lakini kwa mechi kubwa italeta madhara. Manake mtajiona kwa number mko 11 ki nadharia uwanjani kumbe wanaotumika ni 10 tu kivitendo.
Ni wakati sasa Wachezaji waitwe waulizwe wana shida gani na Dejan mpaka wanaamua kutomtumia. Inawezekana ni roho mbaya zetu tu watu weusi, au Dejan pamoja na kuji-position sehemu mbalimbali lakini wenzake wanamuona labda hayuko eneo zuri la kupewa mipira (offside au amekabwa).
Ni vizuri kuongea hili mapema kuliko kuendelea kufuga tatizo. Huu ni mtazamo tu.