Wachezaji wa Mashujaa kulamba Milioni 100 wakimfunga Simba

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
19,232
Reaction score
68,262
Wachezaji wa Kikosi cha Mashujaa FC wamewekewa kiasi cha shilingi millioni 100 kama wataifunga Simba SC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utachezwa Ijumaa Mei 2.

Wachezaji hao wameahidiwa milioni 100 kwa ushindi na milioni 50 kwa sare dhidi ya Simba SC.

Source: Nassib Mkomwa kupitia ukurasa wake wa X zamani twitter
 
Wawafunge mabingwa wa Africa?
 
Kwa mtindo huu sisi Yanga tutaendelea kucheza Mapinduzi cup huku Simba akicheza mashindano ya CAF kila mwaka na kufika hatua za fainali.
8CB26019-E92F-49AE-A2D7-69B49E3A9B98.jpeg
 
Kwanza sitaki kuamini kama ni kweli naona hii ni propaganda tu. Lakini kama ni kweli basi kuna shida mahali. Hivi ukizihesabu hizi ahadi kama ni kweli na kama anayetoa ni mtu yule yule tunayeambiwa kila siku basi nafikiri anahitaji maombi. Ukizijumlisha hela zote tunazoambiwa ametoa kwenye timu pinzani zinazocheza na Simba tokea ligi imeanza basi angeweza kufanya yafuatayo:-
1. Kusajili washambuliaji wawili wakali sana ambao wangeisaidia sana timu yake iweze kushinda mechi zote za ligi bila kupata sare au kufungwa. Na hii ingesaidia timu yake kuziacha mbali sana timu nyingine kwenye msimamo wa ligi.
2. Hizo pesa angewapa benchi la ufundi na wachezaji wa timu yake kama motisha kwa kila mechi itakayoshinda nina hakika wachezaji wa timu yake wangefia uwanjani wakitafuta ushindi.
3. Kutenga kiasi kikubwa cha pesa cha kununua magoli kwenye timu yake na angeita zawadi hiyo goli la raisi wa timu.
4. Chenji inayobaki angewapelekea watoto yatima ili apate baraka kwa Mungu.

Ni mtizamo tu.
 
Nadhani haujaelewa dhana nzima ya kufanya hivi. Hiyo pesa haitoki mpaka matokeo wanayoyataka yamepatikana. Simba na Yanga hazipotezi sana mechi. Hapa Yanga wanatafuta mechi moja tu Simba itoke sare au ifungwe ili wajitangazie ubingwa kwa hiyo watoa ahadi wanajua pesa itakayoweza kuwatoka haizidi hiyo milioni 100.

Niliwahi kumshauri Mo atenge milioni 500 kukabiliana na hili.

Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena
 
Wachezaji wa Kikosi cha Mashujaa FC wamewekewa kiasi cha shilingi millioni 100 kama wataifunga Simba SC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambao utachezwa Ijumaa Mei 2.

Wachezaji hao wameahidiwa milioni 100 kwa ushindi na milioni 50 kwa sare dhidi ya Simba SC.

Source: Nassib Mkomwa kupitia ukurasa wake wa X zamani twitter
Kiherehere
 
Siamini kama jeshi letu linaweza kuchezea pesa kiasi hicho.
Huyu ni yule yule anayekerwa na mafanikio ya Simba ndiye anayetapanya mapesa hayo.
 
Kwa hiyo Simba ina thamani mara 2 ya Yanga. Maana siku wanacheza na Yanga dau lilikuwa mil 50 tu
 
Back
Top Bottom