Wachezaji 5 waliochemka mpaka sasa 2019/2020 premier league

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
1. Willian Borges.
Mashabiki wa Chelsea lazima wafadhaike na utendaji wa Willian msimu huu. Mbrazil huyo aliaminiwa na mashabiki wa Chelsea kwamba ndio wakati wake wa kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na mchezaji wao pendwa Eden Hazard. Waliamini ndio muda wake, ni muda wa kumkabidhi moyo wa Hazard. Mambo yamekuwa tofauti dhidi yake, ameshindwa kuwapa walau hata ya robo alichokuwa anawapa Hazard.

Akiwa na umri wa miaka 31 kwasasa mambo hayaendi sawa pale darajani na kuna taarifa kuwa unaweza kuwa msimu wake wa mwisho huu pale Stamford bridge. Kabla ya msimu huu kuanza Barcelona walifika bei ya kutaka kumnunua kwa Pauni Mil 40,lakini Chelsea walikataa ofa hiyo na kuendelea kumtumia.

kutokana na kiwango chake duni alichokionyesha msimu huu sidhani kama Barcelona watakuwa na mahitaji nae ya kumnunua tena. Katika msimu huu amefanikiwa kucheza michezo 28,kafunga magoli 5 na kutengeneza mengine matano.

100583613_1644180109063351_4112626984889090048_n.jpg



2. Tanguy Ndombele
Mchezaji huyu wa kimataifa kutokea Ufaransa alihamia ligi kuu ya Uingereza na jina kubwa sana kutokea Lyon ya nchini Ufaransa akiwa kijana kabisa na umri wa miaka 23.Tottenham ilishinda katika vita ya kumsajili mchezaji huyu baada ya kuvishinda vilabu kama Manchester united ambayo nayo ilikuwa ikimnyemelea kwa ukaribu sana. Lakini karibu miezi nane aliyokuwa Spurs mpaka sasa ametoka kuwa mchezaji bora na kuwa mchezaji wa kawaida sana.

Na hata hana namba ya kudumu Spurs Jose Mourinho naona hana mipango nae muda mwingi amekuwa akimtumia sana Harry Wings na Moussa Sissoko katikati ya uwanja.

Hakika kwa Spurs huu unakuwa moja ya sajili zao za kawaida sana kwa mchezaji aliyekuja na kujaa na mbwembwe nyingi sana ndani yake, ila kila siku nasema muda ni rafiki sahihi sana wa maisha ya binadamu tusubiri tuone labda msimu ujao anaweza kutupa kitu sahihi katika miguu yake.

skysports-ndombele-tottenham_4745275.jpg




3. Nicolas Pepe
Ndio mchezaji Ghali kabisa katika historia ya klabu ya Arsenal. Lakini bado hajaanza kabisa kuonyesha thamani ya pesa walioyotoa arsenal kumnunua ya Pauni million 72 majira ya joto. Alitarajiwa kwenda kuongeza nguvu katika kikosi cha Arsenal pale mbele lakini mambo yamekuwa tofauti katika msimu wake huu wa kwanza.

Mchezaji aliye sajiliwa kwa gharama kubwa anatakiwa aje na kitu cha ziada kwaajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chake kuliko kiwango anachoonyesha sasa hivi. Katika michezo yake 24 aliyocheza katika ligi amefanikiwa kufunga mabao 4 na kutengeneza mengine saba, sio rekodi nzuri kwa mchezaji wa kiwango chake aliyetoka Lile ya ufaransa akiwa kama mfungaji namba mbili nyuma ya Mbappe. Muda bado anao wa kuwapa thamani halisi mashabiki wa Arsenal has a kutokana na kiwango cha pesa kilicho tolewa juu yake.

RexArsenalvOlympiacosFCUEFAEu10569102AKjpg-JS566722165-2-e1590343850726.jpg




4. Callum Hudson-Odoi
Moja kati ya wachezaji waliopewa matarajio makubwa katika kikosi cha Chelsea ni Odoi, lakini mashabiki wameanza kumzoea. Akiwa kinda kabisa wa miaka 19 alianza kuushangaza ulimwengu na soka lake la kuvutia akiwa na kasi ya ajabu sana na iliwapelekea mpaka Bayern Munich kuanza kuhitaji sahihi yake akawe mrithi wa Frank Ribery upande ule wa kushoto. Ghafla ndoto imezima, labda kutokana na majeraha ambayo yamekuwa yakimsumbua mara kwa mara.

Frank Lampard bado ana imani nae na yupo kwenye mipango yake, kipaji anacho ila ameshuka sana kiwango na matarajio ya watu wengi hasa wapenzi wa Chelsea katika msimu huu. Tumsubiri msimu ujao anaweza atakuonyesha maana halisi ya mchezaji bora.

p209046.png




5. Harry Maguire
Kwa mchezaji alisainiwa kwa kiasi cha pauni milion 80 unategemea kupata kitu kilicho bora zaidi kwa upande wake, japo sina maana kwamba sio bora. Mchezaji huyu wa kimataifa wa Uingereza alitua Old Trafford mashabiki wa Manchester united walikuwa na matarajio mengi kutoka kwake japo uwepo wake umebadili kidogo hali ya ulinzi pale nyuma. Ushirikiano wake na Lindelof umevunjwa kwa urahisi sana msimu huu ambao bado haujamalizika.

Ubora wake ni Undoubted, lakini kwa Manchester united bado hajauthibitisha. Ndio mlinzi ghali zaidi duniani, lakini katika uwanja hasa katika viunga vya Old Trafford bado hajalithibitisha hilo, akiwa na umri wa miaka 26 hadi sasa.

Mchezaji wa zamani wa Leicester city Realguard alisema ni muda wa Maguire kuonyesha au kuthibitisha ubora wake aliokuwa nao kutoka Leicester na kuwapa Manchester united waone kiwango walichotoa kinaendana na thamani ya mchezaji.

0_Manchester-United-v-Leicester-City-Premier-League-Old-Trafford.jpg





By Gascoigen Brian
Ista Mrope_10
 
Kwa Ndombele sawa ila kea wengine umewaonea Willian amecheza vizuri Sana na ametoa mchango mkubwa tu ndani ya Chelsea ila shida yako Ni kumshindanisha Hazard ndo maana umemuona amechemka. Hazard yupo unique na hakuna mchezaji yoyote ndani ya EPL unaweza kumfananisha na Hazard.
 
Back
Top Bottom