Wachawi wanikosesha usingizi usiku wa leo

Kweli ila ushauri wa kuolewa naona hajauchukulia seriously, hapa tatizo lake ni uoga tu. Uoga wake unapelekea aanze ku hallucinate, kuona mambo ambayo hayapo. Akiishi na mtu iwe mme au ndugu uoga utapungua na hiyo hali itaisha.

Waafrika tumeharibikiwa kwa kudhani kila kitu ni uchawi ilhali uchawi wenyewe haupo.
 
Pole sana
Bora umeoneshwa mtu unaemfahamu
Wengine hua tunaomba sana tuonyeshwe mtu anaeipiga familia lakin wapi
Cha msingi hapo anza kuchukua hatua mara moja
Kama ni kuomba ushaur wa kiroho zaidi kutoka kwa mchungaji wako itakua jambo la heri
 
Mmmhhh kumbe loh hii nimesikia Leo kitimoto alivyo tamu kumbe dawa
Naaam mkuuu hapo wachawi na majini hawakufati kabisa.Nyingine vuta cha ARUSHA.

Post sent using JamiiForums mobile app
 


Baadaye niliacha kujibu post zake nikabaki kuangalia jinsi anavyo-react.Kuna kitu nilikigundua baadaye nyuma ya post yake.Huyu ni mdada ambaye yuko umri wa kuolewa na bahati mbaya hajafanikiwa.Angekuwa na mtu kwa matukio kama hayo lazima angemuita mwenzi wake ili aje wawe wanalala pamoja.Wanawake ni viumbe wajanja sana wakati mwingine.Huyu mleta mada ametumia njia hii ya wasilisho la mada ya kukumbwa na "mauzauza" kama njia ya kutafuta mwenzi wa ndoa.Wasomaji wanaume jiongezeni.Amechoshwa na upweke! Wenye nafasi itumieni.Sungura huyo amekaa mkao wa kuwindwa.
 
Mweee me nlijua mwishoni utasema kwa usumbufu huu nimeamua kuokoa kumbe bado!!

~Biblia inasema imani bila matendo imekufa,km una mwagia maji ya baraka na huna imani ww huna kitu na ndio mana unahisi uliyafungulia maana huna IMANI.

~Kuombewa tu haitoshi,amua sasa mwamini YESU,weka nae agano la haki.
Biblia inasema"wote walio mpokea aliwapa uwezo (haki) ya kuwa wana wa Mungu"halafu utaona baada ya hapo YESU nn ana fanya maishani kwako.

~Hakuna kingine dawa ni KUOKOKA tu

Sent from my SHV-E250S using JamiiForums mobile app
 


Dawa sio "kuokoka"! Suluhisho ni wadada wenyewe kuwa na mienendo mizuri mbele ya vijana wa kiume na wanaume ili muweze kuposwa na kuolewa.Jingine ni vijana wa kiume na wanaume wa kikweli kweli (wasioathiriwa na hisia zitokanazo na wingi wa homoni za kike) kuwalindeni.Wawe karibu nanyi kwa kuwapeni psychological consultancy.
 
Ikiwa biblia imezungumzia kuwa uchawi hupo zaidi ya mara 10 halafu unasema uchawi haupo sijui unasoma biblia gani? au unayako umeitunga. mtu mwenye shida ya Maluwe luwe Hallucination kuna mtu anayejua chanzo hicho atupie sasa?
 
Ikiwa biblia imezungumzia uchawi zaidi ya mara 10 halafu unasema uchawi haupo sijui unasoma biblia gani? au unayako umeitunga. mtu mwenye shida ya Maluwe luwe Hallucination kuna mtu anayejua chanzo hicho atupie sasa?

Aiseee....kwamba biblia...hiyo biblia ameiandika nani?
 
Kumbe wewe ukisali naomba kitu kimoja? Polee
 
Kumbe wewe ukisali naomba kitu kimoja? Polee

Sijasema usali kwa kuomba kitu kimoja tu Bali na-discourage kuomba kwa ajili ya vitu visivyokuwepo.Ni kupoteza muda kuomba dhidi ya uchawi,majini,mikosi na au laana.Mambo hayo hayapo na hivi ku-concetrate nayo ni kupoteza nafasi na nguvu zako.
 
Pole pamoja na kuhudhuria Maombi
Soma biblia pia, na uwe na mistari ya kusimamia.
 
Ukiona kitu kama hicho it's damu ya yesu, njoo kesho ubungo Emaus kituo cha karesmatik kuna kongamano limeanza,muda SAA 3 had sits unafanyiwa deliverence na SAA 8 had 12 ndo Luna kongamano lenyew mahubir na maombez
Ushauri mahususi kabisa
 
Wenzako ikifika usiku ni marufuku Kulitamka neno CHUMVI,
huwa tunaita MUNYU,
sasa wewe ita chumvi uje ulale na mazonge...( nimetoka ndani mada maramoja, ila nitarudi baadae)
😀😀
 
Pole mno ila mawazo pia yanachangia kupata mauza uza
 
Umekuja kututangaza humu, ss leo ndio hutolala $#$#@$$$*/('*@!

Post sent using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…