Wachawi wanikosesha usingizi usiku wa leo

Chakorii

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
18,785
Reaction score
51,527
Na imani nyote ni wazima,

Moja kwa moja kwenye mada.

Ndugu zanguni, hapo kabla nilikuwa nilikuwa siamini kuna wachawi ingawa nilikuwa nikisikia watu wakisema. Hapo kabla nilikuwa nikiota ndoto mbaya sana na wakati mwingine nikijikuta natoka nje bila kujua usiku wa manane wakati huo nakuwa siko ktk hali ya kawaida kabisa, naweza kusema ni Mungu tu.

Ile hali ya ndoto mbaya ikawa inazidi nikaanza kwenda kwenye maombi. Nilipoanza maombi ni kama nilizidisha nilikuwa nikiota ndoto mbaya nyingi zikiwa za mijoka mikubwa yenye rangi ya gold na yellow nikalifikisha kwa mchungaji nikafanyiwa maombi ile hali ikawa inapotea kidogokidogo ikafikia hatua naota mara chache sana kwahiyo nikawa najisimamia mwenyew kukemea hizo ndoto.

Jana usiku nikawa namsikiliza Mwakasege saa tatu usiku (huwa ni utaratibu wangu wa kusikiliza mahubiri yake) lakini jana ile anaanza nikapata usingizi ghafla nakuja kustuka anamalizia nikalala.

Sasa usiku wa saa saba hivi usingizi ukakata kabisa lakini nikawa nasisimkwa mwili isivyokawaida, najionea giza tu hapo niko macho kumbuka baadae nikawa naona uso wa mtu ila una jicho moja lipo katikati ya kipanda uso na majitu kama mazombi ya kwenye movie hee! Ikabidi kiamke nikatoka nje niwaamshe majirani ikumbukwe sina usingizi kabisa na wala sipo ndotoni.

Wakati naelekea kuwaamsha majirani nikakumbuka nina maji ya baraka ndani ikabidi nirudi nijimwagie maji ya baraka kitanda na sehemu zote za chumbani nikarudi kulala, yani ni kama nimeyafungulia sasa yakaja upya na makucha juu ila kwa sasa yalikuja kama vile naota lakini niko macho kabisa, mwili mzima ulikuwa unasisimka upande wa kushoto na kulia naona giza kabisa kweli niliogopa sana.

Kilichonichanganya zaidi ni ule uso wa yule mtu ni sura ya mtu ninaemfahamu tena ni mtu wangu wa karibu kabisa na mimi kweli katika hali ya kibinadamu naogopa jamani wakati mwingine naogopa hata kuingia ndani jamani.

Poleni kwa urefu wa uzi, nimeona nishee nanyi hiki kilichonisumbua usiku wa leo.
 
Wenzako ikifika usiku ni marufuku Kulitamka neno CHUMVI,
huwa tunaita MUNYU,
sasa wewe ita chumvi uje ulale na mazonge...( nimetoka ndani mada maramoja, ila nitarudi baadae)
 
naona maimuna, makata, kashikashi, subiani, walikuwa wageni wako, anyway..
ilinitokeaga kipindi hivi ikawa nikiomba kabla ya kulala hali ndo ikawa mbaya zaidi usiku, lakini siku nilizolala bila kuomba nilipiga usingizi murua kabisa,
my take;
usianzishe vita na mapepo/ maruhani kama una imani haba
 
Kwanini ulipoona hizo sura huku kemea tena ,wakati unajua kabisa kuwa bila ya kumkaribia Mungu unatoa mwanya kwa mapepo na wachawi kukuchezea.
 
Hayo maji ya baraka ndo yanakuletea hayo mauzauza,believe me

Sent from my G7-L01 using JamiiForums mobile app
 
Pole Sana hali hizo zinaweza kutokea.

Ila, hayo uliyoyaona na ndoto hizo zinataka kutumika kukukosanisha na watu wako wa Karibu.

Mfano, jitu lenye jicho moja linabeba sura ya rafiki /mtu wako wa Karibu.

Ushauri wangu kwako, jaribu kuwa makini na lifestyle yako mengine mbwembwe tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…