The Counseller.
Member
- Aug 13, 2015
- 94
- 75
Wanajamvi ndugu yenu nimefiwa,
Nina majonzi sana na hasira kali moyoni mwangu, mke wangu alijifungua juzi saa 2 usiku katika hospitali ya wilaya ya Maswa, mtoto alikuwa wa kike na mwenye afya njema, mzuri wa sura na mchangamfu sana.
Jana mida ya saa 4 usiku tukashangaa kumkuta mtoto kalegea na anatokwa damu masikioni na mdomoni na hakuwa akihema, ikabidi tumkimbize hospitali haraka sana, kufika hospitali tukaambiwa ameshafariki dunia, sikumuuliza Dr ni nini kimemuua mwanangu nilikuwa nimechanganyikiwa, kufika nyumbani mwanangu sura yake ilikuwa imebadilika kabisa na siyo yake.
Mchana wa leo wakati maiti inaandaliwa kuvikwa sanda tumeona mambo yasiyo ya kawaida katika mwili wa mwanangu, mwili wake katika sehemu za mbavu umetobolewa tobolewa na kubadilika rangi ikawa kahawia, kucha zake zote zimekuwa nyeusi kama aliyevilia damu, mwili wake ni wa moto kama vile yu hai.
Wakati alikufa tangu jana usiku, amebadilika na kuwa mweupe kupindukia, nimemzika mwanangu kwa majonzi sana, naapa lazima nitalipa kisasi, roho inaniuma sana ndugu zangu, sina niliyemkosea.