Wachambuzi wa soka wa Kitanzania na Simba

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,513
12,862
Wakuuu Habari za wkend,

Kuna hili suala la Wachezaji wanaokaa Benchi pale Simba yaani Akina Ajibu, Ndemla, Morrison, Gadiel nk nk
Lakini kule Yanga napo kuna akina Zawadi Mauya, Ninja, Wazir Junior, Boxer nk nk.

Kwanini Wachambuzi wa Soka wanaumizwa na kukereketwa saana na kuwasema zaidi Wasugua Benchi wa Simba, utaskia wanamwambia Ndemla Ondoka Simba, Ajibu kutoka kuwa kapteni mpaka kukaa benchi Simba, ondoka hapo!

Hivi nyinyi wachambuzi mnapoitazama Simba mnakuwa na makengeza yanayowazuia kuona timu zingine? Mlishindwa kushauri Usajili wa akina Raphael Daudi, akina Buswita, akina Mwashiuya, akina Bahanuzi, akina Busungu nk nk nk kisa tu mimacho yenu kutwa kucha ni kukosoa machaguo ya Wachezaji wanaotua Simba na mwishowe wanaosajiliwa huko kwingine hamuoni wanavyopoteza Vipaji vyao. Badilikeni muwasaidie wachezaji wote.

Paul Boxer wa Yanga yuko wapi? Mbona hamuuulizi kwanini hapewi nafasi??? Yule mtoto alikuwa motoooo chini ya Zahera na sasa amepotezwa mazimaaaa na husikiiii mchambuzi hata mmoja anamtetea wala huoni Wanayanga Wanaanzisha movement yoyote ya BRING BACK BOXER!

Wachambuzi wamejikita kutaka Mafaza akina AJIBU, MORRISON, KICHUYA nk ndio wapewe nafasi??? Unajiuliza hawa wachambuzi wana weledi au Makanjanja?
 
Mkuu! Kichuya tena?

Siwatetei wachambuzi wala waandishi...kwa maana hakuna jinsi wataacha kuongelea wachezaji wa Simba wakaao benchi kwani viwango vyao ni vikubwa mno.

Huyo Ajib kule Yanga alikua mfalme kipindi cha Zahera akapewa mpaka kitambaa na aliku Signatory wa michango inayochangwa kwenye kapu...lakini huku Simba ni wa kawaida tu.

Kahata amekuja Simba akiwa na tuzo ya kiungo bora nchini Kenya lakini Simba hana hakika wa namba. Kuna mengi tutajaza pages tu hapa lakini tuseme tu ukweli pale Yanga kama kuna mchezaji anakaa nje basi ni "Zawadi" ambaye Simba pia hawezi cheza, lakini hao wengine, hakuna mchambuzi au mwandishi ajisumbue kumuulizia kwanini Boxer anakaa nje Apache kuongelea wachezaji wa Maana kina Gadiel Michael, Beno, Kagere au Ndemla kwanini hawachezi.

Wachezaji wa Yanga hawaongelewi sababu quality yao ndogo na wachezaji wa Simba wanaogelewa sababu quality yao ni kubwa sana.
 
Mkuu Kumbuka Boxer huyo huyo unayesema asiongelewe alikuwa ameanza kuitwa hadi timu ya Taifa. Kichuya akiwa Simba alikuwa akiwekwa Benchi utaskia redio zooooote zinalaaaani kuwekwa Benchi, lkn leo yuko Namungo anawekwa Benchi wala huskiiii kidudu mtu yeyote anawashwa.

Salamba vile vileeeee. Ndio najiuliza kwani Macho ya Wachambuzi yanaona Benchi la Simba tu. Mbona hayawaoni akina NINJA, MAKAPU, ALY ALY ambao ni wachezaji wa Kikosi cha kwanza cha Zanzibar Heroz lkn wanasugua benchiii?

Wachambuzi acheni kuwavuruga Wachezaji wa Simba na Uzandiki wenu.
 
Nini tukusaidie??🤔🤔 vipi kodi ya nyumba umelipa mwezi huu??🤔🤔
 
2021-2022 Yanga tutapanda ndege ndugu zangu malalamiko fc watapanda miti tulieni 📌 iwaingie
 
Nendeni mkamfunge kamba ndugu yenu Morrison ashaanza kutukana watu hovyo mitandaoni
 
Mkuu Kumbuka Boxer huyo huyo unayesema asiongelewe alikuwa ameanza kuitwa hadi timu ya Taifa. Kichuya akiwa Simba alikuwa akiwekwa Benchi utaskia redio zooooote zinalaaaani kuwekwa Benchi, lkn leo yuko Namungo anawekwa Benchi wala huskiiii kidudu mtu yeyote anawashwa.

Salamba vile vileeeee. Ndio najiuliza kwani Macho ya Wachambuzi yanaona Benchi la Simba tu. Mbona hayawaoni akina NINJA, MAKAPU, ALY ALY ambao ni wachezaji wa Kikosi cha kwanza cha Zanzibar Heroz lkn wanasugua benchiii?

Wachambuzi acheni kuwavuruga Wachezaji wa Simba na Uzandiki wenu.
Kichuya alienda kuulia soka lake Egypt, Kichuya yule anamfunga "Barthez"goli la kona alikuwa wa moto na hapoi.
 
Wachambuzi wa michezo hapa kwetu ni wachache sna nchi hii wengi ni mareporter na watangazaji htuna watu wanaofanya udadisi uchunguzi na tafiti waje na facts za kuweza kuchambua kwa mapana hoja nyingi za mpira ndio maana unaona wanasubiri kukuza habari na hoja ndogo ndogo kisha wao ndio ziwe maada za vipindi vyao redioni ukisikiliza baadhi ya redio unaweza kuizima hbr ni zile zile mara simba sijui haina kocha mzuri mara kagere hachezi tujikite kwenye hoja za mifumo yetu ya soka tunaweza kuinua vipaji vya vijana wetu
 
Kichuya alienda kuulia soka lake Egypt, Kichuya yule anamfunga "Barthez"goli la kona alikuwa wa moto na hapoi.
Wachezaji wa Kibongo soka la Nje ya Tanzania limewashinda kabisa, akina Samata EPL chali, Kessy Zambia wametoswa, Banda Sauzi hana chake, Singano Mazembe ndio hivyo, Ambokile hata benchi hana namba, Maguli kule Ptatinum ni benchini, Manyika kule Gormahia katoswa yaaani hawa Vijana wetu wakitoka nje ya Mipaka ya Tanzania ni mayaia mayai tu.
Hongera zao Msuva na Himid Mao thats good move, pambaneni.
 
Back
Top Bottom