Wachambuzi kwanini mnataka sana Mohammed Hussein abaki Simba? Meneja wake ndiye atakayemponza kwa uswahili wake

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,512
Naona wanaohangaika sana na hili suala ni baadhi ya wachambuzi na Mzozo. Nadhani kama Simba wanamuhitaji wataongeza wau wangemwongeza.

Sioni issue inakuaje kwa Mohammed Hussein aonekane bila yeye Simba haiwezi kwenda mbele? Nadhani wamwache tu aamue anachotaka, ana haki ya kwenda popote anapotaka.

Mohammed Hussein anaweza achwa tu Simba na wala si nguzo kubwa ya kiasi hicho. Simba ya sasa inaweza acha mchezaji yoyote hasa kwa nafasi ya Mohamed Hussein.

Kitakachomponza Mohammed Hussein ni Meneja wake. Nami nadhani kwa hili Simba wamwache Mo Hussein ili Meneja wake amuuze anapoona panafaa.

Sioni shida ipo wapi. Simba ina haki ya kumwacha na Mohammed Hussein ana haki ya kutafuta sehemu ambayo itamlipa zaidi.

Meneja anaonekana kutokuwa na mstaarabu kutokana na maneno anayoongea. Nadhani Simba wamwachie Meneja ampeleke Mo Hussein popote anapoona panafaa. Simba ni kubwa sana kuliko mchezaji yeyote.
 
Upo sahihi, japo nakubali kwamba MH. ni moja ya wachezaji muhimu simba lakini maneno ya meneja wake ni ya hovyo sana. Nashangaa kwa nini wachambuzi wengi hawalioni ilo wao wanatoa lawama kwa simba tu. Jamaa yupo very unprofessional.
 
Upo sahihi, japo nakubali kwamba MH. ni moja ya wachezaji muhimu simba lakini maneno ya meneja wake ni ya hovyo sana. Nashangaa kwa nini wachambuzi wengi hawalioni ilo wao wanatoa lawama kwa simba tu. Jamaa yupo very unprofessional

Sidhani kama ni maneno ya hovyo bali nadhani anatema nyongo. Honestly wachezaji wazawa hatuwapi thamani wanayostahili
 
Ni kweli mkuu nakubaliana na ww kwa 100% kuhusu kutowapa thamani yao wachezaji wa ndani, lakini meneja ilitakiwa awe na namna fulani ya kuelezea hii ishu kiweredi. Jamaa anabwabwaja sana unless kama ana uhakika mteja wake hatocheza tena simba. Inawezekana kabisa simba hawakupeleka ofa nzuri, lakini bado the way jamaa anavoelezea kwenye interview zake tofauti unaona kabisa ana uhaba wa ueredi. Kwa mfano nimemsikia kwenye clip moja anatamba amepokea simu ya simba lakini hataenda kuwasikiliza kwa muda wake akipenda yeye, sioni kama kulikuwa kuna haja ya kusema hivyo. Mambo ya kimkataba ni mahusiano kama yalivyo mahusiano mengine yeyote hivyo si kila kitu kinatakiwa kuwa hadharani
 
Thamani ya mtu si inaonekana? Kwani ni ya kulazimisha? Kama Simba wanaona hana thamani si anabeba vyake anaondoka... Kwa nini mnataka kulazimisha THAMANI? Akiona kuna sehemu atapata thamani zaidi aende.
 
Aende anapotaka ambapo ataona kuna hela nyingi hatutaki makelele kila siku zimbwe zimbwe wakati Simba ni kubwa sana kuliko mchezaji yoyote
 
Ni kweli mkuu nakubaliana na ww kwa 100% kuhusu kutowapa thamani yao wachezaji wa ndani, lakini meneja ilitakiwa awe na namna fulani ya kuelezea hii ishu kiweredi. Jamaa anabwabwaja sana unless kama ana uhakika mteja wake hatocheza tena simba. Inawezekana kabisa simba hawakupeleka ofa nzuri, lakini bado the way jamaa anavoelezea kwenye interview zake tofauti unaona kabisa ana uhaba wa ueredi. Kwa mfano nimemsikia kwenye clip moja anatamba amepokea simu ya simba lakini hataenda kuwasikiliza kwa muda wake akipenda yeye, sioni kama kulikuwa kuna haja ya kusema hivyo. Mambo ya kimkataba ni mahusiano kama yalivyo mahusiano mengine yeyote hivyo si kila kitu kinatakiwa kuwa hadharani
Nimemsikiliza yule meneja.
Nimegundua hana uweledi kabisa.
 
Kuna mda utamsikia thaman ya mchezaji ni 100 mill
Alafu inashuka hadi 75 mill.
Sasa mbona anajishusha mwwnyewe?

Ilitakiwa atengeneze mazingira timu yoyote iende mezani
 
Wasichojua ni kwamba thamani ya mchazaji inaongezeka kulingana na timu aliyoko. Kazi wanayofanya makocha sijui kwa nn wachambuzi hawataki kuiona. Kwa maana nyingine thamani ya MH inaongezwa pia na mafunzo anayoyapata simba. Akiwa na akili atakataa porojo za wakala njaa. Exposure anayopata simba hawezi ipata timu yoyote. Hii nayo ni incentive pia.
Kwan Ramadhani Singano Messi yupo wapi kwa sasa? Haya mambo ya mameneja. Hawa hawana uchungu kama mnavyodhani.
 
Wasichojua ni kwamba thamani ya mchazaji inaongezeka kulingana na timu aliyoko. Kazi wanayofanya makocha sijui kwa nn wachambuzi hawataki kuiona. Kwa maana nyingine thamani ya MH inaongezwa pia na mafunzo anayoyapata simba. Akiwa na akili atakataa porojo za wakala njaa. Exposure anayopata simba hawezi ipata timu yoyote. Hii nayo ni incentive pia.
Hana akili. Anadanganyw ana media kuwa yeye ni mchezaji mkali sana. Nashauri Simba wamwache
 
hii ishu inakera sana simba ikimpigia magoti huyo meneja muhuni wajue kwamba itakuw a ni style mpya ya wachezaji kwenda kuokota wahuni kitaa kuropoka maredioni na kutishana ,aende tu tunamshukuru kwa kuisaidia team kila la kehri
 
Sidhani kama ni maneno ya hovyo bali nadhani anatema nyongo. Honestly wachezaji wazawa hatuwapi thamani wanayostahili
Hiyo nyongo alitakiwa aiteme wakati wa kukubaliana kwenye mkataba either wa sasa au kabla huu haujaisha. anacho fanya sasa ni kupiga kelele tu
 
Naona wanaohangaika sana na hili suala ni baadhi ya wachambuzi na Mzozo. Nadhani kama Simba wanamuhitaji wataongeza wau wangemwongeza.

Sioni issue inakuaje kwa Mohammed Hussein aonekane bila yeye Simba haiwezi kwenda mbele? Nadhani wamwache tu aamue anachotaka, ana haki ya kwenda popote anapotaka.

Mohammed Hussein anaweza achwa tu Simba na wala si nguzo kubwa ya kiasi hicho. Simba ya sasa inaweza acha mchezaji yoyote hasa kwa nafasi ya Mohamed Hussein.

Kitakachomponza Mohammed Hussein ni Meneja wake. Nami nadhani kwa hili Simba wamwache Mo Hussein ili Meneja wake amuuze anapoona panafaa.

Sioni shida ipo wapi. Simba ina haki ya kumwacha na Mohammed Hussein ana haki ya kutafuta sehemu ambayo itamlipa zaidi.

Meneja anaonekana kutokuwa na mstaarabu kutokana na maneno anayoongea. Nadhani Simba wamwachie Meneja ampeleke Mo Hussein popote anapoona panafaa. Simba ni kubwa sana kuliko mchezaji yeyote.
Ila kumbuka Siba kafungiwa kusajili kwa mwaka mzima
 
Back
Top Bottom