Wachakachuaji mafuta sasa ‘cha moto’ Januari........................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wachakachuaji mafuta sasa ‘cha moto’ Januari........................

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280

  Wachakachuaji mafuta sasa ‘cha moto’ Januari

  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd December 2010 @ 23:55

  WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kuanzia Januari mosi mwakani, kuanza kuhakiki vinasaba vilivyowekwa kwenye mafuta ya petroli ili kubaini wachakachuaji wa nishati hiyo.

  Aidha, ameagiza watakaobainika kuchakachua mafuta wachukuliwe hatua za kisheria haraka. Akizungumza na watendaji wa mamlaka hiyo jana wakati alipofanya ziara kwenye Makao Makuu ya Ewura, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa katika nafasi ya uwaziri, Ngeleja aliitaka pia mamlaka hiyo kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu kupungua kwa tatizo la uchakachuaji.

  Hatua hiyo ya Ngeleja imekuja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Haruna Masebu kuelezea mpango wao wa kuanza kuhakiki vinasaba mwakani. Septemba mosi mwaka huu, Ewura ilianza kuweka vinasaba kwenye mafuta yote yanayoingia kwa matumizi ya nchini na kutoa miezi mitatu kabla ya kuanza uhakiki ili kutoa nafasi kwa mafuta ya zamani yamalizwe.

  Kwa mujibu wa Masebu, wakati wa uhakiki watapima kiwango cha vinasaba walivyoweka na kama itabainika kupungua, maana yake mafuta hayo yatakuwa yamechakachuliwa na iwapo
  hayataonekana kuwa na vinasaba, yatakuwa yalipangwa kusafirishwa nje ya nchi na si kwa matumizi ya nchini.

  Kiwango cha uchakachuaji mafuta kimepungua kutoka asilimia 78 mwaka 2007 hadi asilimia 40 ya mafuta yote Juni mwaka huu.

  Kumekuwapo na malalamiko makubwa juu ya mwenendo huo wa baadhi ya wafanyabiashara kuchanganya mafuta ya taa na petroli na dizeli, kwa nia ya kupata faida kubwa.

  Akizungumzia uagizwaji wa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa nchini kwa pamoja, Masebu alisema “kanuni ndogo na taratibu za uendeshaji wa mfumo mpya wa kuagiza mafuta kwa pamoja, zimekamilika na itahitajika miezi minne kuunda Bodi ya Uratibu na kuajiri watendaji.

  Alisema mwezi mmoja mwingine utahitajika kutangaza zabuni na mwezi mmoja wa kuwasilisha shehena ya kwanza ambapo baada ya miezi sita mfumo huo utaanza kuonesha matunda. Hata hivyo, Waziri Ngeleja alitaka kazi hiyo kukamilika ndani ya miezi minne ambapo Mei mosi, mfumo huo uwe umeshaanza.

  Akifafanua juu ya mfumo huo, Masebu alisema uagizaji huo wa mafuta kwa pamoja hautafanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pekee, bali itashirikiana na kampuni binafsi za wafanyabiashara wa mafuta ambapo kila mwezi kutatangazwa zabuni na kampuni moja itaagiza mafuta na kampuni hizo zitashindana kila mwezi.

  Kwa sasa kuna kampuni 57 za mafuta zinazoingiza mafuta bila kushirikiana. Masebu alisema Ewura imedhibiti upandaji holela wa bei ya mafuta ambapo sasa ni pungufu ya asilimia 30.

  Tangu kuanzishwa kwake miaka minne iliyopita, imeshatoa leseni 835 za sekta ya mafuta.

  Akizungumzia kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 18.5 kuanzia Januari mwakani, Ngeleja aliitetea Tanesco kuwa na haki ya kupandisha bei kwa madai kwa muda mrefu bei zake zimekuwa hazimudu gharama za uendeshaji.

  “Tanesco haipati ruzuku ya serikali na lazima ipandishe bei ili ijiendeshe na imekuwa ikifanya vizuri kila mwaka, mfano miaka minne iliyopita wakati wa Net Group Solution ilikuwa ikipata hasara ya Sh bilioni 168, lakini mwaka jana hasara ni Sh bilioni tano na mwakani hakutakuwa na hasara,” alisema Ngeleja.

  Alisema kila mwaka Tanesco imekuwa ikiongeza makusanyo kwa asilimia 10 kutoka Sh bilioni 19 miaka minne

  iliyopita hadi Sh bilioni 40 mwaka huu. Akijibu madai kuwa Tanesco imepandisha bei ya umeme wake ili kupata fedha za kuilipa Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, Waziri huyo alisema “hukumu ilitolewa Novemba mwaka huu, wakati mchakato wa kupandisha umeme
  ulianza mwaka 2007 wakati ambao hata Dowans haikuwepo.”

  Masebu alisema ili kufikia lengo la asilimia 30 ya Watanzania kuwa na umeme, Tanesco inahitaji kuunganisha wastani wa kaya 230,000 kila mwaka. Kwa sasa ni asilimia 14 wanapata huduma ya umeme.
   
 2. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Hivi, serikali na viongozi wa ccm wanaendesha nchi kwa vitisho? Kutekeleza hawatekelezi.
  Kila mtu akija.. oh kuanzia kesho bla bla bla; mwengine akaja na ya kuwa anawaachia wezi wale krismasi kwanza ...... hadi leo wanakula krismasi.

  ghasia tupu!!
   
 3. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  The same old stories!

  EWURA haya maneno wameyasema miaka mitatu iliyopita lakini hamna lolote mpaka leo!

  Magari ya msafara wa JK mwenyewe yalichakachuliwa!
   
Loading...