Wachaga wajanja

prezdesho

Senior Member
Dec 30, 2015
150
78
Fwd:
UTANI WA WACHAGGA.!!

Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio wote wajanja. Kuna:-

1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana na wanawake wa Marangu na wanawaita "vishohia". Wanawake wa Rombo ni mama Huruma, wanaachia tu.. Ukioa Mrombo ujue umeolea kijiji.

2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake. Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si jambo la ajabu.

3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa wanayofanya ni ya kuchinja... wengi wanamiliki mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili.. Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai kisu chake.

4. WAMACHAME; hawa ni wezi sana, ukifanya nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako makini mno hasa kwenye pesa. Wakiwa na hasira hawaoneshi waziwazi, so Mmachame anaweza kukuua huku akitabasamu. Sio waaminifu sana lakini wanaenda kanisani mara nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake wa machame wanaitwa 'Wapalestina'.. Mume ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.

5. WAURU; hawa hupenda kusoma sana lakini hawapendi maendeleo kabisa. Hadi leo eneo lao la Kishumundu linatumika ku-identify wachagga washamba. Wanawake wakifikisha umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu, lakini wanawake ni wachapakazi hodari. Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.

6. WASIHA; Kwanza hawapendi kuitwa Wachagga. Wanajiita watu wa West-Kilimanjaro. Ni mchanganyiko wa Wachagga na WaMeru. Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za ufundi na kilimo. Viazi vingi vya Chips Arusha na Moshi vinatoka kwao. Wanawake zao wana "vigimbi" mguuni sababu ya kulima mno.!

7. WAKIRUA; wanapenda sifa kama Wahaya. Wanawake wa Kirua ni wachawi kupindukia.. Wanaloga hata jiwe ili tu alikomoe.. Wanaume wa Kirua hawapendi kuoa kwao.. Hawapendi kuishi mjini maana wanaogopa gharama.. lakini siku wakija mjini wawili tu utadhani wako mia.

8. WA OLD-MOSHI; Hawa ni mafundi stadi wa ujenzi wa nyumba, japo hawajengi kwao. Mpaka leo hamna daladala ya kwenda Old-Moshi inayoanzia Moshi mjini, maana ni wabishi kulipa nauli na pesa inaishia kwenye mbege njiani. Wanaume wamezoea kutoka nyumbani saa kumi na moja alfajiri na kurudi saa sita ya usiku kwa miguu.!


✋✋
 
Namba nane nakubaliana na wewe kitu kimoja KWAMBA NI MAFUNDI WAZURI SANA ( MASONRY NA CARPENTRY) lakini kwamba hawajengi kwao sii kweli. eti hamna daladala sii kweli. daladal zipo kibao na kule nyumba za mbavu za mbwa ni chache sana. TENA UKOME KUANDIKA VITU AMBAVYO HUNA UHAKIKA NAVYO.

Old Moshi ya kwetu haina Daladala mkuu na sikujua ni kwanini.

Hapo kwamba hatujengi kwetu kazingua kweli. Tuna mijengo balaa.
 
Wamachame ni hodari sana kuamua kukatisha maisha yao kwa kunywa sumu ya Thiodan itumikayo kama kiatilifu pale mambo yanapowawendea kombo.Kwa ujumla wanauchukia sana umasikini kiasi cha kutokuona faida ya kuendelea kuishi katika hali duni.Either waibe au wajiue.
 
Old Moshi ya kwetu haina Daladala mkuu na sikujua ni kwanini.

Hapo kwamba hatujengi kwetu kazingua kweli. Tuna mijengo balaa.
Old Moshi ni town so unaweza tembea tuu haina haja ya daladala
 
Kikarara ila sifiki Kolila naingia boda la kupandisha lile kanisa la kule juu Mahoma.

Mara nyingi watu huwa wanapiga mdogo mdogo labda itokee lifti.

Duh! Basi huko kwenu mko nyuma. kwetu ziko za kumwaga.
 
Old Moshi ni town na taa za mjini zilikuwa zinatuangazia usiku kabla ya kuletewa Umeme. Sasa hivi Umeme tunao na daladala zipo na zikifika mjohoroni akishashusha abiria unaweza kumkodi kuelekea Mlimani wakati akisubiria foleni ya kurudi town . Kuhusu ufundi ni kweli na mbona sote tumejenga ?
 
Jamaa ve ni mburasi tena ni kshohoia kya varim na wesukwa na tena veningete varombo ulwajua wapi ww?
 
Na lingine wanaume wa kimarangu c waoga kama unavyo sema ww mnunua kabilla jaribu kuchezea mwanaume wa kimarangu uone ni waoga au laa!!!
 
watu wa rombo sijui vip, wanapiga dili za wizi sana au za misukule kweli au inakuaje? mtu amemaliza la saba anakuja dar, ndani y a miaka 5 amejenga jumba kali pamoja na magari ya bei mbaya, ukiona karudi kijijini, utafikiri maisha ya dar marahisi kweli, nenda ukajaribu uone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom