X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Wabunge Zanzibar watetea Muungano; Wamzodoa Lissu
Wabunge wawakilishi toka Zanzibar jana walisahau tofauti zao za kiitikadi na kumcharukia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu kutokana na kile walichodai ni ya kifedhuli na inachochea kuvunja Muungano, suala ambalo Wazanzibari hawa kubaliani nalo.
Katika hotuba yake baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2011/2012, Lissu aliligusia suala la Zanzibar kuhusishwa katika mchakato wa maoni ya uundwaji wa Katiba mpya ya Muungano, jambo analolipinga Lissu akitaka wahusike katika mambo yanayohusu Muungano pekee.
Mbunge wa Magomeni (CCM), Muhammad Amour Chomboh, alisema Zanzibar si koloni la Tanganyika, Napenda kumfahamisha yeye (Lissu) pamoja na wengi walio humu ndani wenye mawazo mgando kama yeye na waliokuwapo nje ya jumba hili, Zanzibar sio koloni la Tanganyika na halitakuwa hata siku moja koloni la Tanganyika. Kauli na hotuba ya Tundu Lissu imejaa ufedhuli na dharau kwa wananchi wa Zanzibar, mtu mwenye mawazo mgando kama haya hapaswi kuungwa mkono, Wazanzibari tuna historia ya vyama vingi tangu mapinduzi mwaka 1964 hivyo mtu ye yote hawezi kutubabaisha. Na mheshimiwa Lissu Agosti 8 mwaka huu, alizungumza huyu kuhusiana na mambo ya Muungano kuchangia katika hotuba ya Muungano akajaribu kuwataja viongozi, ambao ni victim (waathirika) wa Muungano, ambao ni muongo na mnafiki, alisema na kuongeza, Nataka kumwambia kuwa Wanzanzibari hawatakubaliana na mpuuzi yoyote na uozo wowote, ambao umezungumzwa hapa kwa minajili ya kutaka kutugombanisha, alisema. Alipotaka kuendelea, alikatizwa na Lissu aliyekuwa akiomba muongozo.
Kwa mara nyingine, Lissu alisimama akitaka kutoa taarifa lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliingilia kati na kuwataka wabunge wote kuwa wavumilivu na kisha kumruhusu Chomboh kuendelea kuchangia.
Chomboh alisema kauli ya Lissu kwamba mambo ya Muungano pekee ndiyo yajadiliwe na Wazanzibari huku akieleza kuwa nchi inaendekeza utawala wa kifalme, ni sawa na kusema hata wao wabunge wa Zanzibar wasihusike katika kutoa maoni wala elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Alimalizia kwa kusema, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere pamoja na Karume wametutoa mbali na kutufikisha hapa, tumevumilia Wazanzibair tumeona sasa basi, Zanzibar ilikuwa Taifa na ilitambulika Kimataifa hivyo, baada ya kuungana hilo halipo, huyu ni nani anataka kuturudisha humo (makofi), hili hatukubali hata kidogo, tunaupenda Muungano.
Mbunge wa Tumbe (CUF), Rashid Ali Abdallah, alisema kauli aliyoitoa Lissu wakati akisoma hotuba hiyo, inaonyesha kuwa haelewi maana ya taifa.
Haelewi historia ya Zanzibar. Na kwa maana hiyo, mwelekeo wa Kambi ya Upinzani umepotea njia. Nadhani haya ni maoni yake. Unaposema Rais wa Zanzibar atolewe katika mambo yanayohusiana na Muungano una maana gani? Ipo serikali ya Tanganyika kujadili mambo ya Tanganyika hapa? alihoji na kuongeza, Nazungumza hili kwa uchungu kabisa. Huyu ni msomi, lakini sijui amehitimu vipi usomi wake jambo la msingi ni kuimarisha taifa letu liwe na nguvu lenye utawala bora na misingi ya uwajibikaji. Mawazo haya ya mheshimiwa waziri kivuli wa katiba na sheria ni mawazo funyu, yamepitwa na wakati na hayatapewa nafasi.
Naye Mbunge wa Donge (CCM), Sadifa Juma Khamis, alisema mazungumzo yaliyotolewa na Lissu juzi yamevunja hata Katiba iliyopo hivi sasa. Aliwataka kuangalia kifungu namba nane na namba tisa vya Katiba, vinavyomtaka mwananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yanayohusu nchi yake ya Tanzania. Alisema kungekuwa na Serikali ya Tanganyika wasingeingilia mambo yanayohusu serikali hiyo.
IPP Media