Wabunge Zanzibar watetea Muungano; Wamzodoa Lissu

X-PASTER

Moderator
Joined
Feb 12, 2007
Messages
11,649
Points
1,250

X-PASTER

Moderator
Joined Feb 12, 2007
11,649 1,250
Wabunge Zanzibar watetea Muungano; Wamzodoa Lissu

Wabunge wawakilishi toka Zanzibar jana walisahau tofauti zao za kiitikadi na kumcharukia Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu kutokana na kile walichodai ni ya kifedhuli na inachochea kuvunja Muungano, suala ambalo Wazanzibari hawa kubaliani nalo.

Katika hotuba yake baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2011/2012, Lissu aliligusia suala la Zanzibar kuhusishwa katika mchakato wa maoni ya uundwaji wa Katiba mpya ya Muungano, jambo analolipinga Lissu akitaka wahusike katika mambo yanayohusu Muungano pekee.

Mbunge wa Magomeni (CCM), Muhammad Amour Chomboh, alisema Zanzibar si koloni la Tanganyika, “Napenda kumfahamisha yeye (Lissu) pamoja na wengi walio humu ndani wenye mawazo mgando kama yeye na waliokuwapo nje ya jumba hili, Zanzibar sio koloni la Tanganyika na halitakuwa hata siku moja koloni la Tanganyika. Kauli na hotuba ya Tundu Lissu imejaa ufedhuli na dharau kwa wananchi wa Zanzibar, mtu mwenye mawazo mgando kama haya hapaswi kuungwa mkono, Wazanzibari tuna historia ya vyama vingi tangu mapinduzi mwaka 1964 hivyo mtu ye yote hawezi kutubabaisha. Na mheshimiwa Lissu Agosti 8 mwaka huu, alizungumza huyu kuhusiana na mambo ya Muungano kuchangia katika hotuba ya Muungano akajaribu kuwataja viongozi, ambao ni victim (waathirika) wa Muungano, ambao ni muongo na mnafiki,” alisema na kuongeza, “Nataka kumwambia kuwa Wanzanzibari hawatakubaliana na mpuuzi yoyote na uozo wowote, ambao umezungumzwa hapa kwa minajili ya kutaka kutugombanisha,” alisema. Alipotaka kuendelea, alikatizwa na Lissu aliyekuwa akiomba muongozo.

Kwa mara nyingine, Lissu alisimama akitaka kutoa taarifa lakini Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliingilia kati na kuwataka wabunge wote kuwa wavumilivu na kisha kumruhusu Chomboh kuendelea kuchangia.

Chomboh alisema kauli ya Lissu kwamba mambo ya Muungano pekee ndiyo yajadiliwe na Wazanzibari huku akieleza kuwa nchi inaendekeza utawala wa kifalme, ni sawa na kusema hata wao wabunge wa Zanzibar wasihusike katika kutoa maoni wala elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Alimalizia kwa kusema, “Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere pamoja na Karume wametutoa mbali na kutufikisha hapa, tumevumilia Wazanzibair tumeona sasa basi, Zanzibar ilikuwa Taifa na ilitambulika Kimataifa hivyo, baada ya kuungana hilo halipo, huyu ni nani anataka kuturudisha humo (makofi), hili hatukubali hata kidogo, tunaupenda Muungano

Mbunge wa Tumbe (CUF), Rashid Ali Abdallah, alisema kauli aliyoitoa Lissu wakati akisoma hotuba hiyo, inaonyesha kuwa haelewi maana ya taifa.

“Haelewi historia ya Zanzibar. Na kwa maana hiyo, mwelekeo wa Kambi ya Upinzani umepotea njia. Nadhani haya ni maoni yake. Unaposema Rais wa Zanzibar atolewe katika mambo yanayohusiana na Muungano una maana gani? Ipo serikali ya Tanganyika kujadili mambo ya Tanganyika hapa?” alihoji na kuongeza, “…Nazungumza hili kwa uchungu kabisa. Huyu ni msomi, lakini sijui amehitimu vipi usomi wake…jambo la msingi ni kuimarisha taifa letu liwe na nguvu lenye utawala bora na misingi ya uwajibikaji. Mawazo haya ya mheshimiwa waziri kivuli wa katiba na sheria ni mawazo funyu, yamepitwa na wakati na hayatapewa nafasi

Naye Mbunge wa Donge (CCM), Sadifa Juma Khamis, alisema mazungumzo yaliyotolewa na Lissu juzi yamevunja hata Katiba iliyopo hivi sasa. Aliwataka kuangalia kifungu namba nane na namba tisa vya Katiba, vinavyomtaka mwananchi kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yanayohusu nchi yake ya Tanzania. Alisema kungekuwa na Serikali ya Tanganyika wasingeingilia mambo yanayohusu serikali hiyo.

IPP Media
 
Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
5,029
Points
1,500

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
5,029 1,500

Nadhani kuna watu humu JF watawashambulia sana hawa wabunge. Kuna watu hawataki kabisa kusikia Muungano, lakini baadhi ya wabunge wanaona kuwa unafaa. Na wanajua wazi kuwa Zanzibar ni nchi katika jamhuri, na wanajua wazi kabisa kuwa Tanganyika si nchi katika jamhuri.

Lakini naona pia LIssu ana pointi, inakuwaje watu kutoka Zanznibar wajadili katiba inayohusu mambo ya watu wa bara. mbona wa bara hawajadili yanayowahusu watu wa Zanzibar? Itakuwa ni busara kama watu wa zanzibar watashirikishwa kwenye mambo ya katiba yanayohusu muungano, ni vem,a ukiwekwa utaratibu huo.
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
9,743
Points
0

Bajabiri

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
9,743 0
Wabunge wa zanzibar wanautetea,wawakilishi wanaukandia,,,,,,sijui nani mkweli,hawa wabunge wanaskia raha kuja dodoma,,,,wawakilish hawajui raha za bara,,,,,,wabunge wakiukataa watapata wapi posho NONO????MASHAMBA YA BURE,NYUMBA ZA BEI CHEE,kuna wabunge weeeeng wa visiwan wamenunua nyumba za shirika la bima maeneo ya area C na D huko DODOMA
 
Rich Dad

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Messages
737
Points
0

Rich Dad

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2010
737 0
Mkuu hapo umesema jambo ambalo ni kweli tupu, hawa wabunge wanaijadili hii hoja kibinafsi zaidi! Wanaangalia nini wao binafsi watapata au watakosa kama wataungana na TUNDU LISSU katika recommendations zake.
Mimi binafsi nimewahi kuzungumza na wazee wa kizanzibar wakati fulani nilipokuwa zanzibar, hawataki kabisa kusikia kitu inaitwa Muungano. Na sababu kubwa wanayoitoa ni kwamba MUUNGANO umekaa kiujanjaujanja, huku ukiwafaidisha zaidi watu wa Tanzania Bara.
Wabunge wa zanzibar wanautetea,wawakilishi wanaukandia,,,,,,sijui nani mkweli,hawa wabunge wanaskia raha kuja dodoma,,,,wawakilish hawajui raha za bara,,,,,,wabunge wakiukataa watapata wapi posho NONO????MASHAMBA YA BURE,NYUMBA ZA BEI CHEE,kuna wabunge weeeeng wa visiwan wamenunua nyumba za shirika la bima maeneo ya area C na D huko DODOMA
<br />
<br />
 
Userne

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2011
Messages
892
Points
0

Userne

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2011
892 0
si wabunge tu wanaotetea muungano huu wa kisanii, bali wazenj wote wanaofaidika na muungano huu wa kipwagu, wakiwemo wastaafu, madiwani, wafanyi biashara, wajumbe wa nyumba10 Toka Jamuhuri ya Zenj! hadi wanaongea kwa jeuri kama nchi hii ya Tanganyika wamerithishwa na baba zao. Kama ni kweli wanapenda Muungano, basi iwepo serkali MOJA YA MUUNGANO AU MUUNGANO UFE.
 
Nyangomboli

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
3,054
Points
2,000

Nyangomboli

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2010
3,054 2,000
Tundu yupo na mawazo mazuri. Nawaza kama yeye. Hata hivyo viongozi na watz wengi hawajagundua kama wazenj4 wanatudharau sana na kuvfanya majuha. Inakuwaje wao warekebishe katiba na sisi bara tusishiriki ila the oposite wanataka washiriki? Haiingii akilini kumuona mtu akitamka kuwa zanzibar si koloni la tanganyika ni nchi huru halafu mv huyohuyo anataka kushiriki mambo muhimu ya nchi nyingine tena kwa kujiona ana haki sawa huku keshaonyesha kujitenga either kwa kujua ama kutokujua. Ni dharau kubwa sana na mimi pendekezo ni moja tu. Nchi hii iwe moja au zanzibar ijitegemee kivyake. . Hujui thamani ya kitu ulichonacho ila tu ukikipoteza.
 
Kilasara

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2008
Messages
578
Points
0

Kilasara

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2008
578 0
Wabunge watokao Zanzibar wanatetea Muungano, licha ya Wajumbe wa Baraza la Zanzibar la Wawakilishi kupinga Muungano. Ni Baraza la Wawakilishi lililopitisha Azimio la kutoa Mafuta katika Orodha ya Mambo ya Muungano na ni baadhi ya WaZenj wanaowaunga mkono walichana hadharani Muswada uliohusu Katiba Mpya ya Tanzania.

Mimi kama MwanaCDM, ninayeamini ktk mfumo wa Demokrasia ya dhati, nakubaliana na Tundu Lissu, mia kwa mia, kwamba Katiba Mpya tunayotaka kuandika ni lazima ichambue ushiriki wa Zanzibar katika Muungano. Hatuwezi kuendelea kuwa na mfumo unaojaribu kufanya Zanzibar iwe sawa na Tanganyika kama CCM inavyojaribu kufanya sasa. Sasa hivi Zanzibar yenye population isiyozidi milioni 1.5 inawakilishwa sawa na Tanzania Bara yenye population ya milioni 42 katika vyombo na vikao vya CCM na Serikali yake.!!!!!. Na Wazanzibari wanalalamika eti wanabaguliwa! Kwa mtindo wa sasa "The tail is wagging the Dog; rather than the Dog wagging the Tail"!!!!!.

Kama Wazanzibari wakiridhika kwamba ni muhimu kuwa na nchi kubwa ili tupige hatua za haraka na uhakika kimaendeleo, tuunde Serikali moja, badala ya serikali mbili. Ili kuwaridhisha Wazanzibari, tunaweza kufanya Zanzibar iwe ni mikoa miwili, yaani Unguja iwe mkoa mmoja, na Pemba iwe mkoa mwingine. Ikumbukwe kwamba jumla ya wakazi wa hivi visiwa viwili haiwezi kuwa sawa na jumla ya watu wa mkoa mmoja wa Bara.
 
Edward Teller

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
3,821
Points
1,225

Edward Teller

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
3,821 1,225
wananchi wengi pamoja na wabunge wao hawaoni umuhimu wa muungano-hata leo hii wewe nikikuuuliza faida gani umepata juu ya muungano-simply hakuna,tundu lissu alizungumza vyema sana,cha ajabu wabunge wa zanzibar hawaeleweki,mara wasema kama zanzibar ni mzigo ni bora tanganyika iuache huo mzigo na maneno mengi ya kukashifu wanayatoa,mimi ninavyooana hawa viongozi ni waoga wa kuchukua maamuzi magumu,maana wanaogopa wao kuwa wa kwanza kuvunja muungano-ila naamini siku ya huu muungano uchwara kufa itafika tu
'to hell with zanzibar'
 
Mwathirika

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
207
Points
195

Mwathirika

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
207 195
Ndiyo maana ya mjadala. Mjadala unaongeza fikra, Icome again, THINK BIG!!
Hakuna mwakilishi, sijui mbunge au chombo chochote kivukacho maji yale ya bahari kisishangae huu muungano, sasa inapofika kujadili ukweli wa muungano hawa jamaa wanajifanya wamesahau waliyokizungumzia awali! Kwa kifupi hii ni tabia ya kinafiki. Hawa hawa ndo wanashauri kuwapo kwa serikali tatu, sasa itakapofika hapo wataweza kujadili mambo yanayohusu Bara? Tatizo linalowasibu wabunge wengi ni kujua kama wanaangaliwa katika luninga mpaka inafikia mbunge anataka kupinga hoja anaishia kuiunga mkono kwa sababu ya kutokujiandaa au kutojua ninin hasa anataka kuongea. Sidhani katika mawazo yake Tundu alitaka kusema Muungano usiwepo na kwamba haupendi Muungano!! Alisema hawa jamaa zetu wajadili mambo yanayohusu Muungano, na katika kujadili mambo ya Muungano watakuwa na fursa pana ya kujadili huo Muungano wanaoupenda! Mambo ya Geita, Tarime na Katavi yanawahusu nini?
 
Forum statistics

Threads 1,353,420
Members 518,338
Posts 33,076,905
Top