Wabunge wote fanyeni hivi.....!!!

J.K.Rayhope

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
316
31
WanaJF,inaeleweka wazi kwamba Mbunge,ni mwakilishi wa wananchi au kwa tafsiri ya kawaida sana ni sauti ya jimbo lake.Pia ameajiriwa na wananchi wake kwa kura alizopata.Tusiwahukumu kwa huu muda mfupi,ila wayape vipaumbele mambo yafuatayo:
1.Elimu-Leo elimu ni biashara,shule hazina madawati,ubora wa elimu,majengo,vyoo,n.k. Mbunge uwe mkali,weka hata malengo ya hata dawati 5 kwa mwezi......Utapendwa Utakumbukwa
2.AFYA-Afya nayo imekuwa biashara kuu,huna hela unakufa.Hamasisha na shirikiana na wananchi wako,jengeni zahanati yenu,hata mama akijikata wakati anapika awe na sehemu ya kwenda fasta.........Utapendwa utakumbukwa.
3.MAJI-Maji nayo yamekuwa dili,weka malengo walau kisima kimoja kwa mwaka jimboni mwako.Wapo wananchi wasiojua maji safi au yale salama yakoje.Angalia sana hili.
4.MAWASILIANO-Uwe na mawasiliano na wananchi wako,wapo wengine hujiona wao ni "the best than ever before" hashirikiani na watu.KISA!MIMI NI MBUNGE.Ebo!Kwamba ww ni special sana eti?Umetengenezwa kwa bati sasa?.....Tengeneza barabara hata za vumbi,akipita mpiga kura wako aseme "yes!hii ndio kura yangu".Rejesha taarifa kwao,umefanya nini,(sio udanganye)lini,wapi,nini......Utapendwa,Utakumbukwa.
Yapo mengi ambayo yanafaa kuwakumbusha,Naomba kuwasilisha hoja.
 
Wewe ni ************ na cdm wako wooooteeeeeee

duh! I believe today that you can take an African out of the bush, but never take bush out of Africa. Jamaa katoa point nzito tena creative without mentioning political party, af we unacritisize duh!
 
Back
Top Bottom