Wabunge wetu, tusaidieni utaratibu mpya wa Mfuko wa bima ya afya NHIF

ivi kwanza makato yataendana na idadi ya wategemezi katika mfuko au ndo ile % general kwa wote?

Mku ni general % kwa wote ilimradi tu una ngazi fulani ya mshahara. Mfano kama kwa mshahara wako natakiwa kulipa 250,000 itakatwa hiyo hiyo whether uko mwenyewe au mko sita.
 
Wameweka Masharti Mapya Ya Hovyo Sana.1.Wategemezi Wengine Wamewatoa.Wamebakisha Wazazi Au Wakwe,nafasi Zipo Sita,fikiria Unawazai Wote 2,unawakwe Wote 2,wewe Na Mkeo Mpo 2,halafu Unawatoto 3. Maana Yake Watoto Hawana Nafasi Hapo.2.Ikitokea Huna Mke,wazazi Wala Mtoto,ila Unakaka,shangazi Aliyekusomesha Hawamtaki Umjaze Kwenye Bima Hvy Nafasi Zote 5 Zinapotea Bure Na Gharama Unazochangia Hazipungui.3.Mtoto Wako Akifikisha Miaka 18 Wanamtoa Kwenye Bima Ilihali Umri Huo Yupo Kidato Cha Nne Hajaanza Kujitegemea Hvy Utakuwa Unagharamia Matibabu Yake Na Bima Wanakata Kwa Kiwango Kilekile Cha Mwanzo Hakipungui. JAPO WENGI MMEKAA KIMYA KWA SABABU MLIOWAINGIZA KWENYE BIMA HAWATAONDOLEWA SASA SUBIRINI SK APOTEZE KITAMBULISHO CHAKE CHA BIMA NDO UTAJUA NINACHOKIZUNGUMZA HAPA JAPO UNAKIONA HAKIFAI. WABUNGE WOTE Mtusaidie, RAIS JAKAYA KIKWETE HAPA UNAHUSIKA KUTOA NENO LAKO UTUSAIDIE TUNANYONYWA HAPA.
 
Kila Utakaesoma Hapa Naomba Umtumie Meseji Mbunge Wako Ukimweleza Wizi Huo Na Ukimtaka Apeleke Hoja Bungeni. Kulalamika Kwenye Jamiiforum Hakusaidii.
 
Serikali imechota fedha nyingi kwenye hii mifuko kiasi kwamba ni vigumu kujiendesha na ku survive hata kwa miaka kumi. Ndio maana kila siku wanakuja na kali kumbana mwanachama. Ni kama ile sinema ya fao la kujitoa, nchi hii ni hatari tupu
 
Kila Utakaesoma Hapa Naomba Umtumie Meseji Mbunge Wako Ukimweleza Wizi Huo Na Ukimtaka Apeleke Hoja Bungeni. Kulalamika Kwenye Jamiiforum Hakusaidii.

Walikosea kukata mipaka huku ninapoishi, matokeo yake sina Mbunge
 
Kwani hawajui??!!
Kamati husika nayo haijui?????
Waziri kivuli yuko wapi juu ya hili???!!

Yani movement kubwa hivyo unadhani iko unnoticed??!!
 
watakuwa wanataka kuimaliza hiyo bima coz serikali wameshachota hela zote
 
Serikali hii ni mbaya yaani kila kona tabu Bima ya afya ni shidaaa halafu Wabunge kimya sana. Njia ni kuiondoa Ccm tu kama liwalo na liwe tu.
 
Wanakaa kwenye vikao wenyewe, wanatunga taratibu wenyewe, wanalazimsha zifuatwe wenyewe bila kutoa elimu yoyote. Na mbaya zaidi hiyo bima ipo kiserikali na wengi serikalini hawana sauti ya kufanya chochote, kikishapangwa kimepangwa ni utekelezaji tu hata kama kinaumiza.
 
Wabunge wa siku hizi wamekuwa wasaka tonge tu, jamii wanataijuaje kama ina matatizo wakati wote wamekimbulia mjini. Wabunge hawasikilizi matatizo maana sasa hivi wanafikilia jinsi ya kurudi bungeni. Bima ya afya ndiyo mama wa ikulu maana kula kwake kunategemea mfuko huu
 
Tumekusoma mkuu.ila kabla hatujafikisha kwa wabunge wetu tunaomba utupe maelezo ya masharti ya wategemezi ktk bima nyingine mf AAR,NIC,MEDEX nknk. ili tuwe na data za kujitosheleza
 
Kumbe ndiyo UPUUZI waliokuja nao sasa!? NHIF ni mfuko mwingine wa watu kupiga madili, ni VEMA kila mtu akamjulisha mbunge wake kama mjumbe alivyoshauri hapo juu, tunaweza kupindua maovu na mabaya yote kama tuko serious, huu ni wizi mkubwa sana kuliko ule wa Escrow!
 
Tumekusoma mkuu.ila kabla hatujafikisha kwa wabunge wetu tunaomba utupe maelezo ya masharti ya wategemezi ktk bima nyingine mf AAR,NIC,MEDEX nknk. ili tuwe na data za kujitosheleza
Utakuwa sio raia wewe, Bima ya Afya ya Taifa unataka data za private ili ujue ishu za masharti ya wategemezi???!!!
 
Mimi Nilishaanza, Kwa Kuanza Nilianza Na Mheshimiwa Rais Mwenyewe, Nikaja Kwa Mh Zito,nikamtumia Mh Kigwangala. Nanyi Endelezeeni Kwa Wahemiwa Waliobakia Hadi Wasikie Hiki Kilio Chetu. MADAI YETU YAWE,1.NAFASI ZIONGEZWE TOKA SITA HADI 8,wakwe 2,wazazi 2,wewe Na Mkeo Mpo 2,angalau Watoto 2. 2.TUSIWEKEWE MIPAKA MTU WA KUMUWEKA KWANI NAWEZA NIKAWA WAZAZI SINA,WALIFARIKI NA NIKASOMESHWA NA SHANGAZI. AU NAWEZA KUWA NA MTOTO WA KAKA YANGU NAISHI NAE, 3.KUWAONDOA WATOTO KWENYE BIMA KILA WANAPOFIKISHA MIAKA 18 TUIKATAE UMRI HUO ANAKUWA HAJAMARIZA SHULE. Ongezeeni Na Mengine Mnayoyaona Yanafaa. Naomba Kila Mmoja Atume Meseji Ya Kumtaka Mbunge Wake Azuie Wizi Huu Wa Bima.
 
wameweka masharti mapya ya hovyo sana.1.wategemezi wengine wamewatoa.wamebakisha wazazi au wakwe,nafasi zipo sita,fikiria unawazai wote 2,unawakwe wote 2,wewe na mkeo mpo 2,halafu unawatoto 3. Maana yake watoto hawana nafasi hapo.2.ikitokea huna mke,wazazi wala mtoto,ila unakaka,shangazi aliyekusomesha hawamtaki umjaze kwenye bima hvy nafasi zote 5 zinapotea bure na gharama unazochangia hazipungui.3.mtoto wako akifikisha miaka 18 wanamtoa kwenye bima ilihali umri huo yupo kidato cha nne hajaanza kujitegemea hvy utakuwa unagharamia matibabu yake na bima wanakata kwa kiwango kilekile cha mwanzo hakipungui. Japo wengi mmekaa kimya kwa sababu mliowaingiza kwenye bima hawataondolewa sasa subirini sk apoteze kitambulisho chake cha bima ndo utajua ninachokizungumza hapa japo unakiona hakifai. Wabunge wote mtusaidie, rais jakaya kikwete hapa unahusika kutoa neno lako utusaidie tunanyonywa hapa.

[nyongeza ya hilo unakuta wewe na mkeo/mumeo ni wanachma halafu mnapigwa marufuku kuingiza ndugu mwingine cc tuliosomeshwa na akina wajomba na akina shangazi na hatukubahatika kupata watoto wa kuwazaa tumuweke nani...? Au tutalipaje fadhira kwa waliotukuza hadi tukafikia hapa..? Kuhusu miaka kumi na nane ya mtoto mimi nilishawahi kuwaambia walipoweka hili sharti walianagalia uhalisia wa kidemograpfia kwa nchi yetu...? Mtoto anaanza darasa la kwanza akiwa na miaka 7...miaka 14 anamaliza la saba...akifika miaka 18 yuko kidato cha tatu au cha nne utamtoaje...?
Kwanini wao wasibaki na sharti la idadi ya watu halafu mimi nijue nitakaye muweka...? Kuna mmoja nilimuhoji hivyo akasema eti kuna watu wanawaweka watu wa mbali wenye magonjwa sugu halafu bima inawalipia na wao wanalipwa kwa pembeni kama ni hoja ilitoka ofisi za bima ya afya kwakweli haina mashiko...]
 
Wanafanya hivyo ili wakusanye kiwango kikubwa,ila matumizi yapungue. NHIF si imekuwa kimbilio la serikali kuchota pesa kwa ajili ya kulipia mishahara na matumizi mengine.
 
Back
Top Bottom