Wabunge wawasha moto Dodoma

safi sana hii ndio kazi tuliyowatuma kuifanya niliangalia bunge marudio jana sa sita usiku star tv ukweli ni kwamba shelukindo pia alitumia maneno makali lakini spika hakusama neno lolote alipozungumza machali likawa kosa. Makinda anapaswa kufuata nyayo za sitta.
 
Watanzania ni waelewa sio waoga wanafaham uchungu wa nchi hii hawataki kuharibu nchi yao. Mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia maandamano
Mbona hata CCM mlijaribu kuwafanya maandamano sema ya kakosa watu...au maandamano yanayofanywa na CHADEMA ni yapi na yanayofanywa na Nape na Mukama ni yapi...
 
Hivi wabunge wa CCM wakoje lakini?wanatuonaje sisi wananchi?hawataki kabisa kusikiliza hoja za msingi,wao wanachokisimamia kila siku bungeni na kukiona ni hoja nzuri ni maslahi yao na kutafuta namna ya kutunyonya,ACHENI UPUMBAVU USIMUONE KOBE KAINAMA ANATUNGA SHERIA.

Kuna mmoja jana alikuwa anatetea polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya washasha eti angeshangaa kuona polisi kutumia vitu hivyo kwa wanyama ila kwa watanzania wanaodai haki zao ni sawa.
 
wabunge wa upizani wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana na hawa mafisadi lakini wa kulaumiwa ni sie tunaowachagua wanakuwa wengi wanatuburuza.mie huwa nafikiri hizi roho zao sijui zinaujasiri namna gani ndio maana watu waliozoea kushangiliwa kama kina shibuda mnaona utumbo wanaouongea

Mie na wenzangu hatukuwchagua wabunge wa kijani, hao wakijani walichakachua kura zetu, hawana uchungu wanauchungu wa matumkbo yao
 
Watanzania ni waelewa sio waoga wanafaham uchungu wa nchi hii hawataki kuharibu nchi yao. Mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia maandamano

Ila mwenye akili kama zako anaweza kushabikia ujinga unaofanywa na wabunge wa ccm wakiongozwa na spika wao.,..
 
Kuna mmoja jana alikuwa anatetea polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya washasha eti angeshangaa kuona polisi kutumia vitu hivyo kwa wanyama ila kwa watanzania wanaodai haki zao ni sawa.

eeeeh!! mkuu acha uongo, km ni kweli basi nimeamini hapa duniani kuna watu na viatu.. mtu km huyo kweli unaweza ukamvua nguo halafu ukazichoma moto kisha umuache...
 
jamani msitegemeee jipya kutoka ccm may be tuingie vitani, nje yahapo nikuweka chama kingine ili kuwaadabisha hawa wanaojifanya sikio la kufa.
 
1 Tuache ushabiki usiokuwa na maana yoyote,nani asiyejua shule za kata hazina walimu hasa huko vijijini?
2 Kwa huu mgao wa umeme unaoendelea ni familia ngapi zinataabika kwa kukosa huduma muhimu kwa kuwa tu
shughuli za kiuchumi zinazoingizia familia kipato zimesimama?kama vile saluni,welding,vioski vya maji baridi,studio nk.
3.Maji ni tatizo mijini na vijijini ndio kero haswa wakina mama wanatembea kilomita nyingi sana kutafuta maji.
4.Hospitalini hakuna dawa,ukiugua leo kama huna hela wewe ni wakufa tu.
5.Rushwa imetawala katika taasisi nyingi tu za serikali,polisi,mahakama,uhamiaji na kwingineko ni shida tupu.
6Njaa iliyosababishwa na ukame ,kuna sehemu zina vyakula vya kutosha Tz hii lakini watu wanakufa kwa njaa.
7.Mazingira magumu ya kufanyia biashara ndogondogo.
8Kushuka kwa kiwango cha elimu,juzi nimesikia ya mwaka eti kwa kuwa wanafunzi wanafeli sana hesabu basi Wizara imeamua hesabu ziwe multiple choice,wizara ina ma dr lakini ndio hivyo tene.
9Ufisadi uliokithiri,wanaiba kweupe na hakuna wa kusema wala kukemea.
 
wekeni hii habari kamilii kwa liyesema kufunga mlngo zichapwe wengi wanadhani ni lema kumbe Living...... mwenye maelezo kamili jamani
 
You can fool some people some time,but you can't fool all the people all the time!!Ole wenu Magamba!!
 
Back
Top Bottom