Wabunge wawasha moto Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wawasha moto Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibakwe, Jun 29, 2011.

 1. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KITI cha Spika wa Bunge, Anne Makinda jana kilitikiswa kufuatia malumbano makali baina ya wabunge hasa wa kambi ya upinzani walipokuwa wakichangia hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu, huku mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje akidai kuwa nchi imejaa “wezi wasiokuwa na hatia”.Kidhalika kikao hicho cha bunge jana, kilishuhudia malumbano makali baina ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba, ambayo yalitanguliwa na mvutano baina ya Spika, Anne Makinda na Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali.

  Mvutano uliotokea kipindi cha bunge jioni, baina ya Mdee na Mabumba ulikwenda mbali kiasi kwamba Mdee alitoa matamshi makali kwa mwenyekiti huyo wa bunge akimwambia “….mwenyekiti ukiendesha mjadala huu kwa ushabiki, kiti kitakushinda”.

  Malumbano hayo yalisababishwa na kauli za Mbunge wa CCM, Zarina Madabida kusema wanaopinga posho za wabunge (sitting allowance) wanataka chama chao kiwafidie fedha hizo, jambo ambalo lilisababisha Mdee, kusimama kuomba mwongozo.

  Madabida alikuwa akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi za Waziri Mkuu ya mwaka 2011/12 jana na bila kukitaja chama hicho alisema kama kina dhamira ya kweli ya kukataa posho hizo kwanini wabunge wake wanataka kufidiwa posho hizo na chama.

  “Mwenyekiti hizi posho ni muhimu, mimi leo nikienda Dar es Salaam akinamama nakwenda kuwasaidia na hizi posho,” alisema Madabida.

  Baada ya Madabida kumaliza kuchangia hotuba hiyo na kukaa chini, Mdee aliomba mwongozo wa mwenyekiti huku akitaja kanuni ya bunge inayomtaka mbunge asiseme uongo na endapo atasema jambo hilo atatakiwa alithibitishe.

  Lakini kabla hajamaliza kukifafanua kifungu hicho, Mabumba alimtaka Mdee akae chini, lakini mbunge huyo kabla ya kukaa alisita kwa sekunde kadhaa kutii amri hiyo.

  Mabumba alimweleza Mdee kwamba Madabida wakati akizungumza hakutaja chama chochote na endapo angekitaja chama hicho ndio angetakiwa kuthibitisha.

  Baada ya ufafanuzi huo, Mdee alinyanyuka na kusema kwamba chama kinachopinga posho ni Chadema na NCCR-Mageuzi.

  “Kwa implication, Mheshimiwa Madabida alikuwa anavilenga vyama hivi… Mwenyekiti usikikalie kiti kwa ushabiki, kitakushinda,” alisema Mdee.

  Hata hivyo kabla hajaketi, ilisikika sauti ndani ya bunge ikisema “Jumamosi mligombea posho’’ hatua iliyomfanya Mdee kumtaka mwenyekiti huyo wa bunge kumlinda.

  Pamoja na ombi hilo la Mdee, Mabumba hakuzungumza lolote juu ya hali hiyo badala yake alimtaka mbunge huyo kukaa chini huku akiwaita wachangiaji wengine wachangie hotuba hiyo ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu.

  Machali na Spika
  Mvutano baina ya Machali na Spika Makinda, ulitokea katika kipindi cha asubuhi, kufuatia mbunge huyo wa Kasulu Mjini kudai kuwa “…kuna mambo yanafanyika kihuni ndani ya serikali”.

  Machali alisema mwaka uliopita zilitengwa zaidi ya Sh6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kidawe-Kasulu kwa kiwango cha lami lakini, fedha hizo hazijawahi kutolewa na kwamba hata katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi 2011/12 fedha hizo hazijatengwa.

  “Kuendelea kuwaahidi wananchi wakati jambo lenyewe halijafanyika ni uhuni wa serikali.., inawafanyia uhuni watu wa Kigoma,”alisema Machali.

  Kauli hiyo ilimfanya Spika Makinda kumtaka mbunge huyo kutumia lugha nzuri katika utoaji wa mchango wake na kuacha kutumia neno ‘uhuni’.

  “Barabara inaanza kujengewa Nyakanazi.., Nyakanazi sio Kigoma. Hivi Kigoma tumewakosea nini, Rais Kikwete alisema barabara itajengwa, lakini leo mmezihamisha fedha hizo sehemu nyingine, kama sio uhuni ni nini,”alihoji Machali.

  Kitendo cha Machali kurudia neno hilo kilimfanya Spika Makinda kumwonya tena mbunge huyo na kumweleza kuwa akitumia neno ‘uhuni’ anaweza asisikilizwe na anaowapelekea ujumbe huo.

  Lakini Machali alionekana kutokubaliana na Spika kwa kujibu kuwa, “Hata Shelukindo alitumia neno ‘kijingajinga’ na alikuwa akitulenga sisi wapinzani, sasa sisi wapinzani tukitumia maneno ya ukali tutahukumiwa, spika tuwe na 'check and balance' (kuangalia usawa)”.

  Machali alikuwa akifanya marejeo ya mchango wa Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo (CCM), ambaye wakati akichangia alisema kumekuwa na wabunge wanaoingiza hoja za kijingajinga bungeni.

  Machali aliweka wazi kwamba wabunge ni kama wamejivua uwakilishi wa wananchi kwani wamekuwa mbogo dhidi ya hoja ya kufutwa kwa posho za vikao.

  Mbunge huyo alisema maendeleo ya Tanzania hayalingani na umri wa miaka 50 ya Uhuru wake na kwamba wananchi wa Tanzania hawana amani, bali wana utulivu ulioambatana na nidhamu ya woga.

  “Siwezi kukubali kuwa kuna amani, wakati watu wanawaza watapata wapi mlo, polisi wanaendeleza vitendo vya kuwapiga raia kama wakimbizi ndani ya nchi yao, Serikali inakaa kimya na kusema mamlaka husika ziachwe zifanye kazi yake,”alisema Machali.

  Kauli ya Wenje
  Naye Wenje aliungana na Machali akisema kuwa Tanzania haina amani bali wananchi wake wana nidhamu ya woga akihoji kwamba maana ya amani ni mtu kutangazwa kuwa ameshinda ubunge baada ya vurugu polisi kupiga mabomu ya machozi?.

  “Hapa mtu akieleza ukweli au watu wakiandamana wataelezwa kuwa wanataka kuchafua amani, hii si kweli,”alisema Wenje na kuongeza:
  “….. tutaandamana kwa sababu, maandamano ni lugha ya sauti isiyosikika na hata kesho tutaandamana tu,”.

  Alisema kuwa baadhi ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinaonyesha kwa baadhi ya Halmashauri nchini zina hati chafu, lakini serikali haielezi wakurugenzi katika Halmashauri hizo wamechukuliwa hatua gani.

  “Mimi nilitegemea Mkuchika (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI) wakati akisoma makadirio na matumizi ya ofisi yake atasema wakurugenzi hawa amewafuta kazi, nchi ina matatizo mnasema ina amani, amani ipi sasa,” alisema Wenje.

  Wenje ambaye ni mbunge wa Nyamagana alisema nchi imejaa wezi na inaendelea kuporwa lakini, serikali haionyeshi nia ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika. “Nchi imejaa innocent thieves (wezi wasio na hatia), lakini serikali haijali.

  Mimi nilitegetemea wakati Waziri (Tamisemi) aliposema kuna halmashauri nne zimepata hati chafu, nilitegema asema tayari wakurugenzi wake tumewafukuza na zingine zenye kasoro, wakurugenzi wako under probation (chini ya uangalizi) na wakirudia hivyo miaka miwili waondoke. We must sack them!”alisisitiza.

  Aliendelea,”ATCL is almost dead due to poor management, (imekufa kwa sababu ya uongozi mbovu). Nchi iko looted (imeporwa). Tulikuwa na Deepgreen Finance na sasa tuna issue (suala) la rada. Kwa nini hatuchukui hatua?”alihoji.

  Wenje aliitaka serikali ichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika, akibainisha kuwa kuendelea kuwalea mafisadi na watu wasiowajibika, ni tatizo ambalo siku moja, litagharimu amani ya nchi.
  Katika hatua nyingine mbunge huyo aliendeleza madai ya chama chake kutaka posho ifutwe akisema “kwenye suala la posho za vikao (Sitting allowance) haturudi nyuma, na as from tomorrow (kuanzia kesho), tunaomba mtuletee fomu mbili ili sisi (Chadema) tusisaini fomu ya posho hizo.”

  Watanzania ndani ya Chupa
  Mapema, Shellukindo aliwagutua wabunge pale aliposema Watanzania ni kama wako kwenye chupa hivyo kutofahamu chochote kinachoendelea katika nchi nyingine.

  Shelukindo alisema, “ Ukiwachukua panzi ukawatumbukiza ndani ya chupa wataruka na kukosa chakula na baadaye wataanza kuumana, Tanzania tuko ndani ya chupa, nchi ina kila kitu, lakini Watanzania bado masikini, tumebaki kufanya siasa za kuchafuana.”

  Alisema misaada mingi inayotolewa haiwafikii walengwa lakini, wabunge wamebaki kujadili hoja sizizo za msingi bungeni.

  “Ajira kwa vijana hakuna, ndio maana wakiambiwa waandamane wanakubali, ukabila, udini, mauaji ya albino. Jamani Watanzania tumefungwa, tupo ndani ya chupa tumefungwa,” aliongeza.

  Alisema Watanzania ili watoke ndani ya chupa, kila mtu anapaswa kutekeleza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kumwomba Mungu, huku akitolea mfano nchi ya Rwanda ambayo ilikuwa katika vita, lakini kwa sasa imepiga hatua kimaendeleo.

  Naye Mbunge wa Lindi Mjini Salum Barwany, alipendekeza serikali kuanzisha mjadala wa kitaifa ili watu wajadili matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi kwa kuwa serikali, inaonekana kushindwa.

  Alisema serikali imeshindwa kutekeleza ahadi za rais anazozitoa maeneo mbalimbali nchini ikiwamo Lindi mjini na hili linawafanywa wananchi wakose imani naye na serikali yake.

  Barwany ambaye alikuwa akizungumza kwa hisia kali bungeni, alisema kuwa kitendo cha serikali kutotekeleza ahadi hizo za rais ni kumdharau rais mwenyewe ambaye maagizo yake, ni zaidi ya sheria.

  “Kauli ya rais ni ya thamani kuliko hata sheria. Sasa rais kaja Lindi na akatuahidi soko kuu bandari, maji, uwanja wa ndege wa Kimataifa, mashamba ya mkonge na mambo mengine kibao, lakini mpaka leo anapobakiza miaka mitatu, hakuna kinachofanyika,”alisema Barwany.

  Alihoji “Ahadi za rais ziko wapi Lindi leo? Kama nyie serikali mnamdharau rais wananchi watafanya nini? Leo manung’uniko kila kona. Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa na sio mipango isiyotekelezeka ya Kilimo Kwanza, ili watu wajadili namna ya kutatua matatizo yao.”

  SOURCE:Mwananchi
   
 2. samito

  samito JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 621
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hawa magamba wanaudh sana, ndo mana mwana Lema alitaka mlango ufungwe wazichape...
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  haa kungekuwa palestina ilibidi mwanaharakati mmoja awashitue na bomu pembeni ya BUNGE ili wajue watu wamechoka
   
 4. m

  migomo ya vyuo Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman9 naombeni tuweke sawa. aliyeropoka mlango ufungwe sii lema ni mbunge wa mtera MH. LIvingstone lusinde. A.K.A KIBAJAJI. Lema anayo akili hawezi Ropoka kijinga namna hiyo
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nchi imekumbwa na kiza kizito jaman walionamwanga wanadharaulika tunaelekea shimoni nahisi suluhu ya haya yote ni kupata viongoz wanaojitambua, wenyeuzalendo na uchungu na nchi yao. Pia its very possible kufanya maandamano ya amani ya kupinga uongozi wa kipuuzi wa JK lkn wa tz waoga jaman mpk lin? we hav to show them that we got tired of the situation
   
 6. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  halafu Jk mbona kama hajielewi haya matatizo anayahangaikia kweli au ni route tu?
   
 7. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  wabunge wa upizani wanafanya kazi ktk mazingira magumu sana na hawa mafisadi lakini wa kulaumiwa ni sie tunaowachagua wanakuwa wengi wanatuburuza.mie huwa nafikiri hizi roho zao sijui zinaujasiri namna gani ndio maana watu waliozoea kushangiliwa kama kina shibuda mnaona utumbo wanaouongea
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,992
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Hivi wabunge wa CCM wakoje lakini?wanatuonaje sisi wananchi?hawataki kabisa kusikiliza hoja za msingi,wao wanachokisimamia kila siku bungeni na kukiona ni hoja nzuri ni maslahi yao na kutafuta namna ya kutunyonya,ACHENI UPUMBAVU USIMUONE KOBE KAINAMA ANATUNGA SHERIA.
   
 9. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  acha uongo. mazingira gani hayo ? ina maana wabunge wako wa chadema huwa wanakaaga juani huku wa ccm huwa ndani kwenye a/c? fafanua zaidi
   
 10. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  sina muda
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,292
  Likes Received: 19,446
  Trophy Points: 280
  chizi sio lazima uokote makopo
   
 12. c

  chief m Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania ni waelewa sio waoga wanafaham uchungu wa nchi hii hawataki kuharibu nchi yao. Mtu mwenye akili timamu hawezi kushabikia maandamano
   
 13. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,408
  Likes Received: 1,965
  Trophy Points: 280
  tuwalindie amani ili muendelee kula mlivyodhulumu? safari hii vitawatokeeni mbavuni kama sio puani.nani alikwambia amani inapatikana kwa wachache kula na kusaza wengine kukosa hata mlo mmoja? rudi darasani ndugu haya mageuzi hayaletwi na chadema chadema inachofanya ni kufumbua watu macho.
   
 14. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kweli kabisa mkuu, mimi huwa nafarijika kuona wanaweza.... hawa wabunge wa upinzani though ni wachache wanajua sana mitego ya hao walio wengi.. chamsingi waunganishe nguvu wafanye kweli... WABUNGE WA UPINZANI WANAWEZA!
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu wewe ni chizi, kifupi unastahili kupelekwa Dodoma pale Mirembe hospital, wewe ni chizi!
   
 16. MANI

  MANI Platinum Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Message sent and delivered !
   
 17. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Unategemea wakurugenzi wa halmashauri kufukuzwa? sio rahisi kumbuka ndio wanaowapitisha wabunge na raisi ktk uchaguzi{wachakachuaji matokeo) mkuchika hawawezi atacheka tu wasije wakawaumbua wanafanya wanavyo taka ...kazi kwelikweli
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nashangaa upotoshaji huu...
   
 19. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  baada ya matokeo ya ubunge ya 2015,kama jimbo langu bado litakuwa na M'bunge wa magamba,nahamia jimbo la m'bunge wa CDM!!
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kweli kuunganisha nguvu ni mhimu sana lakini unaungana na nani...Mrema...hahahahaha
   
Loading...