Wabunge watoro bungeni wawajibishwe

Ekyoma

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,922
2,000
Wakati Bunge likiwa kwenye vikao vyake muhimu vya bajeti,
mbunge wa Kigoma mjini,yupo ziarani ktk nchi za ughaibuni akijivinjari!

Imekuwa ni tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya wabunge kutoroka bungeni na kwenda kufanya shughuli tofauti na uwakilishi wao.Ifike mahali sasa bunge ikomeshe tabia hii kwa kuweka sheria kali.

Zitto ni mmoja wa wadau wa kubwa wa uchumi/bajeti,tulitegemea michango mizuri toka kwake.

Pili,wapiga kura wajimbo lake hakuwatendea haki,kwa kutokuhudhulia vikao vya bunge.

Bunge liwe linatoa ruhusa kwa wabunge kutokuhudhulia vikao kwa sababu za muhimu kama vile maradhi(ugonjwa),kuhudhulia misiba.

Lakini sababu zisizo kuwa na mashiko,kama ziara za kirafiki,sherehe nk,zisipewe nafasi.

Taifa linapoteza fedha nyingi,kwenye uchaguzi na kuwatunza viongozi wetu,inapotokea mbunge hatimizi wajibu wake ni hasara kwa Taifa.

FB_IMG_1497080617820.jpeg
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,946
2,000
Tangu walipoacha bunge kutangazwa live hiyo hali imekuwa ni ya kawaida ya mahudhurio kuwa ya wachache sana! Wakati ule bunge lilipo kuwa linaoneshwa mubashara yaani live wabunge walikuwa Walau wakihudhurua Kwa wastani lakini tangu Napeee alivyo zuia basi wabunge nao wakaona afadhali watapata kustirika madhaifu Yao! Mleta mada ulichosema Ndiyo hali halisi anaebisha aende akaone! Haiwezi kuwa swala la kuomba ruhusa , yani itakuwa ni coincedence ya aina gani kwamba Kwa mfululizo wa Siku nyingi wabunge walio wengi wawe na udhuru / dharura za Mara Kwa Mara? Ruhusa inatarajiwa itokee Mara chache na Kwa wabunge wachache siyo kiasi kinachotokea!
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,017
2,000
Wakati Bunge likiwa kwenye vikao vyake muhimu vya bajeti,
mbunge wa Kigoma mjini,yupo ziarani ktk nchi za ughaibuni akijivinjari!

Imekuwa ni tabia iliyozoeleka kwa baadhi ya wabunge kutoroka bungeni na kwenda kufanya shughuli tofauti na uwakilishi wao.Ifike mahali sasa bunge ikomeshe tabia hii kwa kuweka sheria kali.

Zitto ni mmoja wa wadau wa kubwa wa uchumi/bajeti,tulitegemea michango mizuri toka kwake.

Pili,wapiga kura wajimbo lake hakuwatendea haki,kwa kutokuhudhulia vikao vya bunge.

Bunge liwe linatoa ruhusa kwa wabunge kutokuhudhulia vikao kwa sababu za muhimu kama vile maradhi(ugonjwa),kuhudhulia misiba.

Lakini sababu zisizo kuwa na mashiko,kama ziara za kirafiki,sherehe nk,zisipewe nafasi.

Taifa linapoteza fedha nyingi,kwenye uchaguzi na kuwatunza viongozi wetu,inapotokea mbunge hatimizi wajibu wake ni hasara kwa Taifa.

Mpaka mtu unajua mtu fulani hayupo basi mchango wake ni muhimu!Ni vigumu mbunge wa ccm kutokuwepo bunge la bajeti halafu watu wakajua kuwa fulani hayupo coz akiwepo asiwepo hana msaada!
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,117
2,000
Mpaka mtu unajua mtu fulani hayupo basi mchango wake ni muhimu!Ni vigumu mbunge wa ccm kutokuwepo bunge la bajeti halafu watu wakajua kuwa fulani hayupo coz akiwepo asiwepo hana msaada!
Zitto ni mbobevu katika uchumi. Uwepo wake bungeni hutusaidia tusio wachumi kupata Mwanga.
Sasa mbunge mwenye fani ya sociology ataweze kuuchambua uchumi vixuri?
Ceteris perubus,multiplier effects, demand and supply, PPF, nk nk.
Akirudi atataka mikutano ya hadhara mwembeyanga.
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,017
2,000
Zitto ni mbobevu katika uchumi. Uwepo wake bungeni hutusaidia tusio wachumi kupata Mwanga.
Sasa mbunge mwenye fani ya sociology ataweze kuuchambua uchumi vixuri?
Ceteris perubus,multiplier effects, demand and supply, PPF, nk nk.
Akirudi atataka mikutano ya hadhara mwembeyanga.
Waliopo wajitutumie,wapige desa vya kutosha!Nadhani wengine wampigie simu awape mchango wake ili waongezee kitu kwenye kujadili!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom