Wabunge wataka siri za mgodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wataka siri za mgodi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,442
  Trophy Points: 280
  Wabunge wataka siri za mgodi
  Tuesday, 14 April 2009 16:06
  Na Gladness Mboma

  Majira

  KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja kuwasilisha taarifa za siri zitakazojitosheleza pamoja na mikataba ya mgodi wa almasi wa Mwadui (WDL) uliopo Shinyanga.

  Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika ndani ya kamati hiyo iliyokutana Dar es Salaam jana, Bw. Ngeleja alitakiwa kupeleka taarifa zilizojitosheleza baada ya kuwasilisha ripoti inayohusu mgodi huo ambayo haikueleweka kwa kamati.

  "Ripoti tumeipokea lakini haijajitosheleza hata kidogo, hivyo tumemtaka Bw. Ngeleja akatuandalie nyingine na kutuletea taarifa kamili. Tumemtaka pia atuletee taarifa za siri zilizojitosheleza na mikataba ya mgodi wa WDL kwani ripoti nzima, haijitoshelezi," kilisema chanzo hicho.

  Bw. Ngeleja aliwashitua wabunge katika maelezo yake baada ya kuwaeleza kuwa kampuni ya Petra Diamonds Limited ambayo imenunua kampuni ya Willcroft itamiliki asilimia 75 bila ya kutolea ufafanuzi.

  "Kamati imemtaka Bw. Ngeleja kutupa ufafanuzi ni kwa nini kampuni hiyo ichukue asilimia 75? Kuna mkanganyiko mkubwa katika ripoti hii, hajatueleza sisi Watanzania tutavuna nini kwenye mgodi huo," chanzo hicho kilifafanua.


  Pia kamati ilishangazwa na deni kubwa la dola za Marekani milioni 87.5 lililoachwa na Willcroft ambalo Serikali inapaswa kulilipa kabla ya kununuliwa na Petra Diamonds Limited.

  "Tatizo ni kwamba wawakilishi wa Serikali kwenye WDL hawajawahi kuhudhuria kikao hata kimoja na ndio maana kampuni hiyo iko kifua mbele. Uzembe huu ni wa kujitakia," alisema.

  Wawakilishi wa Serikali kwenye Kampuni ya WDL, hawajahudhuria vikao kumi. Baadhi ya wawakilishi hao ni Bw. Fred Mpendazoe (Mbunge wa Kishapu), Bi. Lucy Mayenga (Viti Maalumu) na wengine kutoka Wizara za Nishati na Madini na Fedha na Uchumi.

  Alisema hali hiyo ndiyo inayosababisha sekta hiyo ya madini kulegalega na baadhi ya kampuni kufaidika na madini, huku Serikali ikiachiwa mzigo mkubwa wa madeni.

  Awali Kamati hiyo iliruhusu waandishi wa habari kuingia katika kikao hicho. Baada ya Bw. Ngeleja kusoma ripoti yake aliiomba kamati hiyo kuijadili wenyewe bila ya waandishi.

  Mvutano mkali uliibuka kati ya wabunge wa kamati hiyo ambao baadhi yao walitaka waandishi wabaki na wengine wakitetea kauli ya Bw. Ngeleja ambaye alisisitiza Mwenyekiti atatoa taarifa kwa waandishi baada ya kumalizika kwa kikao hicho, jambo ambalo wabunge hao waliridhia kwa shingo upande.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ukisha kula 10% vikao vya nini tena... Hayo ndo mawazo ya watanzania wengi walio ndani ya serikali na CCM. Ndiyo maana hata wakiwa bungeni utasikia wanajadili mavazi ya akina mama huku madini yanaibiwa, hawana hata aibu!! Shame on you Ngeleja na wenzako.... Hivi mnadhani hata mjilimbikizie madini na fedha mpaka mjaze mabenki...mtakufa nazo?? Kwani Mobutu seseseko yuko wapi?? CCM mjiulize haya maswali... Mzee mkapa!! Huo mgodi kumbuka hata ukifa tutautaifisha na wamiliki wake wakati huo tutawafunga jela!! Shauri yako!!
   
 3. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani hii ni hatari kwa ustawi wa taifa letu. Yaani wote kwa umoja wao hawajahi kuhudhuria?. Ninawaomba wenye uwezo watuletee taarifa zaidi ili kujua kama hao wajumbe hawajawahi kukamata mshiko wa vikao. Na kama waliukamata huo mshiko, waliukamataje wakati hawakuwepo kwenye vikao? Pia sheria zinasemaje kuhusu watendaji walioteuliwa kutohudhuria vikao wakati wote wa uteuzi wao.

  Kwa kweli tunakazi ya kuonyosha nchi hii!
   
Loading...