Mkuu ukichukua ela ya safari hata kama umeenda safari mwisho wa siku unatakiwa kufanya retirement ya namna gani umetumia hela kwani unaweza ukawa umepewa dola 200 kwa ajili ya Hotel hivyo lazima uje na viambatanisho vya hotel uliyolala maana inawezekana ukawa umelala hotel ya dola 150 hivyo hiyo 50 ni change inabidi irudi (ela za safari huwa hazitolewi kama unavyotoka mshahara kwamba mwajiri wako hakufuatilii kwenye matumizi but kwenye posho za safari lazima mwisho wa siku ulete viambatanisho) nadhani wanajua taratibu unless kama alitaka mwongozo wa either azitumie ili safari nyingine ikitokea hatapewa posho ya safari atazitumia hizo hizo.
Wakati anachukuwa alikuwa hajui kama anasafiri acheni utoto arudishe pesa za walipa kodi.
Ndizo alizozitoa mchango kwenye harambee na kuwarudishia walipa kodi na si walipwa kodi.
Alitakiwa kurudisha pesa na kuandikiwa stakabadhi, siyo kutoa taarifa na kuomba muongozo.
Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
Barua aliyoandika kwa katibu wa bunge ilishampa mwongozo, either kurudisha ama kuwasaidia wapiga kura wake. Wewe ni nyang'au ama? waambie wabunge wa ccm warudishe fedha au watolee taarifa walizifanyia nini
Sasa anasubiri nini kuzirudisha?
Hao ndo wabunge wa CHADEMA, CHAMA CHA UPINZANI.hAHAHAHA ,wanayoyafanya hakika ni ya kuzidi kumuumiza mTANZANIA.
Harambee za dharura ni nadra. Nyingi hupangwa na kuandaliwa kwa muda wa kutosha. Maelezo ya ziada kuhusu udharula huu yanahitajika.
Leo asubuhi niliposikia kipindi cha tuongee magazeti juu ya Wabunge kutafuna posho ovyo wakiwemo na wa upinzani moyo uliumia sana. Nimefuatilia gazeti la Raia Mwema na ndo maana nikaamua kumpongeza huyo bwana mdogo Nassari kwa kweli ni mfano wa kuigwa
Amekiri kweli kuwa alichukua posho kwa ajili ya safari ya kwenda Malaysia lakini ikatokea dharula ya Harambee jimboni kwake akaona ni vyema akajumuika na wananchi waliomchagua badala ya kusafiri.
Kizuri zaidi ni kwamba aliandika ujumbe kumtarifu katibu wa bunge juu ya dharula iliyokuwa imejitokeza na kuomba muongozo wake kuhusiana na fedha hiyo na nakala akapeleka kwa katibu mkuu CHADEMA.
Swali la kujiuliza hapo ni wabunge wangapi wa CCM wanaoweza kufanya hivyo ? nimesikiliza utetezi wa Godfrey Zambi mbunge wa Mbozi kwa kweli haukunishawishi. Yeye anasema alikuwa na ugeni wa Kinana mkoani kwake na baada ya hapo alifiwa na mdogo wake. Ni kweli kuwa asingeweza kuendelea na safari kwa sababu hizo lakini kwa kiongozi makini unapaswa kutoa taarifa kwa wakati juu ya yaliyokusibu kama alivyofanya Nassari na usisubiri mpaka uhojiwe na waandishi wa habari
Nawasilisha