Hivi wabunge yale maneno wanayatoa wapi?
Mbunge wangu toka achaguliwe amefanya mkutano mmoja tu. Na huo mkutano alihutubia mpaka akaondoka,
Hakutuuliza tunataka nini? Hakutuuliza tuna shida gani akaisemee? Alikuta barabara mbovu akapita akaiacha ilivyo sikusikia akiisemea.
Zaidi alikisemea chama chake na mengine ya huku ambayo sijui aliambiwa na nani,
Nadhani anatekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chake ambayo pia hatukuitengeneza sisi ilitengenezwa na chama chake sasa ni vipi ananiwakilisha? Bado anakiwakilisha chama chake.
Pengine tunahitaji katiba mpya sio hii pendekezwa mpya kabisa, sio ile rasmu ya waryoba mpya kabisa kabla ya hiyo katiba mpya kabisa tupige kura za maoni kwanza kuhusu muundo wa serikali 1, 2 au 3 ili wasiende tena kubishana bungeni huku kila mmoja akisimama kwenye msimamo wa chama chake na si wananchi anaowawakilisha. Hata iliyopita kama wabunge wangetuwakilisha cc naamini isingekwama.
Lkn ccm waliwakilisha msimamo wa chama chao na upinzani wakawakilisha msimamo wa kambi rasmi ya upinzani/ukawa mwisho bunge likavunjika, laiti wangewakilisha wananchi lazima wangekuwa na kauli inayofanana kuhusu muundo wa muungano na kama ni kukinzana pengine ingekuwa zanzibar na bara na wala si ccm na upinzani.
Bado nauliza hivi wabunge wanamwakilisha nani? Mbunge aliemuita mnyika mwizi aliwawakilisha wapiga kura wake? Hicho ndicho walichomtuma?
Halima mdee kumzuia askari asimtoe nje mnyika alimwakilisha mpiga kura wake? Hilo ndilo alilomtuma?
Wanaojibu ndioooooooo! Wanamwakilisha nani? Na wanaojibu siooooooo! Wanamwakilisha nani?
Kwanini kabla ya kikao cha bunge mbunge asiitishe mikutano bungeni kwake, ajenda za kikao hiki ni 1, 2, 3 wananchi waseme kwa ajenda hizo sisi ni ndiooooo au sisi ni siooooo! Kisha akawawakilishe?