Wabunge wana kinga, sisi twende kwa nani?

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,031
1,603
Kufuatia matamshi ya mkuu wa mkoa flani na matamshi ya mkuu wa wilaya, wabunge kwa ujumla wao wamekubaliana wakuu hao waitwe kwenye kamati ya bunge inayoshughulika na maadili ili kujibu tuhuma ya matamshi yao dhidi ya bunge.

Binafsi nimefurahishwa na maamuzi yaliyofikiwa na bunge.

Lakini nilitegemea bunge lingeenda mbali zaidi na kututetea hata sisi tusio na cheo chochote wala pesa ya kuweka wakili ili kudai haki yetu mahakamani. Leo hii DC akiamua niwekwe ndani labda kaambiwa na mkewe au binamu yake ambaye mimi nafanya naye kazi ofisi moja, mtetezi wangu ni nani? Bunge lingetuangalia na sisi wanyonge.
 
kupitia hilo na wewe utaneemeka.
angalia maazimio yote manne
 
Back
Top Bottom