armanisankara
JF-Expert Member
- Jul 15, 2011
- 283
- 49
wabunge wamechoka kukaa Dodoma katika kipindi hiki cha mkutano wa bajeti. hawataki yu kusema kuwa wamechoka mazingira ya mji huo na hata shughuli za bunge kwa kuwa bado wanazitamani posho nono wanazopewa. na kwasababu hii baadhi ya wabunge tena wengi tu wapo wapo tu huko bungeni ilimradi wana uhakika kila siku wanatia kibindoni posho. kwa kweli ni haibu kusikia kikao cha muhimu cha bunge kinaahirishwa kwasababu ya waheshimiwa hawapo ukumbini . ni kweli wamechoka na ndiyo maana hata wakiwa katika mazingira ya jengo la bunge baadhi yao utawaona tu wapo wapo nje ya ukumbi wa wa mikutano. wanachokifanya wanakijua wenyewe ili tu siku iishe wahesabu klichopatikana.