Mara nyingine mtu kupita bila kupingwa siyo kwa sababu anakubalika, hapana, bali inatokana na rushwa au ghilba, kwa watu wanao onesha nia ya kutaka kugombea na wenye uwezo wa kushinda au kuleta changamoto ya nguvu kwa muhusika mkuu. Kama ilivokuwa kule Bumbuli kwa Januari Makamba na kule kwa Nimrod Mkono (kwa kutaja mifano michache)
Sababu za watu kupita bila kupingwa zingali zinaishi, na wahusika wamekuwa wakitumia mbinu tofauti kufanikisha malengo yao, kuna mahali katika uchaguzi wa 2010 wagombea wa CHADEMA, kwa maksudi walijaza fomu za kugombea kwa kufanya makosa, ambapo baada ya kukatiwa rufani na wapinzani wao walishindwa na hivo kukosa haki ya kugombea.
Nimeanzisha huu uzi ili kutoa angalizo kwa watendaji wa UKAWA kuwakumbusha kuwa, wanaosema bao la mkono wana mbinu nyingi na chafu kufanikisha malengo yao, kwa hiyo wawe na tahadhali za kutosha kwa watu wanaopitishwa kugombea katika ngazi tofauti tofauti yaani ubunge na udiwani na hata rais.