Wabunge wakomaa: Ngeleja, Jairo watakiwa kuondoka; Pinda ataka mjadala uahirishwe kwa siku 21

Status
Not open for further replies.
Katibu Mkuu wa Wizara kuandika barua kama ile ni lazima alikuwa amepata idhini through a File Minute ya Waziri kuafiki prposal hiyo. Kwa hiyo nadhani Ngeleja aliposita kujibu juu ya hili swala ana hofu zake. Lakini watakuwa wanamtoa kafara huyu Katibu Mkuu kama watamfukuza kazi kwa shauri hili kwa sababu mashirika na wizara nafikiri zote zina kasma ya ku-lobby wanasiasa na wabunge. At the end of the day budget ya wizara hii itaongezwa baada ya kupitiwa upya kwa hiyo matumizi hayo yatakuwa yamekuwa effective although through unquestionable means. Pia kuleta barua hii bungeni inaweza kuwa ni moja ya intrigues among senior civil servants hasa ukizingatia kuwa huyu Jairo ni mmojawapo wanaosemekana kufikiriwa katika nafasi ya Katibu Mkuu wa Raisi baada ya kustaafu kwa huyo wa sasa. Hili litamchafulia faili lake huyu Jairo - ambao baadhi ya wanaomfahamu wanasema ni effective and efficient civil servant.
Aisee yani unasema Jairo ni "effective and efficient civil servant" kama ndivyo basi nchi hii imekwisha
 
Yaani lijamaa hauwezi hata kulielewa!! tena utakuta linalala kwa amani zake usingizi wa pono wakati nchi iko kwenye matatizo ! Yaani ni kama li FaizaFoxy liko ikulu!
nakwambia jamaa ni pimbi balaa sijawahi kuona !he look like child, poor to him ,very stupidy leader ,shame upon ccm !
 
Hata hivyo wabunge wamechelewa. Walitakiwa wahoji vipaumbele vya nishati tangu wizara ya fedha ilipowasilisha budget yake. Kafungu ka nistati ni kadogo sana, sijui watakuja na mipango gani!
 
Sasa hapo ndio tunapaswa kuhoji zile Ndiooooooooo wakati wa upitishwaji wa Bajeti ya Serikali iliyosomwa na Mkulo. Hivi wakati wapinzani waliposema bajeti hii ni mbaya na hasa walitoa tahadhari kuhusu umeme walikuwa wapi kuelewa hilo. Hii inaonyesha jinsi walivyo wavivu wa kusoma makablasha. Kama bajeti ya wizara ni mbaya na hasa kama inahusu takwimu basi bajeti nzima ya serikali ni mbaya. Kwa misingi hii inamaana burget nzima inaenda kufumuliwa tena yaani kujaribu kupata vyanzo vya mapato kwa ajili ya kutatua matatizo ya umeme, na inabidi serikali sio italazimika kuleta burget ya Wizara hii tuu bali sheria itakayo lekebisha mapungufu ya mafungu kwenye wizara zingine.

Tujiulize walitegemea watatatua vipi hili tatizo la umeme? Yaani Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu hawakuliona hili kama linakuja? Na wabunge wa NDIOOOOOOOOOOOOO wamejifunza nini kutokana na hizo Ndioooooooo zao?. Kama ni wavivu wa kusoma basi wawe wepesi wa kusikiliza ni kipi wapinzani wajaribu kuambia.

Kweli hatuna Uongozi makini.

NAWASILISHA.

Unajua wabunge hawa wa NDIOOOOOOOOOO mara nyingi ni wavivu sana wa kusoma yale makablasha ya badget,wanajua ikishafika muda wa kuunga mkono hoja na kwa vile wao ni wengi...ni just kushabikia tu na hizo NDIOOOOOOOOOO zao! Sasa kwa budget hii ya MEM nazani wameshajifunza!
Nakubaliana nawe Msafiri kuwa,lazima kuna badget tayari zimeshapitishwa wrongly kwa iyo the easy NDIOOOOOO!
Kwa biashara hii ya NDIOOOOOOOOOOOOOO na wakati ni SIOOOOOOOOOOOOOOO,hatuwezi kufika mbali!!!!!
 
sasa ccm wakiamua kufanya mambo kama haya ndo gamba limetoka hivyo but waamue kufanya kwa dhati kwa ajili ya kuirekebisha serikali yao waache mtindo wakufukuza wanachama eeeti ndo magamba!
 
tetesi zilizopo ni kuwa katibu mkuu wizara ya nishati na madini anashinikizwa kujiuzulu baada ya skandali ya barua yake aliyoandika kwa wakuu wa idara, na hii itasababisha bunge kuahirishwa jioni hii ili bajeti ya nishati na madini ikafanyiwe marekebisho na katib mkuu huyo kujiuzulu. Ngeleja kapona.Source! chini ya kapeti. tusubir session ya jioni
Mkuu naikubali sana hiyo source yako.
 
Umeongea ya maana sana. Why are they pretending not to know??? Hivi hizo billion anazochanga akiweka mfukoni? Mi ndio maana nimesema ingekuwa nchi za wenzetu hii ni kashfa ya kutosha kufanya serikali yoote ijiuzuru!
Na hapa ishu si giza wala kurekebisha budget. Kikubwa ni RUSHWA. Hiki ndicho cha kukomaa nacho maana ni kiini cha umasikini wetu including GIZA

Kuna maswali mengi sana ya msingi ya kujiuliza kutokana na kuahirishwa kwa hii hoja ya Ngeleja. Kwanza, budge kuu aliyosoma Mkullo ilijumuisha wizara zote including hii ya Nishati na madini, je serikali na hasa cabinet hawakuona mapungufu hayo? Je Baraza la mawaziri wanakaa na kupitia mapendekezo ya budget kabla ya kusoma bungeni? Kama jibu ni hapana kwa nini? Office ya Waziri mkuu kama kiongozi wa shughuli za serikali huwa inapitia na kuridhia na mapendekezo ya bajeti za wizara zote kabla ya kupeleka bungeni?

Nasema haya kwa sababu Waziri Mkuu Pinda alionekana kama hajui baadhi ya vitu kwenye bajeti ya wizara nishati na madini, na mbaya zaidi ni pale aliposema 'ameshtushwa' na taarifa kuwa Katibu mkuu wa wizara ya Nishati Ndugu Jairo aliandika barua kwa idara mbalimbali chini ya wizara yake akidai wachangie milioni 50 kila moja. Hivi inawezekana kweli mtumishi wa umma akachangisha zaidi ya BILIONI bila ya mkuu wa shughuli za serikali kujuwa? Ile inteligensia (and I am serious on this) wanayojivunia kutabiria hata fujo kabla maandamano hayajatokea kwa nini wasitumia kwenye vitu vya msingi kama hivi? Na kama Waziri mkuu hajui issue kubwa kama hii (BILLION NA USHEE SIO HELA NDOGO) ni vitu gani vingine hajui? Tutamwamini vipi Waziri mkuu akitupa taarifa za shughuli za serikali au kutetea utendaji wa vyombo vya serikali i.e mauaji Arusha kama waziri mwenyewe anaonekana kutojua nini kinaendelea kwenye idara mbalimbali?

Niposema Waziri Mkuu naomba ieleweke office yake, ana all the resources kwa nini ashindwe kujua baheti imejaa makengeza?
 
It's obvious kuwa Jairo ana backing ya Ngeleja na Malima, kwani atakuwa na interest gani as an individual kuhakikisha bajeti inapita kama sio interest ya kikundi chote cha majambazi?? Akifukuzwa kazi atakuwa katolewa tu kafara na lazima maisha yake yataendelea kuangaliwa vizuri kwake ataambiwa ajali kazini ila "pamoja tupo nawe" na wezi wenzake wataendelea kupeta, this is very possible in a country like ours.

Labda mzimu wa baba wa Taifa uamke hapo ndipo tutayaona mabadiliko ya kweli...sasa hivi ni kutoana kafara na kufunika kombe mwanaharamu apite na business iendelee as usual!
 
Baada ya wabunge wengi kuikomalia bajeti ya wizara ya madini na nishati na hasa kwa kushindwa kuja na mikakati madhubuti na inayotekelezeka ya kutatua tatizo sugu la mgao wa umeme unaoendelea nchini hatimaye bajeti hiyo imekataliwa rasmi leo na serikali imeomba wiki 3 kwenda kuiandaa upya.

Akikubaliana na hoja za wabunge wengi waziri mkuu pinda aliliomba bunge wapewe muda huo ili wajipange upya.pia pinda amesema amefedheheshwa sana na kitendo cha katibu mkuu wa nishati na madini ndg Jairo ambaye ameandika barua kwa taasisi zilizoko chini ya wizara hiyo wachange 50 mil kila moja ili kutumika kuhakikisha bajeti yao inapita! Barua hiyo imesomwa bungeni na mh beatrice shelukindo.

Jamani haya yametokea mjengoni jioni hii .
 
Hili ni swala zito, wizara inatakiwa kusafishwa kwani haiwezekani Jairo afanye hayo bila Waziri na Naibu waziri kujua hili. Kinachotakiwa sasa ni wakurungunzi wakuu wote wa mashirika yaliyo chini ya wizara hii wahojiwe na kamati maalumu kujua ni mara ngapi wamepata kutoa fedha za namna hii? na je ni kweli kamati ya bunge ya madini imekuwa ikihongwa na wizara?
 
but wizara kutoa pesa za kulobby haianzi na jairo peke yake. Huo ni mchezo wa wizara lukuki. Kila taasisi chini ya wizara lazima ichangie hako kabajeti... Let alone kumchangia waziri mafuta akienda jimboni, utadhani anakwenda na treni akiendesha mwenyewe......
Na katibu mkuu hafanyi peke yake yeye huwa anasaini tu barua, ngeleja naye lazima alikuwa na habari nadhani wangepisha njia wote....... Pengine waziri kivuli awasaidie kukamilisha hoja ya serikali..
tatizo ni system yoote mbovu ya jk na serikali yake!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom