Wabunge Waibana Serikali

Wabunge Waibana Serikali

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
Na Midraji Ibrahim, Mwananchi

Posted Jumatatu,Aprili22 2013 saa 20:49 PM

KWA UFUPI
Alisema kwenye hotuba ya waziri hakuna sehemu ambayo imekuja na suluhisho la matatizo ya wakulima nchini na akisema ni ukurasa wa 50 tu ambao unataja rasimu ya kuanzisha mfuko wa bei ya mazao.




Dodoma. Wakati Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili kwa umaskini kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, wabunge wameishukia Serikali kwa kutenga fedha kidogo kwenye Bajeti ya Kilimo.


Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), unaonyesha kuwa Burundi ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wengi maskini ikifuatiwa na Tanzania kwenye eneo hilo.


Burundi inaongoza kwa kuwa na asilimia 81.32, Tanzania ikifuatia na asilimia 67.87, Rwanda asilimia 63.17, Kenya asilimia 43.37 na Uganda 38.01. Utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia idadi ya watu wanaoishi kwa Dola 1.25 kwa siku.



Jana, baadhi ya wabunge wakiwamo wa CCM, walikataa kuunga mkono Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wakisema haiwezi kuinua maisha ya wakulima, ambao ni asilimia 70 ya Watanzania.


Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alikuwa wa kwanza kuchangia bajeti hiyo na kusema baada ya kufuatilia kwa makini maelezo ya waziri, hakuna taarifa njema kwa wapigakura wake hivyo hawezi kuunga mkono hoja hiyo.



Alisema kwenye hotuba ya waziri hakuna sehemu ambayo imekuja na suluhisho la matatizo ya wakulima nchini na akisema ni ukurasa wa 50 tu ambao unataja rasimu ya kuanzisha mfuko wa bei ya mazao.


Lembeli alisema hotuba hiyo imewaacha wakulima kwenye mazingira magumu ya kukata tamaa na hasa wale wa pamba na tumbaku kwenye jimbo lake...



“Akilima ekari moja ya pamba kipato chake kwa mwaka hakizidi Sh200,000 sasa leo Serikali inakuja inasema imekuja na rasimu, imekamilisha… ah, siungi mkono hoja.” Alitaka kujua jinsi Serikali ilivyojiandaa kupambana na bei ya pamba iwapo itashuka.


Alisema jimboni mwake kuna wakulima wazuri wa tumbaku wanaoliingizia taifa Sh15 bilioni kwa mwaka, lakini... “Wakulima wa tumbaku wanabambikiwa madeni, matokeo yake mwisho wa mwaka hawalipwi, nimepiga kelele, nimemwomba waziri atembelee sijui ameweka nini masikioni mwake, hasikii.”


Alisema matokeo yake, viongozi wa Serikali hasa ofisa ushirika wa wilaya, ambaye alisema hayupo kwa masilahi ya wakulima ndiye anayechonga michongo ya kuwaibia wakulima.



Lembeli alisema kuna wakulima ambao waliuza mazao tangu mwaka jana na hadi sasa hawajalipwa akisema dhuluma inajionyesha zaidi kwenye uuzaji... “Hivi ni kwa nini tumbaku inanunuliwa kwa Dola, pembejeo inakopeshwa kwa Dola lakini mkulima analipwa kwa shilingi, hii ni nini, ni wizi mtupu.”



Akichangia Bajeti hiyo, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM) alisema: “Mabonde mazuri yapo, lakini Waziri wa Kilimo (Christopher Chiza) ni rafiki yangu tumekuwa tukizungumza naye mara kwa mara, lakini naamini hapa tulikofika wananchi wangu wa Shinyanga ni marafiki zangu zaidi, hakuna hata skimu moja ya umwagiliaji.”



Alisema kuna mabonde ya Msalala na Solwa, yanayotosheleza kuzalisha mazao mengi kuliko Mbarali (Mbeya), lakini kinachofanyika ni kutosikilizwa kwa wananchi wa Shinyanga kwenye matatizo yao.


Maige ambaye mwaka jana alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kilimo cha pamba kinaendesha maisha ya zaidi ya watu milioni 14, lakini wanaendelea kupata hasara kwa kuwa hakuna mfuko wa kuwalinda pindi bei inapoporomoka.



kp22042013.jpg
 
Kweli sisi ni Masikini zaidi ya Rwanda na tuna ARDHI; MADINI; GAS? Serikali ya CCM imeshindwa kutuondoa kwenye hili JANGA la Umasikini, lakini bado wanataka kututawala kujipa wao Wenyewe na kundi lao UTAJIRI wa kupindukia...

CCM sasa hivi sio CHAMA cha JEMBE na NYUNDO wanatumia jina hilo tu kupata kura VIJIJINI; Bila kutumia pesa kwenye Mikutano hakuna anayehudhuria... kwahiyo hawajali wananchi hata kidogo...
 
Hawa wabunge wa ccm ni wanafiki zaidi ya wachawi wanailalamikia serikali wakati wakianza tu wanaunga mkono hoja baadae wanajifanya wanaonyesha matatizo ya kilimo tunataka waikatae isipite ndipo tutajua nia zao za kweli.
 
Lembeli alisema kuna wakulima ambao waliuza mazao tangu mwaka jana na hadi sasa hawajalipwa akisema dhuluma inajionyesha zaidi kwenye uuzaji... "Hivi ni kwa nini tumbaku inanunuliwa kwa Dola, pembejeo inakopeshwa kwa Dola lakini mkulima analipwa kwa shilingi, hii ni nini, ni wizi mtupu."

Nimependa hiki kipengele............, Kinana,Nape juzi mlikuwa mnabariki wizi moro sababu mwajua hatujui linaloendelea, nyie kazi yenu kula vitumbua vya bure wabunge makini wakiibua uozo eti ohhh mnawapotosha wananchi kwamba CCM inalinda maslahi yetu.......ndio haya maisha bora mimi nahisi nyie mnazunguka huko mikoani kuchukua hesabu kwa wahindi mliowapa viwanda kwa ufisadi na kufifisha mawazo ya wanyonge......nikiwakamata 2015.
 
wanategemea nini kwa serikali na Rais dhaifu kama Kikwete????
 
Hakuna wabunge wanafiki kama magamba wakiwa mbungeni,wanalalama bungeni kuhusu majimbo yao alafu wanaunga mkono hoja 100% sasa unabaki unajiuliza kinachowatoa mapovu alafu unaunga hoja ni nini,inamaana umeridhia na sera mbovu za serekali ili hali unamahitaji jimbon kwako...akili ndogo zinatawala
 
CCM sio chama cha jembe na nyundo tena, hiki chama sasa ni tools za kutolea meno na kucha,rasilimali zote hizi tu wapili kwa umaskini? Beno Ndullu na boss wake JK wanaongepea kuwa uchumi unaimarika kumbe sanaa tupu,madog nao bungeni hawajadili jinsi Nchi inavyokwenda wanamjadili mtoto mchanga wa Slaa, mfuga madog nae ametulia kwenye kiti utadhani anatongozwa.....hii Nchi hii.......siku ya kuizika CCM nitacheza mdundiko juu ya kaburi lake.
 
Wabunge wa ccm kama Maige wamekumbuka shuka asubuhi,
Haya anayoyasema yalishasemwa sana na wapinzani Maige akiwa waziri lakini alikua anachekelea tu na alikua busy kutorosha Twiga.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom