Wabunge wahofu Rais kuingizwa kwenye ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wahofu Rais kuingizwa kwenye ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Friday, 11 November 2011 21:20[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Kizitto Noya,Dodoma

  WABUNGE wamehadharisha kwamba Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2011, ‘utamwingiza Mkenge’ Rais, endapo kipengele hicho hakitaondolewa.

  Kipengele hicho kinamtaka kiongozi huyo wa nchi kuthibitisha manunuzi ya mbalimbali.Wakichangia Muswada huo kwa nyakati tofauti, wabunge hao walisema baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu wanaweza kutumia fursa ya kumshirikisha rais, kufanya ufisadi na baadaye kashfa kubaki kwa rais aliyeidhinisha matumizi hayo haramu.

  Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafu, alitaka kipengele hicho kiondolewe ili rais asihusishwe kuidhinisha manunuzi, kwa kuwa mazingira ya Tanzania, atapata kashfa ya ufisadi."Kwa kipengele hiki, kuna watu watamwingiza mkenge rais na sisi hatukubali rais wetu aingie mkenge. Watu watajenga maghorofa kwa kifungu hiki halafu rais atapata kashfa," alisema Seleman Jafu.

  Jafu alisema kifungu hicho kisingekuwa na tatizo endapo watendaji wote wa serikali wangekuwa waaminifu, lakini kwa historia ya Tanzania, watu watatumia saini ya rais kuhalalisha ufisadi wao.

  "Hapa kuna utata na tunapaswa pia kusema watu wakivunja kanuni tutawajibisha vipi, hata kama itatulazimu kutumia sheria za China. Kesho (jana) nitaleta amendment ya kifungu hiki cha kumhusisha rais kwenye sheria hii,"alisema.

  Jafu alisema baadhi ya watu wanaweza kutumia upungufu wa sheria, kutekeleza agenda binafsi ya kumchafua rais kwa kutumia saini yake kujinufaisha.

  "Wazo ni jema, lakini tatizo ni uadilifu,"alisema.

  Kauli hiyo ya Jafu iliungwa mkono na Subiri Mgalu, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) ambaye alisema siyo vyema rais kuhusishwa kwenye suala la manunuzi badala yake kuwekwe utaratibu mwingine.

  "Mimi nasema tusimshirikishe rais kwenye manunuzi haya. Baraza la Mawaziri lisihusike kuidhinisha matumizi,"alisema Magalu.

  Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed alisema Muswada huo wa Sheria ya Ununuzi ya Umma ni mzuri, lakini tatizo ni jinai ya kusimamia sheria.

  “Kikubwa ni uadilifu na uaminifu. Hapa Tanzania kuliwahi kutokea kashfa katika Shirika la Ndege la Tanzania, watu wakanunua ndege mbovu na waziri na Mkurugenzi mkuu wakapoteza kazi. Shida hiyo ya uzalendo na uadilifu bado tunayo Tanzania.


  “Asilimia 55 ya manunuzi yanatokana na watu kutowajibika katika kusimamia sheria. Linapotokea tatizo watu wawajibishwe haraka. Tujiulize kwenye sheria hii ni kanuni gani tunatumia kudhibiti ufisadi? Mimi kwa mawazo yangu rais angehusika moja kwa moja kwenye suala hilo la manunuzi ili kuwe na udhibiti mzuri,”alisema.

  Hamad alipendekeza njia ya kupunguza tatizo la ufisadi katika sheria hiyo mpya ya ununuzi kuwa ni kupunguza ushuru kwa vifaa vipya na kuongeza ushuru kwa vifaa chakavu.

  Mbunge Viti Maalumu (CCM) Diana Chilolo, alipinga wazo la kununua vifaa vilivyotumika badala yake akataka vinunuliwe vifaa vipya ili kuzuia ifisadi.


  Ester Matiku Viti Maalumu (Chadema) aliwataka wabunge bila kujali itikadi zao za vyama kuupinga muswada huo kwa kuwa baadhi ya watendaji serikalini hawana historia nzuri ya uadilifu.

  Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) alikiponda kifungu cha 66 cha Muswada huo kinachotoa fursa ya kununua vifaa vilivyotumika alisema: “kipengele hiki kinahitaji kuangaliwa vizuri zaidi.”

  Alisema pamoja na Baraza la Mawaziri kuthibitisha manunuzi hayo, ni bora kamati za bunge zikahusishwa kikamilifu ili kupunguza mwanya wa rushwa.

  Asumpta Mshana (Nkenge) alisema: “Siungi mkono hoja ya kununua vyombo chakavu. Hatuwezi kukaa hapa watu wazima tunazungumzia kununua vifaa chakafu. Watu hawana uzalendo, watajinufaisha na kifungu hiki.”

  Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi alipendekeza Muswada huo uboreshwe kwa sheria zake zitakazotumika ziandikwe kwa Lugha ya Kiswahili ili madiwani waelewe wanachofanya.

  "Ni bora sheria hizo ziandikwe kwa lugha inayoeleweka na ikiwezekana iwe kwa lugha mbili; Kiswahili na Kiingereza ili madiwani wajue wanachotaka kumshauri Mwenyekiti wa halmashauri,"alisema.

  Katika mchango wake, mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa aliponda kifungu cha 66 cha Muswada huo kinachotaka kutoa ruhusa kwa serikali kununua vifaa vilivyotumika kwa kuwa mawazo hayo ni ya kimaskini.

  "Hii ni poverty mentality (haya ni mawazo ya kimaskini). And I don't understand ..(na sielewi) eti sasa tunasherehekea miaka 50 ya uhuru. Tunasherehekea kitu gani kama mawazo yetu hayataki kubadilika?

  "Kipengele hiki cha kununua vifaa vilivyotumika kitupiliwe mbali, tununue vitu vipya. Mawazo hayo ni sababu ya umbwe la uongozi. Dhana kwamba hatuna fedha ni umaskini. Sisi siyo maskini ila tuna mawazo ya kimaskini, hatuwezi kupanga. yaani viongozi wa CCM mmekaa ana kutafakari kununua vitu chakavu?"alihoji.

  Naye Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu aliwatoa hofu wabunge na kuwasihi waipitishe sheria hiyo ya ununuzi wa umma akiamini kwamba mambo hayatakuwa mabaya kiasi hicho.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Tayari ni Fisadi; Hofu ya nini tena?
   
 3. k

  kada1 Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu muswaada hata mimi naona sio mzuri, hapo ni mkenge kwa kwenda mbele.
   
 4. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  kwn itakuwa mara ya kwanza kuingia au kuingizwa mkenge mbona wanajifanya wanamuonea huruma wakat ye hawaonei huruma
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sasa wanahofu nini akati tayari siku nyiiiiiiiiiiiiiiiiiiingi.
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  wanamjua mzee deal,bado wanakumbuka alivyopiga richmond
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  hakuna haja ya kupuuza hoja zote mbili wanaopinga na wanaounga mkono muswda huo. ukisikiliza kwa makini kwa sisi tunaopinga zipo hoja za wanaounga mkono ambazo tunaweza kuchota nzuri pekee na kuondoa mbaya ili muswada huo ukaye kwa maslahi yetu wote. Siamini kwamba hoja zote za wanaounga mkono ni mbaya.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nimewapenda wabunge wote walioshiriki kuuchambua muswada kipengere kwa kipengere wakisema hiki sawa na kile si sawa. Hii ndio njia bora ya kurekebisha kasoro za muswada huo.
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  HATA KAMA kuna watendaji walikaa na kuandaa muswada huo watanzania tunayo haki ya kutoa mchango wetu bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Mswada wa manunuzi sio wa CCM au CHADEMA pekee tukianza kurumbana kwa misingi ya vyama sina shaka tunawapa faida wale waliotumbukiza vipengere kwa maslahi binafsi. tutangulize utanzania mbele tujenge hoja matusi hayatasaidia kuufanya muswada ukaye vizuri kwa maslahi yetu.
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ndio maana watanzania tu wepesi kuibiwa ukileta mjadala wa Richmond hapa utasababisha wengi tutoke kwenye nafasi ya kujenga hoja za muswada wa manunuizi na wakati huo tunabishana kuhusu Richmond muswada wa manunuzi utapita na viraka kibao. Mada moja hoja moja ni mbinu nzuri ya kufunga mjadala mmoja kabla ya mwingine badala ya kuchanganya mada nyingi kwenye jambo moja.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kama umefuatilia kwa makini mjadala huu bungeni hakika ndio wakati wake na huko nyuma ulikuwa na mapungufu umeletwa wakati muafaka ili na sisi tuchangie. Huko nyuma muswada wa manunuzi uliacha mianya ya rushwa na ufisadi sasa tunataka kuondoa mianya hiyo. Tufuatilie kwa makini na kujaza hoja pale kwenye mapungufu
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wewe unaleta siasa za CCM na Chadema kwenye jambo la msingi. Inashangaza kwenye mambo ya msingi kwa taifa letu wewe unayatizama kisiasa. kwa kuwa tumeingizwa mkenge huko nyuma unataka tuache kuijenga nchi yetu?
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  siamini kama hapo ndio mwisho wako wa kujenga hoja. sasa kama ni mkenge basi mods afute post hii hatuna haja ya kujadili. muswada ukipita na viraka wewe ni mmoja wa watu wa kulaumiwa katika taifa hili unaleta mzaha kwenye mambo ya msingi. tunajadili kuondoa hiyo unayosema mkenge wewe unaturudisha kwenye mkenge. Huna tofauti na waliosababisha hiyo mikenge kwa kwenda mbele.
   
 14. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Sasa hawa wabunge wanahofu nini? Rais mwenyewe anapaswa kuilinda nafasi yake isiingiliwe na mawaa ya ufisadi; siyo sisi hapa tuanze kumlinda na kumsafisha rais. Kwetu hapa rais siyo mfalme. Anapaswa kuwajibika kwa nafasi yake na hata kwa wale anaowateua chini yake. Ile misemo ya "rais si mbaya ila watendaji wake wanamuangusha" ni misemo ya kijinga sana. Sasa kama wanamuangusha mbona hawawajibishi? Hawa wabunge waliotoa hizo hoja za kumlinda rais yaani ni hoja za kitoto sana na ni watumwa wa fikra hasa....
   
 15. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  mbona raisi anaanza kuwa fisadi kabla hajazaliwa! Nalog off
   
 16. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Awe fisadi mara ngapi?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,802
  Trophy Points: 280
  Wait a minute! Tukimpata Rais mfanyabiashara si ndio ten percent zote zitakuwa zake? Nani anatunga miswada kama hii ya sheria? Anajua analolifanya kweli?
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,995
  Trophy Points: 280
  Sijailewa kabisa hii habari.Ina maana Raisi alikuwa haushishwi kwenye manunuzi ya vifaa vya umaa?

  Yani ina maana taasisi ya urais haihusiki kabisa?

  Kama thats the case then hizo kashfa za RICHMOND/DOWANS, Rais hakuhusika?

  Ni kweli Rais hausishwi kwenye maamuzi kama haya?

  Naomba kujulishwa tafadhali.Sijailewa kabisa hii habari kwamba wanataka muswada huu wa sheria usipite ili Mh Rais asiweze kuhusishwa na ufisadi, je ina maana mara zote amakuwa akionewa ama ndo loopholes kama hizo anazitumia kwasababu anajuwa sheria haitambana?

  Tuelimishane hapa tafadhali.
   
Loading...