Wabunge wafungua kesi kupinga DOWANS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wafungua kesi kupinga DOWANS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUKUTUKU, Feb 23, 2011.

 1. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Katika hali inayodhihilisha watanzania kukerwa na malipo ya kampuni ya Dowans,mahakama kuu ya Tanzania imepokea na kusajili kesi ya kikatiba kupinga malipo hayo.

  Kesi hiyo ya kikatiba ilifunguliwa mahakamani hapo jana na watanzania saba wakiwemo wabunge watatu na kupewa namba tano ya mwaka 2011 chini ya kampuni ya mawakili ya mpoki na lukwaro.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu,msingi wa kesi hiyo ni kwamba malipo ya DOWANS ni kinyume cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sehemu ya tatu kifungu cha 27 Ibara ya kwanza na ya pili.

  Katika kesi hiyo watanzania hao wanaiomba mahakama kuu kutengua uamuzi wa malipo hayo kwa kuwa yanakwenda kinyume na katiba ya nchi.

  "Sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu,tunahurumia taifa letu na watu wake masikini wanaokosa hata huduma muhimu kutokana na hali ngumu,tumeamua kwenda kuomba haki mahakama kuu"alisema Bw.Senkoro Nzoka Mmoja wa Watanzania hao.

  Alisema kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Kifungu cha 27 Ibara ya kwanza naya pili, malipo ya Dowans ni uvunjaji mkubwa wa katiba ya nchi kwa kuwa ni matumizi mabaya ya rasimali za nchi.Alisema kifungu hicho ndio msingi wao wa kufikia maamuzi ya kufungua kesi hiyo wakiwawakilisha Watanzania.

  Uchunguzi wa Majira ulibaini wabunge watatu wanaowawakilisha wenzao katika kesi hiyo kuwa ni mbunge wa Kibakwe, Bw.George Simbachawene, Bi.Anjera Kairuki pamoja na Bw.Gosbert Blandes wote wa CCM.

  Source:
  Majira 23/02/2011, pp 1&4

  My take
  Hakuna kulala kwa suala la Dowans,uwe CCM,uwe CHADEMA,au CUF,tuungane sote kwa pamoja kama watanzania kuhakikisha haki yetu kama watanzania inapatikana.
   
 2. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huo ni unafiki huwezi kuwa ccm then unapinga ufisadi, kama kweli wana uchu na chi hii wajiuzulu na kujiunga na upinza, ni katika ccm kuifanya hoja kutoilipa dowans ni ya kwao, ile hali ccm ndio wamiliki na wanaolazimisha dowans kulipwa.

  Haiingii akili kusikia leo wanakwenda kufungua kesi hizi ni propaganda tu.

  Ni jambo la kushangaza eti ccm wanasema hoja ya katiba mpya ni yao kumbe baada ya kuzidiwa na wananchi, kwa shingo upande wanakubali katiba kubadilishwa.

  Hawa jamaa ccm ni wanafiki wakubwa, hata hii ishue ya umeme ni planned na walitaka kurudisha hela yao waliyotumia kwenye kampeni.

  Mimi siwaamini hao wanaccm wanaotaka dowans islipw, ni danganya toto tu, hii hela inaenda kwa ccm na wamafia wake, msituchanganye tushawajua siku nyingi,

  hakuna kulala mpaka kieleweke!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  Peoples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa hili tuwaunge mkono mkuu,labda ndiyo mwanzo wa wao kujiunga na upinzani,maana sasa kuna mgawanyiko mkubwa sana ndani CCM!!
   
 4. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  1. hoja ya kafulila (umeme)imetekwa na january makamba,hoja ya john mnyika (katiba) imetekwa na hao hao ccmizi.
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  WANAFKI TUU HAO WAMEJIPANGA KUMSAFISHA jk MSIWASIKILIZE WANATUCHEZEA
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0

  KAFULILA NI MAMLUKI WALA USIMUAMINI NAHISI ALIPEWA CHOCHOTE,MNYIKA BADO ANAENDELEZA LIBENEKE

  mpaka kieleweke
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nchi yetu kweli shamba la bibi!!! wewe utumie umeme wa watu ati usilipe kwa sababu ya katiba? mnatakiwa kushitaki viongozi wenu... sio kutolipa DOWANS ambao wamefanya kazi yao kama walivyotakiwa.
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu lengo letu la kutoilipa Dowans si litakuwa limefanikiwa!tusijali tunapitia njia gani!!
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sisi hatutaki ilipwe kwa kuwa wao ndio walikuwa wa kwanza kuvunja au kukiuka vifungu halali vya mkataba mama kati ya TANESCO na RICHIMUND,Na uhalali wa wetu wa kuvunja mkaba na kampuni feki ulianzia hapo!hivyo kulipa fidia ya kuvunja mkataba si halali!!
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Peoples power wenyewe wakimwagiwa maji ya kuwasha na mabomu ya machozi wanakimbia kama upepo aisee, acheni unafiki bana !
   
 11. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sasa ndugu nani kakwambia RICHMOND ni DOWANS... hapa ndipo mnapokosea....

  wakati wa kubadilisha mkataba kama TANESCO iliridhia... hape ndipo tuliloba steps... kwa sasa DOWANS must be paid... period mengine ni mambo ya watu kujitoa waonekane tu.... everything is blablablaaa....
   
 12. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbona Arusha walikomaa,mbaka watu watatu wakapoteza maisha,kwani huo huoni kama ni ujasili wa kutosha!!
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  How in Tanzania one be in CCM and have gutts to attach "ufisadi". Hii ni gemu kama ilivyokuwa gemu ya kumleta mtu na Kujifanya ni mmliki wa Dowans.

  CCM iliishapoteza siku nyingi public trust hasa yanapokuja maeneo ya ufisadi maana watanzania wote wanajua kuwa nchi yao inasumbuliwa na kirusi kibaya sana cha kudumaza maendeleo yao kinachojulikana kama CCM.

  Hawa jamaa wameitwa na kupewa go ahead ya kufungua hii ze komedi ya kunajisi mahakama na mfumo mzima wa sheria. Dowans ya bwana jumbe, mahakama ya bwana jumbe, wabunge wa bwanajumbe, na hukumu ni lazima iwe ya bwana jumbe, hakuna jipya hapo. Hii mikakati wanayoifanya kuelekea 2015 haitazaa matunda.

  The only way to convince the public ni kumkatama RA, EL na huyo anayejiita mmiliki na pia kuhakikisha kuwa kabla ya 2015 85% ya wananchi wana ajira, umeme wa uhakika, maji safi. Otherwise ni ule ule mchezo wa ada kadabla!.
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Assume una kampuni yako:- yenye kitengo cha manunuzi, wafanyakazi wako wa manunuzi wakapiga fraud na wakatoa a bindina Purchase Order... i mean iliyosainiwa na signatory wote..kampuni lilipewa Purchase Order halihusiki na uduwanzi wenu wa ndani ya kampuni yako... hilo kampuni lazima lilipwe kwa kuwa limepewa purchase order halali na limetekeleza kulingana na Purchase Order... the rest ni siasa tu.

  Wanasiasa wanao-angalia mbali hii ni cheap popularity ambayo inafifia muda si mrefu, hivyo hutawasikia wakiingilia hili jambo.
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu nachofahamu mimi ni kuwa DOWANS iliinunua RICHIMOND,na kuridhi madeni na mikataba yote ya RICHIMOND na hakukua na mkataba mpya kati ya TANESCO na DOWANS!Wewe unaelewaje sakata hili kwa kifupi?tuelimishane mkuu!!
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mkuu mimi siiamini CCM kama chama cha siasa, lakini naamini kuna watu wachache makini, ambao wanafunikwa na wababaishaji wengi.

  Pengine hao wachache waliofungua kesi ni baadhi ya wale wachache ambao ni makini! Unaonaje hapo mkuu?
   
 17. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na watu ambazo zitasaidia kupambana na hao mafisadi pamona na wapambe wao, bila kujali hata kama ni wanachama wa CCM au sivyo.

  Wenzetu wa Misri, Tunisia, Libya, Bahrain na kwingineko walikusanyika na kudai mabadiliko bila kuweka mbele maslahi ya vyama vya siasa, ndipo wakafanikiwa.

  Leo ukisema hutaki watu wa CCM wapendao mabadiliko waungane na wazalendo wengine huoni ndio utakuwa unakosea?

  Hakuna mwenye hakimiliki ya kudai mabadiliko. Kama watu wa CCM nao watadai haki ya kweli basi nao wakaribishwe na kutiwa moyo.

  Kesho ni Mwanza. Inatakiwa hata wa CCM na wasio na vyama waende kuandamana...
   
 18. s

  salisalum JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi mkuu. CCM kuna mgawanyiko mkubwa. Wakipinga kulipa Dowans tayari wako na sisi kiroho, na nadhani hilo ni muhimu zaidi.
   
 19. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Colleagues,

  I do not see any true judgement to come out from our as far as DOWANs is concerned. JK has strategically organised his government in a way that no right will be granted by the High court to ruin his power. The presence of Othman and Wirema in those positions are there to make sure that the gvt of JK is defended in any way possible. The same applied to security whereby Shimbo and Mwema (in addition to Waziri mambo ya ndani). These ones are ready to demolish any mobilised demonstrations more than Gadaffi in Libya.

  My take: Only people's power that would do to change and bring the true Tanzania of Mwl Nyerere for those days. To my view yet people's power is far to reach since tanzanians are still devided in 'udini', 'uchama' and 'ujimbo'. Once we are all on the same page, true revolution is possible. Let's try and dare to do it!!
   
 20. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,742
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Nani amekutuma kuuleza upumbavu huu? Nenda kijijini kwenu ukaone maisha watu wako wanaishi ndio urudi hapa utuambie tulipe hiyo DOWANS mav%%&***#@#. Wamefanya kazi gani? kutudanganya? Chukua wewe hiyo mitambo ukaihifadhi nyumbani kwako utapata umeme full usituletee hadithi za abunuasi hapa. Yes i said unakera na unaudhi na majibu yako mbofu mbofu.
   
Loading...