Wabunge wafungua kesi kupinga DOWANS!

Hivi serikali bado imekomalia kuwalipa hawa jamaa? Maana enzi za sakata hili serikali ilisema ingetumia wataalamu na wanasheria wake ili kulitazama suala hili kiufundi zaidi, ili ikiwezekana fedha hizo zisilipwe, au la la zilipwe kidogo. hapa naona km vile tunaelekea kulipa!

Hivi serikari ni nani hasa!!! .....katika hili suala la Dowans, serikari ni watu. Wetu wenyewe ni sisi na kwa vile sote hatuwezi kwenda Magogoni wameteuliwa (WATEULE) wenzetu wachache kwa niaba yetu na hawa ndio wenye DOWANS.
Kwa maana nyepesi ni kuwa pamoja na pensheni na mafao mengine tunayowapa (out of our sweat) hawajaridhika nayo na wanajiongezea kwa kuilipa dowans ...amabyo ndio wao wenyewe.
Je, haya ni matatizo ya kawaida au ni laana!? Tuendelee kuzunguka mbuyu tu!!!
 
Source:

Thread kama hii iliwahi kuwekwa hapa JF miezi kama mitatu iliyopita. Leo imekuja vile vile. Kesi ile ya awali ilifutwa imefunguliwa nyingine? Au ni ile ile? Na mpaka sasa imefikia wapi?
 
Ninamashaka na hawa wabunge! Hili linaweza kuwa ni changa la macho tena la kutufanya tuone ccm hawakotayari kulipa while on the other hand wapo tayari. Tutasikia mengi sana watz.
 
Yooote yazungumzwe humu, lakini alichokifanya Chenge ni zaidi ya Usaliti! Sijui ni kwanini JK anamwogopa huyu jamaa! Kama nchi nyingine mtu kama huyu ananyongwa tu.
 
Huu ni usanii mwingine wa wabunge wa CCM kutafuta cheap populality.

Kwa mtindo huu DOWNS badala ya kulipwa mil 90 itaishia kulipwa mil 180 mark my words.

Mkataba katika ya TANESCO na DOWNS unasema explicity kwamba shauri lolote kati ya TANESCO na DOWNS likishaamuliwa na ICC then hakuna mahakama yeyote ile inayoweza kutengua au kuilisikiliza upya. (huu ndiyo mkenge alio-sign JK na serikali yake).

Haya yote yanayofanyika ni maigizo at the end of the day DOWNS italipwa tena na RIBA (Huu ndio ukweli watanzania inabidi muuelewe hata kama ni mchungu kama chloroquine). The sooner the better lpieni pesa ya watu. Kama ni matapeli mlitakiwa mulifahamu hilo from the beggining, hiyo sio kazi ya mahakama.

The best they can do hao wabunge wa CCM kwa watanzania ni kuishinikiza serikali ya CCM kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu wale wato waliotuingiza kwenye mkenge huu (read ufisadi).

Lakini nani ana ubavu huo? Wakati mkuu mwenyewe JK kwanza ndiyo anawapa vyeo hao akina Bashir Mrindoko waliotuingiza kwenye ufisadi huu.

Hakuna mwa-CCM wa kupigana na ufisadi kwasababu MIZIZI yake ni IKULU ya Jakaya Mrisho Kikwete. Jukumu lililobaki ni moja tu kwetu watanzania kuindoa CCM pale MAGOGONI faluire do so we are doomed!
 
Sasa ndugu nani kakwambia RICHMOND ni DOWANS... hapa ndipo mnapokosea....

wakati wa kubadilisha mkataba kama TANESCO iliridhia... hape ndipo tuliloba steps... kwa sasa DOWANS must be paid... period mengine ni mambo ya watu kujitoa waonekane tu.... everything is blablablaaa....

Kwa taarifa RICHMOND = DOWANS = SYMBION
Ni yule yule RA na matapeli wenzake katika kuwanyonya na kuibia wazalendo
 
Sasa ndugu nani kakwambia RICHMOND ni DOWANS... hapa ndipo mnapokosea....

wakati wa kubadilisha mkataba kama TANESCO iliridhia... hape ndipo tuliloba steps... kwa sasa DOWANS must be paid... period mengine ni mambo ya watu kujitoa waonekane tu.... everything is blablablaaa....
Hivi ninyi mnaotaka Dowans ilipwe ni kwamba mnaijua sana sheria au mnaiogopa sana?Kama mnadhani Dowans wanastahili kulipwa ni bora mkawashauri hao mafisadi wailipe kupitia mifuko yao wenyew!Ila Nchi kama nchi haistahili kuilipa Dowans!Hivi mnataka kujifanya hamuoni maisha wanayo ishi wakulima huko vijijini mwenu?Yet you have the audacity to claim for Dowans payments!shame upon you!
 
Katika hali inayodhihilisha watanzania kukerwa na malipo ya kampuni ya Dowans,mahakama kuu ya Tanzania imepokea na kusajili kesi ya kikatiba kupinga malipo hayo.

Kesi hiyo ya kikatiba ilifunguliwa mahakamani hapo jana na watanzania saba wakiwemo wabunge watatu na kupewa namba tano ya mwaka 2011 chini ya kampuni ya mawakili ya mpoki na lukwaro.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu,msingi wa kesi hiyo ni kwamba malipo ya DOWANS ni kinyume cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sehemu ya tatu kifungu cha 27 Ibara ya kwanza na ya pili.

Katika kesi hiyo watanzania hao wanaiomba mahakama kuu kutengua uamuzi wa malipo hayo kwa kuwa yanakwenda kinyume na katiba ya nchi.

“Sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu,tunahurumia taifa letu na watu wake masikini wanaokosa hata huduma muhimu kutokana na hali ngumu,tumeamua kwenda kuomba haki mahakama kuu”alisema Bw.Senkoro Nzoka Mmoja wa Watanzania hao.

.

Source:
Majira 23/02/2011, pp 1&4

My take
Hakuna kulala kwa suala la Dowans,uwe CCM,uwe CHADEMA,au CUF,tuungane sote kwa pamoja kama watanzania kuhakikisha haki yetu kama watanzania inapatikana.

sikubaliani nawe kuwa hili la Dowans hao wezi wa ccm wanadhamira ya kweli. . . . Ccm ni wezi, ccm ndio waliomtishia Sitta kuwa ananyang'anywa kadi kisa sakata hilo . Upuuzi wao haumithiliki , Hekima zao ni sawa na hekima ya Kunguru. . . . . . Acha fikra kua hao ccm kuna mpinga ufisadi.
 
Hao wambunge wametumwa na watu walio nyuma yao. Huo ni unafiki tu. Watoke CCM kwanza CCM ili waweze kupinga UFISADI.
 
Back
Top Bottom