Wabunge wa upinzani wana uwezo wa kutetea wananchi kuliko wa CCM

wogakuria

JF-Expert Member
Aug 15, 2018
743
1,223
WABUNGE WA UPINZANI WANA UWEZO WA KUTETEA WANANCHI KULIKO WA CCM.

Na Thadei Ole Mushi

Wakati Ester Bullaya mbunge wa upinzani anapoteza Muda pamoja na Fedha kwa ajili ya kutetea maslahi ya wastaafu na watumishi nchini Waziri na Mbunge wetu wa CCM amesema hadharani kuwa wao CCM wapo kwa ajili ya matumbo yao. Haya ni matusi ya wazi wazi kwa wananchi, ni matusi kwa walipa kodi ni kejeli kwa mtu ambaye Leo au Jana amepoteza maisha kwa kukosa fedha ya kujitibu.

Hiki ni kiburi cha hali ya juu kabisa kuwahi kukiona, na ndio Tunavyotafsiriwa sisi ccm.

Inductive reasoning inatutaka ku draw conclusion from particular to general.Ndio maana nasema kama Kigwangala ni mbunge wa ccm na ni waziri wetu basi wabunge wote na mawaziri wote wanahangaikia matumbo yao sio wananchi. Kama Kigwangala anafikiria hivi PhD Holder vipi kuhusu ambao hawakufika ngazi za juu za Elimu?

Tunaenda kupigwa tena na upinzani kwa wananchi hii agenda ya mafao wanaipigania haswa kama walivyopigania ile ya Korosho na mpaka sasa Zitto ndiye Mshindi kwenye Korosho. Hapa Bulaya na wapinzani wataibuka tena kidedea.... Niliwahi kuhoji CCM inakosa watu Smart wa kudeal na agenda za wananchi.

Wanashindwa kumsaidia Rais kwa kila hali. Kungekuwepo watu Smart nyuma ya Rais wetu asingelipata upinzani huu anaoupata kwenye jamii.

Rais anafanya mambo makubwa kweli lakini wa chini yao wanahangaika na ugali wa matumbo yao. Wanashindwa kumshauri....

Huwa nashangaa CCM huwa tunashindaje wakati matatizo ya wananchi wanayopigia kelele huku mtaani hatujawahi kusimama nayo hata kidogo.

Ninashauri kila Siku kuwa badala ya polepole kuhangaika na madarasa ya Itikadi awasemee wananchi kwenye agenda zinazohit kama hizi. Wastaafu hawa ni baba na mama zetu na kwa taarifa yenu karibia kila familia hapa nchini ina Mtumishi wa Umma ndiye anayealisha na kuwavisha, ukigombana na mtumishi umegombana na karibia robo tatu ya wapiga kura.

Siku mtaruhusu mikutano ya hadhara mmtaliona hili, endeleeni kuwekeza kwa wanaotafuta ugali wa matumbo yao kama kina Mtolea na wengineo.

Inaumiza sana.... Kiongozi wa Umma lazma uchague kauli za kuwajibu watu. Wao ndio wamekupa hilo V8 na mshahara wako nk.

Ole Mushi
0712702602
 
Kigwangala ni daktari wa binadamu (alikuwa) si PhD holder. Kuweka sawa
 
Back
Top Bottom