Wabunge wa Ukraine watwangana makonde

Wabunge wa Ukraine watwangana makonde

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,141
Reaction score
143,742
Huko Ukraine yaelekea wabunge huwa wanamaliza tofauti zao za kisiasa kwa kutwangana makonde. Hebu cheki hawa jamaa wawili.....nani mshindi hapo?

Last edited by a moderator:
Hii imetokea jana tarehe 12/02/2015 kati ya Yegor Sobolev wa chama cha "Samopomochi"na Vadim Ivchenko kutoka chama "Fatherland" katika bunge la Ukraine.

Mapigano yaanza baada ya kutokubaliana kuhusu mswada kuhusu rushwa uliosomwa bungeni hapo. Wote wamepewa adhabu ya kutohudhuria bunge hilo kwa siku tano.

Wenzetu hawana mchezo kwenye bunge, Kuna cha kujifunza hapa?

Last edited by a moderator:
HICHO NDICHO WALICHOTUMWA NA WAPIGA KURA WAO WAKAFANYE BUNGENI? Maruhuni wakubwa.Wamekula hela za posho za walipa kodi bure.Wangekuwa wabunge wangu wakirudi toka bungeni ningewacharaza viboko wote wawili.
 
Mimi nilidhani wabunge wa JMT wamekutana mahala wakatwangana makonde hadharani kumbe ni wabunge wa huko wametwangana tena bungeni!
 
Huyo mwenye suti ya blue ana idea ya kupigana naona.. Maana alikuwa anapeleka makonde mahali pake lol..
 
Bunge la Tanzania ni lakilokole Sana, kupigana Bungeni ni kawaida kabisa tena kwa mataifa yenyr Demokrasia ya juu kabisa kama INDIA, USTRALIA na kwingineko, India huwa kuna wakati mkono unatembea bungeni na Demokrasia ya India ni ya kipekee hakuna Taifa lenye Demokrasia kama ya ni India.
 
Wakishapigana hivyo wanakuwa wame-achieve kitu gani?
 
Back
Top Bottom