Wabunge wa UKAWA,mnaona kinachoendelea Bungeni? Fikirini tena

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Niliwashauri humuhumu JF,kwakuwa wengi wenu mmo,kuwa mbaki Bungeni ili kulisaidia Taifa. Kulisaidia Taifa kwa kuijadili na kuiboresha bajeti. Mkanisikiliza kiduchu. Mkabaki tu kusoma Hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi yenu ya Upinzani. Mkaendelea kutoka.

Sasa,bajeti haijadiliwi Bungeni. Wabunge wa CCM waliobaki Bungeni wanafanya vituko visivyo vya heko. Kila mchangiaji anaposimama,humsifu Naibu Spika na kuwaponda bila kuwapenda wapinzani. Sanasana,Wabunge hao hueleza uoga wao wa kukatwa kodi mafao yao. Bajeti na mambo yake inawekwa kando.

Bajeti itapitishwa kama ilivyowasilishwa. Inabaki na mapengo yasiyo na malengo. Wabunge wa UKAWA,mnaona? Kwetu CCM,kutokuwepo kwenu Bungeni ni safi tu. Mawazo ya Wabunge wetu hayapingwi na wala bajeti haiguswi. Ndiyo maana,tunamweka mbele Naibu Spika kila siku! FIKIRINI TENA!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza)
 
Wao ccm wameamua kung'ang'ania Dr Tulia kila siku aongoze bunge ili kuwakomesha wapinzani wasiwepo bungeni, na sisi wananchi tunasema hao wabunge wa ccm waipitishe hivyo hivyo hiyo bajeti namba tutaisoma wote maana hakuna namna
 
Niliwashauri humuhumu JF,kwakuwa wengi wenu mmo,kuwa mbaki Bungeni ili kulisaidia Taifa. Kulisaidia Taifa kwa kuijadili na kuiboresha bajeti. Mkanisikiliza kiduchu. Mkabaki tu kusoma Hotuba mbadala ya bajeti ya Kambi yenu ya Upinzani. Mkaendelea kutoka.

Sasa,bajeti haijadiliwi Bungeni. Wabunge wa CCM waliobaki Bungeni wanafanya vituko visivyo vya heko. Kila mchangiaji anaposimama,humsifu Naibu Spika na kuwaponda bila kuwapenda wapinzani. Sanasana,Wabunge hao hueleza uoga wao wa kukatwa kodi mafao yao. Bajeti na mambo yake inawekwa kando.

Bajeti itapitishwa kama ilivyowasilishwa. Inabaki na mapengo yasiyo na malengo. Wabunge wa UKAWA,mnaona? Kwetu CCM,kutokuwepo kwenu Bungeni ni safi tu. Mawazo ya Wabunge wetu hayapingwi na wala bajeti haiguswi. Ndiyo maana,tunamweka mbele Naibu Spika kila siku! FIKIRINI TENA!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mwanza)

Kama wametoka hakuna haja kuwaambia kinachoendelea, timesheet zao zisidanganye Wao Si kufuata Tu wanachoambiwa Na Mwenyekiti Wao. Mwanza wenyewe hawataki fujo mkizingua mtapasuka Amani iwe juu yenu.
 
Back
Top Bottom