Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 892
- 1,226
Habari wana Jf,
Naanza kwa kusema ni kweli katiba imeruhusu sifa ya muwakilishi wa wananchi ajue kusoma na kuandika tu na sio degree lakini;
Matatizo ya wabunge ambao hawakupata elimu ya juu katika kujenga hoja na kutoa michango bungeni tumeyaona,wengi wamekuwa wakirusha vijembe na kusema maisha binafsi ya wenzao badala ya hoja za msingi.
Ni kweli kuna lile swali tunalojiuliza "waliosoma wametufikisha wapi"?
Ila natoa tahadhari kama muwakilishi wako wa jimbo kaishia form 4 linapokuja swala la kujadili masuala mazito yanayowahusu kama uchumi ,teknolojia ,mifumo ya elimu,mikataba mikubwa huko bungeni yeye huwa sawa na bubu anachoishia ni kugonga meza tu.
Sidhani kama mtu wa darasa la 7 anaweza kubishana na data za waziri wa fedha wakati hata decimals na percentage kwake ni msamiati
Nadiriki kusema hili limeifanya siasa ya nchi yetu kuwa ya vijembe na sio hoja ndio maana wabunge wetu wanaongea kutengeneza clip na kurushiana maneno mtandaoni.
Elimu inaweza kumpa mbunge urahisi wa kwenda nje na kukutana na wafadhili wakakaa meza moja na kuongea lugha moja ya "kimaendeleo" simaanishi kingereza na wakaelewana.
Tutake tusitake ni lazima tukubaliane na mabadiliko ya karne hii,bila elimu utaburutwa tu
Namalizia kusema sidharau ambao hawajasoma ila najaribu kumtafuta atakayehoji kitu ambacho nnachotamani ahoji.Hata vitabu vya dini vimesema "HAWAWEZI KUFANANA WALIOSOMA NA AMBAO HAWAJASOMA"
Katiba imeruhusu ila sisi wananchi tukataeee "WABUNGE WA STANDARD 7 NA FORM 4 MWISHO 2020"
Qualification entry ya ubunge mtaani iwe ni at least Diploma.