Wabunge wa CHADEMA vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CHADEMA vipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtz flani, Sep 1, 2011.

1. m

mtz flani Member

#1
Sep 1, 2011
Joined: Aug 31, 2011
Messages: 36
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
hawa jamaa ni wanamapinduzi na hakuna anayebisha kuhusu hilo, lakini kuna issue wamefanya na haijanipedeza. nawauliza kwa nini walituhadaa kukataa posho za vikao then wakarudi kwa mlango wa nyuma wakachukua? je ilikuwa ni propaganda ya kujitafutia umaarufu wa kisiasa?

2. only83

only83 JF-Expert Member

#2
Sep 1, 2011
Joined: Oct 15, 2010
Messages: 5,252
Likes Received: 445
Trophy Points: 180
................Mimi ni mwanachama wa CDM damu,naunga mkono hoja mkuu,ni bora watoe tamko juu ya hili,ama sivyo ni doa kwa chama...

3. D

Dopas JF-Expert Member

#3
Sep 1, 2011
Joined: Aug 14, 2010
Messages: 1,151
Likes Received: 18
Trophy Points: 135
Tumeshaelezwa kwa maelezo marefu na ya kueleweka na Mhe Zito Zuberi Kabwe, tatizo hatusomi au hatuelewi.
Amefafanua kuwa fomu ya kusaini kwa ajili ya mahudhurio na posho ni moja. Hivyo kuonesha umehudhuria kikao lazima usaini. Ukisaini moja kwa moja unapata posho. Alifafanua kuwa walishapeleka ombi kuwa fomu hizo zitenganishwe, labda sasa bado hawajalifanyia kazi. Usiposaini inaonesha hukuhudhuria, na usipohudhuria sijui mikutano mitatu unafukuzwa.
Kwa upande wake Zito ameeleza kuwa yeye hawatamfukuza kwani kuna njia nyingi ambazo ataonesha kuwa alihudhuria hata bila kusaini. Mojawapo ni uchangiaji. Kwa vyovyote huo ulikuwa uamuzi mgumu aliouchukua, TUNAMPONGEZA KWA DHATI.
Ni uamuzi ambao wengine wanapaswa kufuata. Ila la Muhimu labda wapiganie hizo fomu zitenganishwe ili kuwafahamu nani ni Shibuda type na nani sio.

4. Lunyungu

Lunyungu JF-Expert Member

#4
Sep 1, 2011
Joined: Aug 7, 2006
Messages: 8,836
Likes Received: 75
Trophy Points: 145
Nimeamini wewe ni MTZ Fulani maana kweli umekuja hapa na hoja ya kichovu mno.Posho hizi Mbowe kesha sema sana sana na kufafanua kwa undani .Posho hizo kuziacha kwa kususoa si jibu Chadema wanataka neno posho lifutwe kote na si kwao pekee so uelewe kwamba upupu wako hauna nafasi .Kaa tulia jenga hoja na upupu acha maji marefu hapa jamvini mkuu .

5. Kimbunga

Kimbunga Platinum Member

#5
Sep 1, 2011
Joined: Oct 4, 2007
Messages: 13,012
Likes Received: 1,817
Trophy Points: 280
Mkuu kwa nini wengine nao wasifanye kama Zitto? Wangefanya hivyo posho za vikao zingeondolewa lakini wao wanazipenda na kuzitaka. Katika hili Wabunge wa CHADEMA akiwemo mbunge wangu niliyempigia kura, Ndg. John Mnyika, wameonyesha unafiki mkubwa wa NATAKA SITAKI. Wajivue Gamba la posho mbona mwenzao Zitto amejivua kwa kutosaini?

6. Ritz

Ritz JF-Expert Member

#6
Sep 1, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 42,252
Likes Received: 4,673
Trophy Points: 280
Mkuu, mbona unataka kupotosha umma! CDM hamna Wanamapinduzi ni kikundi cha wasanii watupu pamoja na porojo

7. makwimoge

makwimoge JF-Expert Member

#7
Sep 1, 2011
Joined: Apr 14, 2011
Messages: 294
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Ni heri wazichukue Hizo Posho kwa sababu wakiziacha zinaliwa na wanamagamba,Hoja ni KUFUTWA KWA POSHO NA SIO KUZIACHA.
Hakuna sababu ya wao awawaachie hao wezi jamani eleweni kuwa hoja ni kutaka kufutwa

8. makwimoge

makwimoge JF-Expert Member

#8
Sep 1, 2011
Joined: Apr 14, 2011
Messages: 294
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
RITZ ! uwe mwelewa wewe je unajua maana ya Usanii kweli wee..................

9. Ritz

Ritz JF-Expert Member

#9
Sep 1, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 42,252
Likes Received: 4,673
Trophy Points: 280
Tafsiri fupi ni wababaishaji

10. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#10
Sep 1, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,966
Trophy Points: 280

unamaanisha nin?

11. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#11
Sep 1, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,966
Trophy Points: 280
Wanachopigania ni posho zifutwe. Na si kuzigomea. Hata ktk mapinduz huwa hawaanz wote at once, ameshaanza Zito hope makamanda wote watafata. Labda mwanzoni hawakuwaza hiyo alternative ya kutokusaini form za mahudhurio.

12. Dark City

Dark City JF-Expert Member

#12
Sep 1, 2011
Joined: Oct 18, 2008
Messages: 16,277
Likes Received: 241
Trophy Points: 160
Nilisikitika sana baada ya kusoma hiyo habari jana. Nashauri wabunge wa CHADEMA waliochukua posho watupatie ufafanuzi. Na kama kuna uwezekano wazirejeshe.

13. Ritz

Ritz JF-Expert Member

#13
Sep 1, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 42,252
Likes Received: 4,673
Trophy Points: 280
Wabunge wa CDM ni wasanii wametudanganya Watanzania kuwa watagomea posho zote bunge cha kushangaza juzi ofisi ya katibu wa bunge imetoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa hakuna hata mbunge mmoja aliekataa kuchukuwa posho wote wamechukuwa mpaka Mbowe, Msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni.
Hii ndio maana yangu kijana nadhani utakuwa umenielewa, kama wewe ni mateka wa CDM najua uwezi kunielewa

14. MtamaMchungu

MtamaMchungu JF-Expert Member

#14
Sep 1, 2011
Joined: Apr 10, 2011
Messages: 3,695
Likes Received: 507
Trophy Points: 280
Tatizo la watu wengi, wanasikiliza kidogo na hata hicho kidogo wanachosikia wanachoelewa ni kidogo zaidi. Haya mambo yameongelewa hapa tena na tena lakini bado watu hawataki kuelewa.

15. Mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo JF-Expert Member

#15
Sep 1, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 7,253
Likes Received: 244
Trophy Points: 160

na kama na wewe ni mateka wa magamba, basi huwezi tegemea ukaongea mambo mazuri kuhusiana na makamanda!

16. d

deecharity JF-Expert Member

#16
Sep 1, 2011
Joined: Nov 5, 2010
Messages: 831
Likes Received: 56
Trophy Points: 45
kaka kuwa mwepesi kuelewa zitto kasema yeye hawezi fukuzwa kwa point ya kuwa anachangia sn hoja so ht asiposign bado anapakujitetea na hasard inarecord kama unavyojua zitto mara nyingi anchangia sn sasa wengine uchangiaji wao sio sawa na wa zitto so ni bora wasign kuliko kufukuzwa bugeni.... si chadema wote wanachangia sawa mkubwa ila kwa zitto inaeleweka ni mchagiaji kwa sn so haiwezekani waseme hakuudhuria bungeni kisa hukusign wakati hasard inaonyesha kuna sauti ya zitto... point kubwa hapo form zitenganishwe.

17. nice 2

nice 2 JF-Expert Member

#17
Sep 1, 2011
Joined: Aug 10, 2011
Messages: 746
Likes Received: 3
Trophy Points: 0

hata kama ni ushabiki, punguza kidogo uongo, habari iko hapo juu na haijasema hayo unayoyasema!

18. Ritz

Ritz JF-Expert Member

#18
Sep 1, 2011
Joined: Jan 1, 2011
Messages: 42,252
Likes Received: 4,673
Trophy Points: 280
Wewe ni CDM-Kata unafuata mkumbo tu, ujui chochote nitajie basi wabunge wawili tu wa CDM ambao hawajachukuwa posho bungeni

19. Mzee

Mzee JF-Expert Member

#19
Sep 1, 2011
Joined: Feb 2, 2011
Messages: 12,971
Likes Received: 2,966
Trophy Points: 280

umeisoma barua ya Zito, ametoa ufafanuz vizur sana. Kwanin unakuwa mgumu.

20. m

mtz flani Member

#20
Sep 1, 2011
Joined: Aug 31, 2011
Messages: 36
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
kama kweli walimaanisha kile walichosema basi wangezikataa hizo posho halafu tumuone huyo mpuuzi wa kuwafukuza!nawaambia nchi ingewaka moto na mapinduzi yakweli yangeanzia hapo. but what happened?i don't support watu waoga ambao hawawezi even to stand kwenye maamuzi yao.kama zitto aliweza kwa nini wao washindwe?kama point ni kuwa zitto anachangia sana mijadala bungeni wengine wanabaki wasikilizaji sasa wana tofauti gani na zana nzima ya sitting allowance? maana kama kukaa tu na kulipwa posho basi hao ndio mwake!jamani vijana wezangu tuwe na uthubutu wa kuhoji pale tunapoona mapungufu sio kuwa na mapenzi ya upofu.kama tutashindwa kuwahoji sasa hivi wakiwa hawapo madarakani tutaweza kweli wakikamata dola?kumbukeni,tunataka kuwaondoa magamba madarakani kwa sababu wameshindwa kusimamia misingi ya utawala bora na mambo yenye maslahi kwa taifa.tuna Rais anayetoa amri zisizotekelezeka na pia kupuuzwa na watendaji wake,hatutaki kuona kitu kama hicho kikitokea kwa watu ambao tunaamini ni mbadala wa hawa magamba!

Loading...