Wabunge wa chadema na laana walioitaka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa chadema na laana walioitaka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lubaga, Apr 24, 2012.

 1. l

  lubaga Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WABUNGE WA CHADEMA NA LAANA WALIOITAKA.

  Tunafahamau fika kwamba ,chama chochote cha siasa kote duniani ,kinapo anzishwa kinakuwa na lengo la kutawala kikinuia kuwaboreshea maisha watu wake ,ingawa vyama vingi vimeshindwa kukidhi hitaji la wananchi.

  Ndiyo maana chama cha siasa kinaingia kwenye mchakato wa uchaguzi kikijinadi kupitia Ilani ya chama chake, ilani ambayo inakuwa imesheheni sera na utekelezaji wa ahadi zake , ambazo zitatekelezwa katika kipindi chao cha uongozi wa miaka mitano ili kuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo ama kuwatatulia matatizo yanayowasibu.

  Kwa hiyo, dhima ya chama cha siasa ni kushika dola na kuunda serikali ambayo itatekeleza ilani ya chama kilichopewa ridhaa ya kutawala na wananchi pamoja na kukusanya kodi kwa ajili ya maendeleo yao.

  Sasa kwa msingi huo, chama cha mapinduzi ,ccm kilipewa ridhaa na wananchi ya kutawala , ingawa hatuna uhakika kama kweli ushindi wa ccm wa mwaka 2010 ulitoka kwa wananchi” lakini tuache hilo sote tunajua kuwa Dr Slaa ama chadema waliporwa Urais , ndiyo maana hata leo tunaweza kuthibitisha hilo kwa tafsiri kwamba JK anashindwa kutekeleza maazimio ya kamati za kuduma za bunge ambazo zimependekeza mawaziri wezi wajiuzuru ,kamati hizo zimebaini uozo na uwizi mkubwa wa mabilion ya fedha ya umma.

  Uwizi wa mabilioni unaofanywa na mawaziri akina mkulo tena asiye raia wa Tanzania raia wa nchi ya Malawi ,JK anapuuza kilio cha wananchi,wananchi wanataka mawaziri wezi wafukuzwe kazi yeye anasema ni upepo unapita sawa ! ni upepo unapita lakini namuonea huruma kwa kauli zake hizo ,anatoa kauli kama vile anakufa kesho kama hatakuwepo tena baada ya kumaliza muda wake wa utawala ,basi asubiri dhoruba ama sunami inakuja ,hii ni ishara tosha kuwa jk hakuchaguliwa na wananchi kama angelichaguliwa na wananchi angeliheshimu mawazo na kilio chao ,JK alikataliwa na wananchi walimwadhibu wakamnyima kura akapata ushindi mwembamba kutokana na kuwapuuza wananchi.

  Naomba nijikite kwenye mada muhimu hapa ,watanzania wengi hawajui kuwa chama kinachoshinda uchaguzi ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kushika dola na kuunda serikali ambayo itatekeleza ilani ya chama husika ambayo ndiyo mkataba baina ya chama na wananchi.kwa maana nyingine serikali ya kikwete imeajiriwa na wananchi ambao leo wanapuuzwa na kikwete,kikwete anawakandamiza watanzania kwa kuendelea kuwalea mawaziri majizi ,kikwete anatawala kwa mabavu kwa kuwa anajua anamaliza muda wake .tunafahamu anavyo fanya na njama za kupigia chapuo Dr Asha Rose migiro kwa Lengo la urais 2015.jambo ambalo anapoteza muda maana ccm haina mvuto ni marehemu .

  Sasa hoja ya kuwalaumu wabunge wa chadema na abunge wa vyama vingine vya upinzani kwa madai kuwa wameshindwa kutimiza ahadi zao ni kutowatendea haki.,na hatuwezi kuwatuhumu wa bunge hao kwa namna yoyete ile kwa sababu wao hawakusanyi kodi kutoka kwa wananchi anayekusanya kodi ni serikali ya ccm , rasilimali za nchi nyingi ziko rehani mikononi mwa serikali ya ccm zinaibiwa na mawaziri wakishirikiana na wawekezaji wa nje na ndani ama kujimilikisha wenyewe na watendaji wao majambazi wakubwa hao bila hata huruma.

  Ikumbukwe kuwa Kwanza vyama vyote viliingia kwenye ushindani vikanadi ilani zao,bila kujali kama havitashinda ,lakini vilikuwa na matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi uliopita.

  Tundu Lissu kama wabunge wengine, wali wahidi wananchi wapiga kura wao kupitia Ilani za vyama vyao ,kama endapo wangeshinda wangeweza kutekeleza mambo kadhaa waliowahidi wananchi ikiwemo uchimbaji wa visima.hoja hapa ya msingi ni kuibana serikali ya chama cha mapinduzi iliyoshika dola itekeleze ahadi hizo.isipotekeleza iadhibiwe yenyewe kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi.

  Lakini kwa bahati mbaya sana Chadema hawa kushinda uchaguzi mkuu ,kushindwa huko hawakuweza kushika Dola ,wakakwama kuunda serikali hivyo ilani yao ikawekwa kando ikakosa nanafasi ya kutekelezwa ,ingawa baadhi ya halmashauri kama karatu wanatekeleza ilani ya chadema kwa sababu baraza la madiwani linaundwa na madiwani wa chadema .

  Kwenye halmashauri ambazo hawakushinda madiwani wengi ni jambo gumu sana kwa chama cha upinzani kutekeleza ilani ya chama nje ya kile chenye madiwani wengi

  Kwa hiyo hoja ya Tundu Lissu kwamba ameshindwa kutekeleza uchimbaji wa visima ni kumwonea ,wanachi wanapaswa kufahamu kwamba wanapo piga kura nilazima watambue isiwe kwa mbunge tu,bali ni kwa diwani ,mbunge na rais wa chadema hapo tutakuwa tumejikomboa kwahiyo kura zote ni kwa chadema wakifanya hivyo watanzania wataona mabadiliko ,kama wabunge 48 tu wa chadema wanatikisa bunge na kikwete anaogopa kukaa ikulu, je wabunge wa chama hicho wangekuwa nusu tu ya bunge zima ingekuwaje ?,na je kama halimashauri zote nchini ama nusu ya halimashauri hizo zingeshindwa kuwabana mafisadi lahasha ! kwa sasa jambo hilo ni kikwazo sana katika kutekeleza ahadi za mbunge wa upinzani. kwenye majimbo yao .sasa hivi watanzania tuamke tuache longo longo tunaliwa jamani acheni propaganda za ccm.

  Kama halimsahuri nyingi zina madiwani wa ccm, majimbo hayo yangefanikiwa kupata madiwani wa chadema ama chama kingine cha upinzani basi halimashuri zingeweza kuuda baraza la madiwani na kupata meya ama mwenyekiti wa baraza husika kupitia madiwani wake na hivyo kutekeleza ilani ya chama chenye madiwani wengi walioshika dola ya halimshauri .

  Kwa maana hiyo basi ,hata Tundu Lissu ambaye baadhi wanamulaumu kwamba ameshindwa kutimiza ahadi zake ni kumwonea ,pengine hili nadhani ni kutoelewa tu mifumo ya utendaji.Wachangiaji ni vema tukajikita zaidi kujua jambo kabla ya kuchangia hoja ,naamini kuwa hapa mjamvini .ni kisima cha chemi chemi ya maarifa na watu wengi hujifunza mambo mengi kupitia hapa na shauri tujaribu kujikita kwenye hoja uundifu zenye mantiki .na wakati mwingine watu hubadili hoja na kuanzisha hoja nyingine baadala ya kuitafauna hoja husika hadi isagike .

  kwanza Lissu pamoja na ubunge wake pale alipo anatekeleza Ilani ya ccm kama hamjui ,kwanini? kwa sababu halimashauri anayotoka ina madiwani wengi wa ccm ambao ndiyo wanaounda baraza la madiwani ,kama ilivyo huko Iringa kwenye jimbo la peter msigwa,sasa kama aliahidi kuchimba visima ilikuwa ni kupitia Ilani ya chama chake kama kingeshinda chama chake ,sasa chama hakikushinda,Tundu lissu atoe hela yake ya mfukoni achimbe visima ? wakati serikali ya ccm ndiyo yenye dhamana ya kuchimba visima kwa sababu ndiyo inayokusanya kodi na michango mingine hata kwenda kukopa madeni ya kuanzishia miradi mbali mbali ambayo leo mnalalamika kuwa deni la nje limeongezeka kutoka trion 10 hadi trion 14 .4 hizo ni hela zenu mnalipa kupitia vitu mnavyonunua ikiwemo chumvi ,kalamu ,sukari ,powertiller na vingine vingi hizo ndio kodi zenu .

  Kama CCM Hawajachimba visiama sio kosa la Tundu Lissu , ni aibu kwa ccm ,kwasababu wao ndio walipewa ridhaa ya kukusanya kodi ,sasa kodi wanazo kusanya zinakwenda wapi? Wananchi wanapaswa kuihoji serikali sio Tundu Lissu na wabunge wengine .Labda Tundu Lissu amue kuingia kwenye ufisadi akauze twiga na madini ili akachimbie visima .

  Ebu kwanza fikiria kuna mtu amewahi kuhudhuria baraza la madiwani ,kuna utaratibu madiwani wa ccm ambao ndio wengi wanaunda mabaraza ya madiwani hapa nchini,kabla ya baraza ,kikoa cha baraza la madiwani hukaa kama kamati kujadili mikakati na kupitisha mambo wanayoyataka kabla ya baraza lenyewe, je hapo unategemea nini kwa wabunge wa upinzani ambao madiwani wao ni wa chache.

  Lakini watanzania tuwe na shukrani kubwa kwa wabunge wa vyama vya upinzani wakiongozwa na chama kikuu cha upinzani chadema .hoja zinazaoundwa bungeni ni hoja zenye afya ambazo hazichagui wala hazina ubaguzi ni za kitaifa ,Tundu Lissu ataendelea kuwa jembe na wezake wakina mbowe ,mnyika ,zito, msigwa kwa wachache tu ,lakini wanapaswa kupongezwa na kuombewa .

  Sasa laana ya wabunge wa chadema waliojitakia ni kupendwa na wananchi kwa sababu wameonesha moyo kabla ya silaha kuwatumikia wananchi ,wamethubutu kujituma kujitoa kafara ,wako tayari kufa kwa ajili ya watanzania ,kama Lema alilazimaka kwenda kuishi gerezani waliko watanzania walioonewa, huko diyo kuthubutu na ipenda chadema na wapenda wa bunge wa chadema .Chadema ni roho ya mabadiliko ,mwiba wa majizi na mwanga kwa umma .
   
 2. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  A good and remarkable ideas.CHA MSINGI TUZIDI KUUNGANISHA NGUVU,2015 PIGA KURA,LINDA KURA,SHANGILIA USHINDI.
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Respect!
   
 4. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii thread, ila heading ilinistua kiaina. Very good analysis
   
 5. k

  kibaya-kenya JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkubwa hapo nimekusoma sana, ila tuendelea kuwaelimisha wabongo kwamba anaye kwamisha maendeleo yetu ni sera mbovu na ilani mbovu ya ccm ambayo ndo inatumika kama dira ya maendeleo kwa watanzania na halmashauri zetu, ndo maana wao wanatumia uelewa mdogo wa wanatz, kama ndo fimbo ya kuwachapia WABUNGE WA CDM NA VYAMA VINGINE ila tuendelee kutoa elimu mana cdm hakika kitaeleweka tu mana Mungu yupo nasi siku zote, kikubwa tuachane na swala la udini,ukanda na ukabila huu ndo mtaji mkuu wa ccm lakini wameumbuka, makamanda tusonge mbele.
  tuwatoe ccm katika mioyo yetu na nia zetu hawa ni madui wa haki na wezi wa raslimali lukuki za watz.
  WAKUBWA NAWAKILISHA.


  .
   
 6. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kama CCM wako madarakani lakini madudu yanafumuka na kutoka nje, je siku waki kaa pembeni CHADEMA itakuwa na kazi ya ziada kusafisha ndani! Viongozi wa CDM kazeni boot sisi wananchi tuko tayari tunasubiri kauli yenu tuanze kazi ya fagia fagia!
   
 7. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #7
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viva kamanda
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu hapo zaidi ya kujifariji, na hakuna nguvu ya umma zaidi ya kura za wananch
   
 9. O

  Ongeauchoke Senior Member

  #9
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unamaanisha nini kusema laana? Pengine ulimaanisha lawama? Maelezo na mawazo ni sawa lakini kichwa cha somo inapa shida.
   
 10. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  ni hadithiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii ndefu sana.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Apr 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Dah! Umenistua sana Mkubwa, hiyo heading imekaa kimtego. wakati naingia humu nilikuwa nimejaa ghadabu!
  Kumbe Mada imekaa safi.
  Hongera, CHADEMA ndiyo tumaini na njia itakayowafikisha wananchi kwenye Tanzania tuitakayo

  Mungu Ibariki Tanzania
  Mungu Ibariki CHADEMA
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kamanda nimekukubali wewe umetulia nakupanga mambo ya ukweli napia wewe hauwezi kufananishwa na magamba yeyeto ulivyo kichwa hata nape hafui dafu mbele yako wewe mkali nimeipenda sana hii maana ni kweli
   
 13. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu laiti watz wangekuwa waelewa, leo hii usingezumbua akili yako na muda wako kutoa elimu kama hii, lakini kwa kuwa ndivyo walivyoamua kuwa basi tuendelee kuwaelimsha usiku na mchana. Mpaka kieleweke, thanks a lot mkuu!
   
 14. STRATON MZEE

  STRATON MZEE Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Mimi najua si wote waliomo JF ni wazalendo. Maana kama sote tungekuwa wazalendo, tusinge comments upuuzi kama wengine wafanyavyo. Tunahitaji wana JF wenye fikra pana, zenye nia ya kuleta mageuzi ndani ya Tanzania. Tunahitaji watu wenye kuona uchungu pale nchi inapochakachuliwa, inapoliwa, inapotafunwa kama mchwa atafunavyo kijiti. Tuache kuwa na mawazo mgando ya kukebehi harakati za mageuzi.
  Viva M4C Viva CHADEMA.
  Tunaandamana na tutaendelea kuandamana kudai usawa na maisha mazuri, ikiwa ni pamoja na kutetea mishahara mizuri kwa FFU wanaoendelea kutupiga mabomu. Hata watuue, hatutaacha kutetea Maslahi yao.
   
 15. l

  lubaga Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa na tafuta gadhabu za wanamapinduzi iliwaweze kusoma ,waijadili ,watoe hoja zao na kuendeleza na jadi yetu ya kuwa elimisha watu wengine ambao hawana fursa hii ya kuingia humu mjamvini tunakutana nao kwenye vijiwe ,kweli kichwa cha habari nimefanya makusudi kuwa mtego ili hata wanaccm wajue kuwa tunajua propaganda zao.tumegundea wanatumia ujinga wa kuwadanganya watanzania .
   
 16. i

  isoko Senior Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 186
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kichwa cha habari kilishtua lakini mkubwa imetulia
   
 17. K

  Kichebwax hood Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwel cdm mwanga kwa umma.
   
 18. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cha mhimu tu wajulishe magamba wenzio kuwa kunyongwa kwao kumekaribia,tena anza na baba mwanaasha
   
 19. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  thread ilivyokaa kumbe ndani ni kigeugeu, ndivyo mtakavyotawala cdm
   
 20. S

  Shekispia JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Swafi sana mkuu kwa kudadavua mfumo hasi wa kisiasa unaleta sintomfahamu kat ya wapigakura na wapigiwa kura..tulipeleke hilo kwenye katiba mpya.
   
Loading...