WABUNGE WA CCM WAMTISHA MAGUFULI

Mugasha umesahau humu ni Jf? Unasoma kichwa cha habari gazetini unahamishia humu. Aya kasome ndani ya gazeti uje utuambie ni hoja gani hiyo..
 
Itakuwa hoja ya kukatwa mafao yao ya kiinua mgongo.

Hata hivyo ambacho wachumia matumbo hao wanasahau ni kuwa wabunge wa Ukawa wanasimamia kuwapigania wananchi wao waliowapigia kura, tofauti na wenzao wabunge wa CCM ambao wao wanapigania matumbo yao binafsi na ya chama Chao Cha Majipu.
 
Sitaki kuamini kuwa huu upuuzi ulioandikwa hapa unafanana na aliyeuleta.

JF imeingiliwa.
 
Hilo ni kweli hata prof jay kwenye wimbo wake aliwahi kusema ukitaka kuona umuhimu wa tako kalia kichwa.
 
Tafadhali mama Ndalichako jitahidi lile zoezi la utambuzi wa vyeti feki lianze....JPM amesema pesa ya kuwapa NEC kwenye chaguzi za marudio ipo.
 
Wabunge wa CCM wanaweweseka nani ataweza kubishana na watawala kuhusu kodi kwenye mafao? Walitaka wasimame nyuma ya ukawa kupinga!! Sasa wamewekwa wazi wamefyata! Chama kwanza!
 
Watishia kutoka nje ya bunge,wawalila ukawa
"kwenye hoja hii, tumefanya kosa kubwa kuwapoteza ukawa, naamini wangekuwa ndani wangetusaidia kulisema tofauti na sisi ambao wengi wetu ni waoga kusema ukweli"

CHANZO:TANZANIA DAIMA
Mkuu, si utulie uandike kinachoeleweka? Hata kama imekurupushwa isiwe kwa mtindo huu sasa.
 
Bila kujali ukweli na usahihi wa hii habari, matatizo mengi yanayotokea bungeni chanzo chake kikubwa ni wabunge wengi kutokua na sifa/vigezo vya kufanya kazi nyingine zaidi ya sasa. Ndio maana kuna wakati wanajitoa ufaham kuhakikisha wanaendelea kulinda ajira.

Ndio maana hoja za kuhakiki vyeti, kuongeza kiwango cha elimu kama sifa ya kugombea ubunge, kugusa maslahi yao haziwezi kupewa kipaumbele.

Hili tu ndio eneo pekee ambalo MTU anaweza kupiga hela ndefu ya halali hata kama hajasoma.
 
Back
Top Bottom