mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
WABUNGE WA CCM MSAIDIENI MHE. RAIS.
Chama cha Mapinduzi ndicho chama kikongwe Afrika kilichobeba historia iliyosheheni mambo mazuri na mabaya. Mambo mazuri ambayo tunaweza kujifunia kama Taifa, ni kongole kwa chama na viongozi wake, kama ambavyo mambo mabaya yanahusishwa na chama hicho. Kinachonifurahisha kwenye jina la chama hicho ni neno “Mapinduzi”. Sina uhakika kama waasisi wa chama hii walimaanisha maana halisi ya neno hilo, au walikusudia vinginevyo. Kama walikusudia ile maana halisi ya neno hilo, ni vema sasa wakajitafakari, kama wako kwenye mstari ulioonyoka.
Kwa maoni na taathimi yangu, Chama cha Mapinduzi kilikuwa imara zaidi wakati wa chama kimoja kuliko wakati wa vyama vingi. Chama hiki kimewahi kufanya maamuzi magumu sana enzi hizo. Kwanza, kabla ya ujio wa vyama vingi, chama kilikuwa na itikadi na falsafa zilizowazi kabisa. Kwa mfano, nchi ikiwa inakabiliana na mambo magumu sana, chama kilikuwa kinakaa kujadili mambo kwa kina sana, na mwisho wake kuja na majawabu maridhawa. Mfano mzuri ni Mwongozo wa Chama wa Mwaka 1981, ambapo chama kilifanya uchambuzi maridhawa wa hali ya uchumi na mambo mengine na kuweka mikakati ya kukabiliana nayo.
Pamoja na kwamba bunge lilikuwa la chama kimoja, mijadala yake ilikuwa moto moto sana, ambayo ilikuwa na tija kwa taifa. Mawaziri walitakiwa kujiandaa hasa kukabiliana na maswali na hoja za wabunge. Moja ya hoja ambazo zimewahi kutikisa bunge la chama kimoja, ni Mabadiliko ya Katiba, hoja ya Tanganyika kupewa mamlaka yake n.k. Hoja ya Mabadiliko ya Katiba baadae ikaondoka na baadhi ya wabunge akiwemo Mr. Chogga (Iringa), Mwakitwange (Mbeya), Anangisye (Mbeya), Oscar Kambona na wengine, ambao walifukuzwa uanachama wa TANU kwa kutetea mamlaka ya bunge dhidi ya chama.
Kwa sasa tuko kwenye mfumo wa vyama vingi. Kwa bahati mbaya sana, tumeingia katika mfumo wa vyama vingi huku Taifa likiwa halina cha kusimamia. Vyama vya siasa vimewagawa Watanzania, na kugawika. Hata panapoibuka mijadala mizito yenye masilahi mapana ya Taifa, ni kawaida watu/wabunge kuona wanajadili mambo kwa kuvutia upande wa vyama vyao. Hili ni tatizo kubwa sana. Kwa kusema ukweli, vyama vyote vya siasa vina mambo mazuri na mabaya. Lakini kibaya zaidi ni pale ambapo wananchi hatujui nini tunatakiwa kufanya, na mwisho wa siku tumekuwa bendera fuata upepo.
Aidha hakuna ubishi kwamba serikali ya CCM ndio iliyotufikisha hapa, iwe kwa mazuri au mabaya. Tuna wajibu wa kuwasema, ama kwa kuwapongeza au kuwakosoa maana ndio waliopewa dhamana ya kuongoza. Tunapowakosoa, haina maana kwamba tuna chuki nao. Ni wajibu wetu wa kiasili. Kama nchi, bado tuko kwenye hali mbaya sana kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tuna machache ya kujivunia, na mengi ya kujutia, ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi. Tangu uhuru hadi leo, nchi haifaidiki na rasimali tulizonazo kwa sababu ya viongozi wachache ambao wametanguliza masilahi yao binafsi kuliko nchi. Unaposikia kuna mikataba mibovu na ya kinyonyaji kama vile IPTL, MEREMETA, TANGOLD, MWANANCHI, RICHMOND, ESCROW TEGETA, MIKATABA YA MADINI, SHERIA MBALIMBALI n.k ni serikali ya CCM iliyotufikisha hapa. Hakuna ubishi katika hilo.
Katika hali kama hiyo, amejitokeza Rais Magufuli (ambaye ni uzao wa CCM) ,ambaye anaonekana kukerwa na hali ilivyo. Tangu wakati wa kampeni hadi sasa, Mhe.Rais JPM hafurahishwi na mambo mengi yanavyoendeshwa. Katika hali kama hiyo, amekuwa akichukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwatumbua baadhi ya viongozi ambao hawaendani na maono yake. Sakata la hivi karibuni, ni jinsi Rais alivyoamua kulishughulikia suala la madini. Hakuna ubishi kabisaa kwamba katika sekta ya madini tunaibiwa sana. Lakini kwa bahati nzuri, tunaibiwa kisheria. Makampuni ya madini yangekuwa yanachimba na kusafirisha madini/mchanga kwa kificho ingekuwa jambo rahisi sana. Lakini sana, tunaibiwa kisayansi. Wizi wao uko ndani ya sheria.
Katika hilo, ndio maana naona kuna umuhimu sana kwa wabunge wa CCM kumsaidia Mhe. Rais. Kwa kiasi kikubwa wabunge wa vyama vya upinzani (wenye hoja nzito zenye masilahi kwa Taifa) wamekuwa wakipuuzwa, n ahata ikifikia hatua ya kufanya uamuzi, bado wanashindwa kwa sauti za “NDIO” kutoka kwa wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni. Mijadala ya mikataba ya madini imeanza muda mrefu sana. Lakini mijadala hiyo ilifikia hatua ya juu sana kwenye bunge la mwaka 2007/2008, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe (sasa mbunge wa Kigoma Mjini) aliadhibiwa vikali. Alikuwa anatetea masilahi ya nchi, lakini wabunge wa CCM wakaona ni heri kutetea chama chao kuliko nchi. Kwa msingi huo, wabunge wa CCM hawawezi kujitutumua na kudai eti wanaunga mkono hatua anazochukua Rais wakati matendo yao na rekodi za nyuma zinaonyesha wao ndio chanzo cha tatizo.
Wabunge wa CCM wanatakiwa “kuokoka” na kuamua kumsaidia mhe.Rais katika harakati zake za kujenga nchi. Wanaweza kumsaidia kwa njia nyingi sana. Moja, wabunge wa CCM wanatakiwa kuacha unafiki. Wache utetezi kwa chama na serikali hata kwa mambo ambayo hayana masilahi kwa wananchi. Wamechaguliwa na wanannchi ili kuweza kuisimamia serikali. Serikali inapofanya vibaya wanatakiwa kukemea.Wache kuwa wasemaji wa serikali hata kwa mambo ambayo hayana faida kwa wananchi. Huu ndio upendo mkuu ambao watamwonyesha Rais na wananchi wao.
Rais ni binadamu, kuna wakati naye anakosea pamoja na watendaji wake. Wabunge wasimame kwenye nafasi zao. Pili, wabunge wa CCM wana wajibu wa kutunga sheria nzuri ambazo zinakuwa na masilahi kwa wananchi. Watunge sheria ambazo zitamsaidia Mhe. Rais kutimiza adhima yake .Huu ni wajibu wao wa kimsingi. Kujipendekeza kwa Mhe. Rais, ni njia ya kumpotosha Rais kuliko kumwimarisha. Kwa aina ya uongozi wa Rais, anahitaji bunge kusimama kwenye nafasi yake ili mambo yaende sawa. Hapa nimewazungumzia wabunge wa CCM kwa sababu ni wengi, na kimsingi ndio wanaofanya maamuzi. Mungu akinijalia nitajadili nafasi ya wabunge wa vyama vya upinzani.