Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,682
- 1,234
MHE. ENG. MWANAISHA NG'ANZI ULENGE KATIKA MKUTANO WA JUKWAA LA WABUNGE WANAWAKE WA IPU
Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge ameshiriki katika Mkutano wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani unaofanyika Jijini Geneve, Switzerland Wenye Mada Kuu ya kuunganisha Sayansi na Ubunifu kwa Amani na Kesho Endelevu yaani, "Harnessing Science, Technology and Innovation for more Peaceful and Sustainable Future"
Akiongozana na Rais wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, wameshiriki Mkutano wa Jangwa la Sahara Kanda ya Afrika na Mkutano wa wabunge wa Afrika nzima wakiangazia changamoto mbalimbali za Bara la Afrika na hoja za dharura za Afrika itakayopelekwa kwenye Sekretarieti ya Umoja huo.
Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge amesema kuwa atashiriki kwenye Mabadiliko ya Kanuni zinazoongoza Umoja wa Mabunge Duniani kuhakikisha changamoto za Tanzania na Afrika kwa ujumla zinapata nafasi ya kusikika na kupatiwa ufumbuzi.
Vilevile, Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ulenge ameshiriki mkutano wa Jukwaa la Wabunge Wanawake wa Umoja wa Mabunge Duniani wenye Mada ya Kukuza na Kulinda Haki za Wanawake na Wasichana ili kutoa Haki na Amani endelevu.
Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ulenge alipata nafasi ya kuchangia kwenye Jukwaa la Wabunge Vijana wa IPU namna ambavyo Sayansi, Teknolojia na Ubunifu vinavyoweza kuchangia kuboresha na kuimarisha amani endelevu. Miongoni mwa wasilishaji Mada ni wabunge wanawake kutoka Palestina, Ukraine, Kongo, Urusi, Uturuki na nchi nyengine nyingi duniani.
"Ndugu zangu niliyoyasikia kutoka kwa Wanawake wenzetu, madhila, mateso na mahangaiko yanayowakumba wanawake wa Palestina, Ukraine na Kongo yananikumbusha umuhimu mkubwa wa kulinda tunu kubwa Mungu aliyotubariki Tanzania, AMANI yetu. Tunapaswa kuwakimbia kama ukoma wale wote wenye viashiria vya kuvunja amani yetu" - Mhe. Mhandisi Mwanaisha Ng'anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga
Kwa Upande wetu Tanzania, Mhe. Esther Matiko amewasilisha kwa niaba yetu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania kuhakikisha Tunalinda na kukuza Haki na Amani ya kudumu kwa Wanawake na watoto nchini Tanzania.