Kikao cha mashauriano TCD chaenda sambamba na falsafa ya Rais Samia ya 4R

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
981
649
KIKAO CHA MASHAURIANO CHAENDA SAMBAMBA NA FALSAFA YA RAIS SAMIA YA 4R

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, akiongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho, mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kilihudhuriwa na mawaziri na manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.

Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Chadema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ndugu Dorothy Semu, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Ndugu Joseph Selasini, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR - Mageuzi.

Upande wa Serikali, uliwakilishwa na Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, aliyemwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mhe. Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMG-20240818-WA0046(1).jpg
IMG-20240818-WA0052.jpg
IMG-20240818-WA0050.jpg
IMG-20240818-WA0048.jpg
IMG-20240818-WA0046.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240818-WA0044.jpg
    IMG-20240818-WA0044.jpg
    438 KB · Views: 3
  • IMG-20240818-WA0042.jpg
    IMG-20240818-WA0042.jpg
    541.3 KB · Views: 3
  • IMG-20240818-WA0040.jpg
    IMG-20240818-WA0040.jpg
    425.8 KB · Views: 3
Huu kwangu ni ujinga kabisa na ningekuwa Mbowe, hata hicho cheo cha uenyekiti wa TCD ningejiuzulu mara moja.

Kesho hizo picha mtaziona kwenye mabango ya kumsifia Mama halafu sijui nani atakuwa mjinga na nani atakuwa mjanja.

Wapinzani eleweni CCM hawawezi kuwapenda hata siku moja. Wanawazuga tu.

Mbowe na wenzako, kuweni na misimamo kama ya Mandela wakati anapambana. na makaburu.

Majibu ya CCM mtayaona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Nilitegemea kuona Polisi waliowatendea unyama wanawajibishwa, ila ndio kwanza kama hakuna lililotokea. Hapo ndio mjiulize hawakuwatuma na ndio maana hawachukuliwi hatua?
 
Hawa kweli Viazi,yaaan vyama vya upinzani Tanzania hakuna kwakweli.
Washasahau ya Mbeya😂😂
 
Back
Top Bottom