Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Siyo lazima wapeleke hoja bungeni. Kama wamekubaliana mawaziri wajiuzulu, basi wawaache wajiuzulu.Bungeni, labda waziri mkuu akijiuzulu ndipo mawaziri automatically watakuwa hawana lao. Mawaziri wote!
Another option ni kuwapeleka ethics tribunal.
Kuepuka bureaucracy na fedheha, bora waandike barua za kujiuzulu, mambo mengine yaendelee.
Sawa. Lakini nauliza tena, "wasipojiuzulu"; nikimaanisha kwamba, barua zao zisipokubaliwa na mwenye mamlaka ya uteuzi, hiyo "caucus" ya CCM itafanya nini?
Ndiyo maana naungana na Mag3 katika kuamini kwamba, wabunge wa CCM wameshindwa kutumia wingi wao katika kuweza kupitisha ajenda muhimu ya kitaifa. Wange-table hiyo hoja, waliyojadili ndani ya "caucus" hakika wangekuwa wame-revolutionise siasa za Tanzania. Kwani hoja yao ingeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wabunge kutoka minority camp, na hapo ndipo wangekuwa wamemtega vizuri "mwenye mamlaka ya uteuzi".
Lakini kwa hicho walichokifanya "wenyewe tu" ndani ya caucus,hakika narudia kusema ni mazingaombwe.