Wabunge wa CCM hawana mamlaka ya kumwachisha kazi Waziri; JK awatosa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM hawana mamlaka ya kumwachisha kazi Waziri; JK awatosa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Apr 21, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli kuna mawaziri wamelazimika kuachia nyadhifa zao kwa shinikizo kutoka CCM na kama ni kweli wameshinikizwa kujiuzulu ili kukinusuru chama tawala, CCM, inasikitisha, inaudhi na inatisha. Itakuwaje kile kilichoshindikana kufanywa na Bunge linalowakilisha Watanzania milioni arobaini, kiwezekane kwa CCM inayowakilisha Watanzania milioni tano!

  Hivi kuna haja gani ya kuwa na Bunge kama lengo la Mbunge ni kulinda maslahi ya chama badala ya taifa na kwa hali kama hiyo hatma ya taifa ni kwamba liko mikononi mwa chama cha siasa. Hii ina maana moja tu kwamba mihimili mikuu mitatu ya dola inayotambulika ambayo ni serikali, bunge na mahakama, sasa kwa Tanzania imeongezeka na kuwa minne pamoja na CCM!

  Tutegemee nini kutoka kwa viongozi watakaoteuliwa, je kuna tumaini lolote kwa hali kubadilika au ni kundi moja la walafi kupisha kundi lingine? Raisi anabakia kuwa yule yule, Waziri Mkuu yule yule, Bunge lile lile, Spika yule yule na woote hao ni wa chama kile kile, kitu gani kitazuia vitendo vile vile visiendelee? Watanzania amkeni, tumeliwa na tutaendelea kuliwa kama hatukugutuka!
   
 2. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Serikali nzima niya kupigwa chini.
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Kwani unaamini kuwa wabunge wote walichaguliwa kihalali na wananchi? (ukiacha wabunge maalum/kuteuliwa)
   
 4. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  wacha tuanzie panapoanzika.........
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Yawezekana ikawa kweli wako ambao hawakuchaguliwa kihalali lakini mbunge kama ilivyo kwa Raisi akishatangazwa anatakiwa awe wa wote, wanachama na wasio wanachama.
   
 6. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Good. Sasa tatizo lipo wapi kama wabunge ambao wamechaguliwa na wananchi (regardless of party affiliation) wakawawajibisha mawaziri baada ya kupokea ripoti kutoka kwa CAG?
  Labda sijakuelewa, that was a caucuss meeting ya wabunge wa CCM na wameamua kuwashikia kidete mawaziri. Only CCM MPs can do that.
  Wapinzani, hata ku-caucuss kwa ajili ya posho wameshindwa na bado wanazila kama kawaida. Only CCM Mps can change the government. Hata kama rais angekuwa Mbowe au Mtei.
  So what's da beef???
   
 7. w

  warea JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wanafanya hayo wanayofanya kinafiki ili kujikosha tu.
  Kama wanachukia ufisadi wamuwajibishe rais? walikuwa wanasubiri upinzani waanze kukusanya sahihi?
   
 8. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Nani anzungumzia mambo ya sahihi? Kwani kuna wabunge wa upinzani wangapi? Mbona hizo sahihi ukiondoa wabunge watano wa CCm bado hazijafikia idadi ya wapinzani?
  Haikuwa hoja ya wabunge wa CCM kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Hiyo ni hoja ya Zitto Kabwe.
  Wamuwajibishe rais kwa kosa gani?
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  serukamba alitoa hoja hiyo ya kuwawajibisha mawaziri kwenye caucus ya ccm hata kabla ya zito kutoa hoja yake ya kukusanya sahihi
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hivi chadema ina wanachama wangapi?
   
 11. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Swali ni kwa nini kwenye Caucus ya CCM na siyo bungeni? Je ina maana caucus ya CCM imenyakua nafasi ya Bunge? Kwa nini hii hoja ya kuwawajibisha mawaziri haikutolewa bungeni, woga gani uliwazuia? Hapo ndipo wengine tunasema, bunge letu limebakwa!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  ....Wabunge wa CCM sijui wametumia kipengele gani cha katiba ya nchi au hata ile ya CCM kuwashinikiza Mawaziri waachie ngazi. Walichotakiwa kufanya ni kumshinikiza Mwenyekiti wa Magamba Msanii Kikwete kuwatosa Mawaziri wote ambao utendaji wao umekuwa zero.

  Ni aibu nyingine kubwa kwa Kikwete kushindwa kuwawajibisha Mawaziri wake wengi ambao wamekuwa wakivurunda kila kukicha na kusubiri hadi Wabunge wafanye hivyo.

  Kilichofanywa na Wabunge hawa ni kulinda maslahi yao kati ya sasa na uchaguzi wa 2015 ili hatimaye waweze kuchaguliwa tena kwa kutumia kete ya kwamba "waliwawajibisha" Mawaziri wazembe.

  Wameona anguko la chama chao linakuja kwa kasi kubwa na hivyo kutishia usalama wao wa kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa 2015 na hivyo kuamua kukurupuka ili kulinda maslahi yao, kama kweli wanekuwa wanataka kulinda maslahi ya Tanzania na Watanzania basi wangeishinikiza Serikali yote ijiuzulu ili kupisha Serikali ya muda kwa kipindi cha miezi 12 hadi 15.
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hata mkiwaondoa hap 8 Itakuwaje bado ngumu kumeza, asilimia kubwa ya viongozi walioteuliwa na Rais wameivuruga serikali. Dawa ni kuondoa wote na kuanza upya
   
 15. mbise victor

  mbise victor Member

  #15
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kauli ya kwamba jamaa wanjiuzulu kukinusuru chama cha mapinduzi ni kusaliti wananchi hao mawaziri wanawajibika kwa maslai ya taifa kwa ujumla what is ccm by the way huu ni ufukara wa mawazo i hate this scenario mch.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Kuna styles nyingi za kulegislate!

  Unaweza kukutana na wabunge wenzako kabla au baada ya kuomba mwongozo au kutoa hoja, ukapata uhakika wa kura, au uhakika wa hoja yako kutimizwa. Hii huttumika sana na majority camps.

  Unaweza ukatable motion individually, na kupata votes kutoka kwa wabunge mbalimbali, hii ni style inayotumika sana na minority camps.

  Whatever the style, the aim is to get what you want or what you think your constituency want.
  Ila humu jamvini tunapenda sana ushabiki, tunapenda mapinduzi, which is okay as long as the laws are followed. If you don't wanna follow the laws, then you better have some muscles. Something that the oppossition lacks.
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Staili nyingi za kulegislate? Yaani caucus ya CCM inaweza kumvua cheo Waziri? Kobello, you cant be serious! The most they can do ni kumfukuza uanachama, siyo kumlazimisha ajiuzulu uwaziri na kuendelea kuula. Akifukuzwa uanachama, which would be the move that makes sense, hapotezi uwaziri tu bali hata ubunge halafu hatua za kisheria zinafuata. That is the way to deal with thieves and the like but CCM cant afford to do this because they are all thieves anyway and if they tried, nobody, I repeat nobody amongst them would survive.

  The opposition might not have the muscles but they now have the people and I am not so sure what constituency you are talking about. Mambo mangapi, pamoja na uchache wao, wamefanikisha hadi serikali kusalimu amri - peoples power si mchezo na at the rate things are moving wenye mawazo kama yako mtakuwa extinct, obsolete and irrelevant much faster than a speeding bullet. I pity you Kobello!
   
 18. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,684
  Likes Received: 639
  Trophy Points: 280
  Nadhani unafanya makusudi kutoelewa. By caucus namaanisha wabunge wenye mtizamo sawa. Kwa mfano kwenye congress ya US wana black caucuss, democratic, Repubs, Latino caucuss, women etc.

  Hata Tanzania kwa mfano wanawake wanaweza kuanzisha caucuss yao wakakutana nje ya bunge na kuamua kuintroduce a motion. Caucuss ya wanawake inaweza haitajali party affilliation, as long as there's something in common that they share.

  Na ukikutana nje ya caucuss unaweza ku-invite watu wowote unaotaka waje, kwa mfano caucuss ya kina mama/dada wanaweza kuwakaribisha wajumbe kutoka NGO yoyote wanayoitaka wakajadili issues zao.

  Kwa taarifa yko, watanzania wengi wakianza kushtukia haya mambo, you will be the extinct creature, not me!!..

  Mna mawazo mgando sana, ila mnajiona mko enlightened.
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bora uwaeleze hawa great chadema(sio great thinker),maana wakishaga ingiza kitu kichwani hawa mabwana kukitoa huwa ni kazi mno,lakini umewagonga vizuri sana hapo,wasipoelewa ni ukaid wao wa kawaida usikusumbue
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Apr 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Haa! Kobello, si wabunge hao hao wa CCM waliozuia tusijue hatima ya Richmond,Kagoda, meremeta, Tangold n.k. !!! Kwanini uwape credit kwa hili wakati wamebeba dhambi ya dhulma,wizi na ufisadi kwa vipindi viwili kwa uchache wa kusema.

  Kwani hoja inayofanyiwa kazi na wabunge 'makini na maarufu' wa CCM kuhusu mawaziri imetolewa na nani kama si wapinzani.

  Hivi Kobello, unaamini kwa dhati kuwa kuna cauccus ndani ya CCM!!! Ni ipi hiyo? ya Lukuvi kumwita na kumtisha Filikunjombe! mara ngapi wamekuwa wakikaripiwa kama primary school boys and girls.

  Hoja ya Mag3 ni kuwa bunge la Tanzania lenye wabunge wengi wa CCM limenyanga'anywa hadhi, heshima na madaraka ni kikundi cha watu 200 kinachojiita cauccus! Ya kwamba ule mhimili wa tatu sasa umekuwa mhimili wa wabunge wa CCM!
  Huoni hatari hapo?
   
Loading...