Wabunge wa CCM aibu

Wabunge wa CCM aibu

Steph Curry

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
5,936
Reaction score
4,713
Huitaji kuwa na degree kutambua upumbavu wa wabunge wa CCM.. Hichi kisa kimetokea muda huu bungeni.

Baada ya Ester Matiko kutoa hoja, sasa Naibu Spika anahoji bunge..

Naibu Spika : Wanaohafiki hoja ya Ester Bulaya (alikosea jina) waseme NDIO..

Wabunge wa CCM: Ndioooooooooooo

Naibu Spika : Samahani sio Ester Bulaya, ngoja nihoji tena "Wanaohafiki hoja ya Ester Matiko wasime ndio"

Wabunge wa CCM : "kimya"

Naibu Spika : wasiohafiki hoja ya Ester Matiko wasime sio.

Wabunge wa CCM : Siooooooooo

Ina maana wao wanapiga kura kwa kusikiliza mijadala au kusikiliza majina?? Ina maana kama jina ni la mpinzani jibu ni sio hata kama hoja hiyo inafaa. Maana mwanzo walipohoji kwa jina la Ester Bulaya waliikubali hoja..

Kuna hoja moja imetolewa jana mjengoni dodoma na mh. esther wa kambi ya upinzani akichangia hoja juu ya mpango wa suala la mazingira na haswa zaidi alijikita kwenye upande wa migodi ukiwemo huu mgodi wa norhtmara mining. acacia n.k

kuna athari zinawapata wanavijiji waishio jirani na migodi hiyo ambao wameathirika na wanaendelea kuathirika sana na mpaka wengine kupata na maafa ya kufariki kutokana na ulipuaji huo.

mh. Esther alitaka kupata maelezo ya kina kutoka serikalini/wizara ni kwa nini haichukui hatua za kuwahamisha wananchi hao kwa kwa kutekeleza kuwalipa haki yao stahiki kama fidia ili kupisha mradi huo na pia kuepuka kupata athari zitokanazo na milipuko inayofanywa na mgodi huo.

mh. Esther alitoa angalizo kwa naibu spika ndugai kuwa atazuia shilingi endapo hapatapatikana suluhisho kwa ajili ya kuwaokoa kima mama wajawazito wanao na walio athirika na milipuko hiyo kwa mimba zao kuharibika, nyumba zao kuanguka kila inapotokea shughuli hiyo ambayo inasemekana kisheria mhusika mwenye mradi alipaswa kuhakikisha kuwa wananchi walio pembeni mwa mradi huo wnahamishwa kwa kulipwa fidia ili kuwaepusha na adha hiyo. na ndipo mradi uweze kuendelea na shughuli zake bila athari kwa wananchi whausika,

Kutokana na kukosa majibu ya kuridhisha naibu spika ndugai alitumia njia ileile walioizoea ya wanaccm ili kuokoa jahazi lisizame. ndugai aliamua baada ya waziri mhusika wa mazigira kushindwa kutoa majibu yenye kueleweka naibu spika aliinusuru waizara kwa kutaka ipigwe kura kwa style yao ile walioizoea ya sioooooo ama ndioooooo na waliosema sio (ccm) wameshinda.

Kilichonishangaza ni pale wabunge wa ccm tena wachache waliskika na style yao ya siooo kwa kuishinda kura ya ndiooooo iliyosemwa na wabunge wa upinzani ambao tena kwa wingi wao mkubwa na hatimaye naibu spika ndugai akishirikiana na wabunge wa ccm kwa kusema waliosema sio wameshinda.

Kwa unafiki wao wa kuona heri ccm idumu lakini hawa vikaragosi (wananchi) wanavijiji waathirika wafe kwa kutokana na kazi ya ulipuaji(blasting) inayoendelea hapo mgodini kuliko kuiadhiri wizara husika kwa kuleta hoja ya kupiga kura ya kufanya maamuzi mepesi ya kupiga kura ya siooooo iliyopigwa na wajumbe wa ccm wachache na ndiooo iliyosemwa na wapinzani waliosikika kwa wingi zaidi ya sioo ya ccm na hatimaye spika ndugai kumaliza mjadala kwa kusema waliosema syooooo wameshinda.

Hii maana yake ni kwamba wananchi walio karibu na migodi hiyo waendelee kuathirkia , kufa, kuvunjika kudondoka kwa nyumba zao bila huruma na bila kuwalipa fidia zao.

Hii ndio serikali ya ccm inayowakandamiza wananchi bila huruma na kuwajaliwanaowaita wawekezaji..

mh. Esther alilzimika kutembelea maeneo ya migodi hiyo na kuonana na wananchi waathirika na wahusika wa mgodi huo na aliweza kukutana na viongozi wa mgodi huo ambapo waliweza kuongea mengi na hatimaye kampuni ilisema pesa za kuwalipa wananchi zipo zinawasubiri ila tatizo ni ccm kupitia serikali yake ndio kikwazo.

Hii ni aibu kubwa na udhalilishaji na uuaji wa wananchi wasio na hatia.

Tahadhari chukua hatua mapema''

Yote haya inaonyesha ni namna gani tunatumia fedha za serikali kwa maaslahi ya ccm na si yataifa. Hainiingii akilini kuwa na kundi la watu bungeni badala ya kuangalia hoja na umhimu wake kwa taifa, wanaangalia watu na umuhimu wao kwa ccm.

Lazima Ccm waondoke!.
 
Hata mimi huu upumbavu wahawa ndungu unanishangaza sana.
 
naona wameamua kufia chama na siyo raia walio watuma ama kweli ccm ni janga kuliko majanga mengine wakazane kuvuga kwenye bvr tu vinginevyo wengi hatutakua nao kwenye bunge lijalo
 
maccm yamechoka Mkuu wanachostahili ni kutupa kule na kuyasahau kabisa. Jina tu la mbunge linasababisha hoja kukubaliwa au kukataliwa!

Huitaji kuwa na degree kutambua upumbavu wa wabunge wa CCM.. Hichi kisa kimetokea muda huu bungeni.

Baada ya Ester Matiko kutoa hoja, sasa Naibu Spika anahoji bunge..

Naibu Spika : Wanaohafiki hoja ya Ester Bulaya (alikosea jina) waseme NDIO..

Wabunge wa CCM: Ndioooooooooooo

Naibu Spika : Samahani sio Ester Bulaya, ngoja nihoji tena "Wanaohafiki hoja ya Ester Matiko wasime ndio"

Wabunge wa CCM : "kimya"

Naibu Spika : wasiohafiki hoja ya Ester Matiko wasime sio.

Wabunge wa CCM : Siooooooooo

Ina maana wao wanapiga kura kwa kusikiliza mijadala au kusikiliza majina?? Ina maana kama jina ni la mpinzani jibu ni sio hata kama hoja hiyo inafaa. Maana mwanzo walipohoji kwa jina la Ester Bulaya waliikubali hoja..
 
Huitaji kuwa na degree kutambua upumbavu wa wabunge wa CCM.. Hichi kisa kimetokea muda huu bungeni.

Baada ya Ester Matiko kutoa hoja, sasa Naibu Spika anahoji bunge...

Naibu Spika : Wanaoafiki hoja ya Ester Bulaya (alikosea jina) waseme NDIO...
Wabunge wa CCM: Ndioooooooooooo
Naibu Spika : Samahani sio Ester Bulaya, ngoja nihoji tena Wanaohafiki hoja ya Ester Matiko waseme ndio
Wabunge wa CCM : "kimya"
Naibu Spika : wasioafiki hoja ya Ester Matiko wasime sio.
Wabunge wa CCM : Siooooooooo

Ina maana wao wanapiga kura kwa kusikiliza mijadala au kusikiliza majina?? Ina maana kama jina ni la mpinzani jibu ni sio hata kama hoja hiyo inafaa. Maana mwanzo walipohoji kwa jina la Ester Bulaya waliikubali hoja..

Kwamba hatma ya nchi hii imekuwa, iko na wako wanaotaka iendelee kuwa mikononi mwa hawa wajinga, wapuuzi na wapumbavu inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inakasirisha.
 
Ingawaje Siko Chama Chochote Lakini Nimeona Jinsi Uchama Unatumika Bungeni Hata Kama Kuna Jambo Lenye Maslahi Kwa Taifa Linaweza Kukwamishwa Kwasababu Ya Uchama
 
mkuu angalia tu usijekufa kwa presha na hasira tukapoteza nguvu kazi ya taifa cha msingi tukomae tu awa wapuuzi wasirudi afta oktober

Asante kipngozi kwa ushauri maana inauma mpk inaweza tengeneza sumu
 
maccm yamechoka Mkuu wanachostahili ni kutupa kule na kuyasahau kabisa. Jina tu la mbunge linasababisha hoja kukubaliwa au kukataliwa!

Mkuu hii imenishangaza sana.. Hawa sijui ni wabunge wa aina gani
 
Back
Top Bottom