Wabunge UKAWA warudishe pesa za hotel na usafiri walizopewa kwa siku zote walizogoma

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,992
Kwa kawaida kila mbunge hupewa pesa za kujikimu kwa ajili ya malazi na usafiri awapo bungeni.Sasa kwa kuwa walikuwa hawafanyi kazi yoyote ya kibunge bungeni siku zote walizosusia ina maana walikaa mahotelini bure na kutumbua bila kufanya kazi yoyote ya kibunge.

Pesa hizo wazirudishe upesi sababu lengo la kupewa hizo pesa si kulipia mahoteli na kuwawezesha kutalii Dodoma badala ya kuwa vikaoni bungeni.

Naibu Spika toa maelekezo warudishe hizo pesa za siku zote walizogoma.
 
Demokrasia ingepewa kipaumbele.......UKAWA wasingegoma......
Hakuna aliwayewazuia kuingia bungeni.Na hakuna mbunge hata mmoja ambaye mambo anayoyagomea yana uhusiano na matatizo halisi ya jimboni kwake!!!

Muulize mbunge yeyote anayegoma kuingia bungeni kama anayoyagomea ndiyo waliyomtuma watu jimboni kwake na ndiyo alijinadi kuyasemea bungeni kuwakilisha jimbo lake.Wameenda kuyatunga bungeni.

Badala ya kubeba ajenda za matatizo lukuki yaliyoko majimboni kwao wao wanazurura na kuhangaikia vitu ambavyo wapiga kura hawakuviainisha kuwa ndio matatizo majimboni kwao
 
CCM wanalia sana baada ya raiya kuwa upande wa UKAWA.
Sio kawaida yangu kupita sokoni, lakini jana baada ya kukumbuka kuwa natunda yameisha nikapita.
Nilishangaa kukuta mjadala kuhusu bunge sokoni umepamba moto na matusi ya chuki kabisa ambayo hayaandikiki hapa yakitokewa kwa Naibu spika, wabunge wa ccm na chama chao kwa ujumla bila hata woga lakini mie nikaogopa.
Ni ishara kuwa ccm imewakasirisha wananchi
 
Mtambo wa uongo ukiwa kazini.TAJA JINA LA HILO SOKO LIKO WAPI
 
Hakuna aliwayewazuia kuingia bungeni.Na hakuna mbunge hata mmoja ambaye mambo anayoyagomea yana uhusiano na matatizo halisi ya jimboni kwake!!!

Muulize mbunge yeyote anayegoma kuingia bungeni kama anayoyagomea ndiyo waliyomtuma watu jimboni kwake na ndiyo alijinadi kuyasemea bungeni kuwakilisha jimbo lake.Wameenda kuyatunga bungeni.

Badala ya kubeba ajenda za matatizo lukuki yaliyoko majimboni kwao wao wanazurura na kuhangaikia vitu ambavyo wapiga kura hawakuviainisha kuwa ndio matatizo majimboni kwao
Kazi ya Mbunge sio kutumwa tuu na wananchi Bali kutumia na akili yake. Ndio maana wabunge wengi wa ccm kwa vile hawatumii akili za xiada wako kimya maana kama alitumwa barabara na kesha uliza basi anakaa kimya.
Ukawa wanaenda extra mile mpaka kwa yale msiyoyaona kwa macho
 
Sio kawaida yangu kupita sokoni, lakini jana baada ya kukumbuka kuwa natunda yameisha nikapita.
Nilishangaa kukuta mjadala kuhusu bunge sokoni umepamba moto na matusi ya chuki kabisa ambayo hayaandikiki hapa yakitokewa kwa Naibu spika, wabunge wa ccm na chama chao kwa ujumla bila hata woga lakini mie nikaogopa.
Ni ishara kuwa ccm imewakasirisha wananchi
sasa CCM roho zinawauma wamepanic kwa matokeo haya ya fitina zao dhidi ya UKAWA.
 
RAIA gani anaweza kuwaunga mkono watu wenye akili za kushikiwa! UKAWA habari yao kwisha mitaani!
Mitaa ya wapi? Labda humo kwenu Namanyere. Mahali mbapoweza kuwa na Mbunge kama Messy na mnajiona kawaida
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kazi za kibunge ni zipi mkuu? Kupiga kimya bungeni au kugongagonga meza hata pale pasipostahili?

Kazi ya mbunge ni kuwakilisha matatizo ya jimbo anakotoka.UKAWA kususa matatizo ya majimboni kwao msemaji wao nani? Matatizo ya mabarabara,maji nk

Wao badala ya kusema waongelee hayo unasikia sisi tunataka BUNGE LIVE!!!!!!!!!! Ndicho walichotumwa bungeni? BUNGE LIWE LIVE LISIWE LIVE watu wanataka maji,wanataka barabara.Bunge live kwao ni kuona BARABARA LIVE inayoonekana jimboni na maji LIVE yanayoonekana jimboni.
 
Warudishe kwa nani? Kupinga unyimwaji wa demokrasia ni moja ya kazi tulizowatuma,, ukawa wapo kwa maslahi ya wana nchi wanyonge na sio kwa maslahi ya ccm
 
Kazi ya mbunge ni kuwakilisha matatizo ya jimbo anakotoka.UKAWA kususa matatizo ya majimboni kwao msemaji wao nani? Matatizo ya mabarabara,maji nk

Wao badala ya kusema waongelee hayo unasikia sisi tunataka BUNGE LIVE!!!!!!!!!! Ndicho walichotumwa bungeni? BUNGE LIWE LIVE LISIWE LIVE watu wanataka maji,wanataka barabara.Bunge live kwao ni kuona BARABARA LIVE inayoonekana jimboni na maji LIVE yanayoonekana jimboni.

Sanamu ya Diamond Live na Mnara wa Kumbukumbu ya Push Up Live? Au hayo sio matatizo naona hujayataja!

Sikiliza bwana mjipendekeza. Demokrasia na haki ya kupata habari ni msingi wa ustawi wa jamii. Kama leo unapata kazi ya kutusimulia uhuni wa wabunge wetu, huoni kwamba tulipaswa kujionea wenyewe ili tuwahukumu? Unaposema 'watu wanataka maji, watu wanataka barabara...' hao ''watu'' ni wewe na familia zao au unawasemea hata na wale wanaounga mkono wabunge wao kutoka nje?

Wale vijana waliodimwa UDOM, unadhani kipaumbele chao ni barabara? Jiangalie ndugu yangu, Mungu hapigwi mabomu wala hatishiwi jela...siku moja utakufa na utahukumiwa kwa unafiki wako.
 
Kwa maoni yangu, UKAWA wanafanya kazi kubwa zaidi kwa kutoka kuliko wabunge wote wa chama tawala waliobaki bungeni, na faida za wanachokifanya huwezi kuziona kama umegubikwa na blanket la uchama. Bunge lisiendeshwe remotely na Serikali, bunge liishauri serikali, bunge liikosoe serikali pale inapoyumba na bunge litunge sheria zenye tija kwa maendeleo ya wote. Kinachofanyika kwa sasa bungeni ni kulinda majina ya akina fulani, na sidhani kama hilo ndo tuliwatuma wakalifanye bungeni.
 
Kwa kawaida kila mbunge hupewa pesa za kujikimu kwa ajili ya malazi na usafiri awapo bungeni.Sasa kwa kuwa walikuwa hawafanyi kazi yoyote ya kibunge bungeni siku zote walizosusia ina maana walikaa mahotelini bure na kutumbua bila kufanya kazi yoyote ya kibunge.

Pesa hizo wazirudishe upesi sababu lengo la kupewa hizo pesa si kulipia mahoteli na kuwawezesha kutalii Dodoma badala ya kuwa vikaoni bungeni.

Naibu Spika toa maelekezo warudishe hizo pesa za siku zote walizogoma.
Mwambie mkulu atalifanyia kazi
 
Sio kawaida yangu kupita sokoni, lakini jana baada ya kukumbuka kuwa natunda yameisha nikapita.
Nilishangaa kukuta mjadala kuhusu bunge sokoni umepamba moto na matusi ya chuki kabisa ambayo hayaandikiki hapa yakitokewa kwa Naibu spika, wabunge wa ccm na chama chao kwa ujumla bila hata woga lakini mie nikaogopa.
Ni ishara kuwa ccm imewakasirisha wananchi

Hata mimi nilipita pale soko la Kibororoni, bahati mbaya wananchi wa Kibororoni hata wachukue na maiti za babu zao kura zao haziwezi kuiondoa CCM madarakani. Kwahiyo wataendelea kuisoma TARAKIMU huku wakitukana tu maana ndio uwezo wao unaishia hapo.
 
Back
Top Bottom